Mtu asiye na hela ana mawazo, ana huzuni, ana hasira, hajiamini.... Mtaishia kukwazana tu kila siku. Labda awe ameridhika na umaskini wake.
Inategemea na mazingira Mkuu.
Pesa huwa na thamani pale penye matumizi lakini Kama hakuna matumizi basi thamani ya pesa hakuna.
Wanawake wanaoishi katika majiji ndio huiona thamani ya pesa tofauti na wanaoishi vijijini au miji midogo.
Hii ni kwa sababu wanawake wa mjini hukabiliwa na changamoto nyingi za kimuingiliano, mabadiliko ya fasheni mablimbali, usafiri na masuala ya mavazi na teknolojia.
Lakini wanawake wa vijijini huhitaji mambo ya kawaida ambayo ni chakula, maji, na malazi. Jambo hili huwafanya wasiione thamani ya pesa Kama wanawake wa mjini.
Pesa haifiti maeneo mengi Sana japo wengi hufikiri ndio kila kitu.
USHAURI: Kama unatarajia kuishi mjini basi suala la pesa haliepukiki hata kwa asiye na akili. Hivyo ni wajibu wako kutafuta mwanaume/Mwanamke ambaye atakufanya uishi mjini ukiwa unaheshimiwa kuliko uishi kwa kujidhalilisha Kama kuomba omba hela wanaume za watu, kujiuza, kuvaa nguo zisizo na stara au na thamani.
Ni wajibu wenu kina Dada kujichagulia wanaume wa hadhi zenu. sio we kwenu masikini, huna elimu, huna uzuri wowote zaidi ya kujigeuza mwanasesere kwa mapambo alafu unataka wanaume tulio na hela.
Hata sisi hatutaki wanawake masikini, wasio vutia na wasio na elimu. Huwa tunawaepuka vibaya mno. Tunaona wanaweza kutuletea mikosi ndani ya familia zetu.
Pia lazima uelewe hakuna tajiri mwenye ndoto za kuwa na mwanamke masikini na wala hatuwazagi kuhusu nyie.
Ndio maana ikitokea inakuwa moja kwa matajiri 100.