Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Hii inahusu jinsi zote. Hela ndo inaweka chakula mezani, nguo mwilini, watoto shuleni, paa juu ya kichwa, heshima kwenye jamii n.k. Ukiona huna kitu halafu watu wanakukimbilia basi wee mganga. Si vinginevyo.
Hahahaaaa!!!
Eeti mganga.

JF kuna komedy huku
 
Inategemea na mazingira Mkuu.
Pesa huwa na thamani pale penye matumizi lakini Kama hakuna matumizi basi thamani ya pesa hakuna.

Wanawake wanaoishi katika majiji ndio huiona thamani ya pesa tofauti na wanaoishi vijijini au miji midogo.
Hii ni kwa sababu wanawake wa mjini hukabiliwa na changamoto nyingi za kimuingiliano, mabadiliko ya fasheni mablimbali, usafiri na masuala ya mavazi na teknolojia.
Lakini wanawake wa vijijini huhitaji mambo ya kawaida ambayo ni chakula, maji, na malazi. Jambo hili huwafanya wasiione thamani ya pesa Kama wanawake wa mjini.

Pesa haifiti maeneo mengi Sana japo wengi hufikiri ndio kila kitu.

USHAURI: Kama unatarajia kuishi mjini basi suala la pesa haliepukiki hata kwa asiye na akili. Hivyo ni wajibu wako kutafuta mwanaume/Mwanamke ambaye atakufanya uishi mjini ukiwa unaheshimiwa kuliko uishi kwa kujidhalilisha Kama kuomba omba hela wanaume za watu, kujiuza, kuvaa nguo zisizo na stara au na thamani.

Ni wajibu wenu kina Dada kujichagulia wanaume wa hadhi zenu. sio we kwenu masikini, huna elimu, huna uzuri wowote zaidi ya kujigeuza mwanasesere kwa mapambo alafu unataka wanaume tulio na hela.

Hata sisi hatutaki wanawake masikini, wasio vutia na wasio na elimu. Huwa tunawaepuka vibaya mno. Tunaona wanaweza kutuletea mikosi ndani ya familia zetu.

Pia lazima uelewe hakuna tajiri mwenye ndoto za kuwa na mwanamke masikini na wala hatuwazagi kuhusu nyie.
Ndio maana ikitokea inakuwa moja kwa matajiri 100.
Bila kujali mazingira swala la "mwenza mwenye nguvu" linabaki pale pale. Kwa kijijini hupimwa kwa chakula na kanyumba na uchapakazi. Kwa mjini hivi hupatikana kwa fedha. Mwanaume nyoronyoro ambaye kikwetu tunasema shamba lake limepotea hawezi kupata mke wa maana labda mvivu mwenzie.
 
Sijui kwanini siku zote kuna negative perception mwanamke akimpenda ama akipendwa na mwanaume mwenye pesa...nani kasema wasio na pesa ndo wana guarantee ya mapenzi ya kweli....
Always pray,ukibahatika kumpata mwenye utu hio hela yake ni tamuuu mno mana Ina complement yale mema anayokufanyia..pata asie na hela na asie na utu u will experience hell on earth...
Hayo huwa ni maneno ya wakosaji tu my dear, na wivu tu, hivi nani anataka shida humu duniani? Si basi tu!! Wangapi wanaishi stoo(chumba kimoja kila kitu humo,baba,mama na watoto pia) lakini full majuto!!

Kama hauna pesa hangaika saka zako sio kuonea wivu wenye pesa wakipendwa, huo muda wa kukaa kumuwazia mabaya ungewaza kupiga pesa si ungefika mbali, bora hata akiongea mwanamke unaweza sema anamuonea mwanamke mwenzie wivu, sasa na mwanaume tusemeje!!!
 
Hawana maana... Bora kutemana nao tu manake wanakuwa hawana tofauti na wakule Uwanja wa fisi
Hilo ndilo la msingi, tena ingeondoa hizi shida za thread mia mia humu za wanawake wapenda pesa. Temaneni nao mkasake pesa muone kama thread hazijabadili muelekeo humu.
 
Kila mwanaume ndoto yake kubwa katika mapenzi ni kuoa au kumiliki mpenzi ambaye ni mzuri wa sura na mrembo. Japo wahenga walisema mwanamke Tabia usemi huu umetupiliwa mbali na vijana wa leo wanaoamini kuwa Tabia inafundishika.

Sasa kwa maisha ya sasa na jinsi minavyowaona wadada wa kileo kama ukimiliki msichana mrembo wa kuvutia na hauna hela ujue kuna mambo mawili, kwanza yawezekana una zali la mentali, ambalo kwa miaka hii ya karibuni limepotea, pili unasaidiwa pia kula chakula cha ndoa na mtu mwingine mwenye pesa.

Ili kuondokana na kero hii njia kuu ni moja kupigana kiume, usiku na mchana kuzisaka pesa, ukizipata utapata mrembo wa aina ile unayemtaka vinginevyo kumiliki binti mrembo na mzuri wa sura ni ndoto za alinacha.

Kama wanaume tukiwa wavivu kujituma tutegemee mambo mawili kwanza kukumbatia ule useme wa mwanamke tabia na kutumia usemi huu kama kimbilio letu la kujitenga na mabinti warembo au tusubiri zali la mentali.
 
inamana mkuu wenye pesa wake zao hawaliwi?

Ifike mahali tusidanganyane mkuu mwanamke ni akuridhie mwenyewe ila swala la kumiliki mwanamke kisa pesa hapa tunafeli sana mkuu ,maana wenye pesa kila siku wanachapiwa na tunashuhudia mitaani ..

Kuwa napesa hakusababishi mwanamke wenye kujielewa kukubali

huwa tunashindwa kuelewa kuna mwanamke na kijimwanamke
 
Teh teh teeeeh!!!
Pesa muhimu sanaaaa zitafuteni tu, hayo ya kuchapiwa ni mambo mengine.
 
pesa muhimu kweli ila mtu asitafute kisa anataka kuzuiwa kuchapiwa au kumiliki mademu wakali

kupata watoto wa zuri ni bidii yako tu
Bidii hiyo inaambatana na pesa. Mwanamke huamua mwenyewe kutulia kwahiyo palipo na uhakika wa pesa na penzi la dhati atatulia tu. Mnachokosea ni ile kudhani ukiwa na pesa umemaliza, tafuta pesa(ni security) then mpende mkeo uone kama mtalialia tena.

Usitafute kwa nia ovu ya kujikusanyia wanawake,tafuta kwa nia ya kuwa na maisha bora na mkeo/wakezo(kwa waislamu) na familia yako.
 
Pesa muhimu,we huoni akina Jared Kushner wanavyowafaidi akina Ivanka Trump,jamaa angekua hana pesa angeionea wapi papuchi ya mtoto mkali na anaetokea familia ya kitajiri kama Ivanka Trump?
 
Kila mwanaume ndoto yake kubwa katika mapenzi ni kuoa au kumiliki mpenzi ambaye ni mzuri wa sura na mrembo. Japo wahenga walisema mwanamke Tabia usemi huu umetupiliwa mbali na vijana wa leo wanaoamini kuwa Tabia inafundishika.

Sasa kwa maisha ya sasa na jinsi minavyowaona wadada wa kileo kama ukimiliki msichana mrembo wa kuvutia na hauna hela ujue kuna mambo mawili, kwanza yawezekana una zali la mentali, ambalo kwa miaka hii ya karibuni limepotea, pili unasaidiwa pia kula chakula cha ndoa na mtu mwingine mwenye pesa.

Ili kuondokana na kero hii njia kuu ni moja kupigana kiume, usiku na mchana kuzisaka pesa, ukizipata utapata mrembo wa aina ile unayemtaka vinginevyo kumiliki binti mrembo na mzuri wa sura ni ndoto za alinacha.

Kama wanaume tukiwa wavivu kujituma tutegemee mambo mawili kwanza kukumbatia ule useme wa mwanamke tabia na kutumia usemi huu kama kimbilio letu la kujitenga na mabinti warembo au tusubiri zali la mentali.
Acha ujinga dogo wengine hatutafuti pesa ili tuwe ña wanawake warembo, tunatafuta pesa kwa maendeleo yetu binafsi ña kuwa ña aset ambazo zitatufaa hapo badae ña vizazi vyetu, mwanamke yeyote ni mzuri kwa mumewe, ww ukimuona hawafai mumewe anamuona mke bomba ndio maana akaamua kuishi naye, pía usihadaike ña wanawake saña kwani urembo wenyewe siku hizi ni artificial saña ambapo ukiwa na pesa tuu, hata kama mke wako ni wakaida badae ña wengine wataanza kumuona mrembo kwa kumtunza vizur ña kumpatia pasa za kununua urembo wa artificial , tafuta pasa kwa maendeleo binafsi ña c kwa sababu ya kuwa ña warembo, nahisi ni utoto tuu ukikua utaacha
 
Watu hawana pesa na wanawake wazuri wanapata.......Wanawake wanahitajika mwanaume anayejua mapenzi......handsome....mwenye maneno matamu na anauejua kufikisha kileleni.....
Pesa ni factor ndogo sana kwenye mapenzi....Unaweza kuwa nazo na kila siku hao wazuri Wanakukimbia.
 
for the record hapa uliandika pumba ila nikajua ni muhemko tu kwa my wife
Teh teh teeeeh!!!
Pesa muhimu sanaaaa zitafuteni tu, hayo ya kuchapiwa ni mambo mengine.

kushuka hapa ndio nikakutana na mke wangu kwenye ubora wake
nikaripoti kwa mods wai stick coment yako
Bidii hiyo inaambatana na pesa. Mwanamke huamua mwenyewe kutulia kwahiyo palipo na uhakika wa pesa na penzi la dhati atatulia tu. Mnachokosea ni ile kudhani ukiwa na pesa umemaliza, tafuta pesa(ni security) then mpende mkeo uone kama mtalialia tena.

Usitafute kwa nia ovu ya kujikusanyia wanawake,tafuta kwa nia ya kuwa na maisha bora na mkeo/wakezo(kwa waislamu) na familia yako.
 
for the record hapa uliandika pumba ila nikajua ni muhemko tu kwa my wife

kushuka hapa ndio nikakutana na mke wangu kwenye ubora wake
nikaripoti kwa mods wai stick coment yako
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Nimekumiss kipenzi.
 
pesa lazima itafutwe either unataka kuwa na bebe mzuri au laa!
 
Back
Top Bottom