Habari za jioni wakuu,
Kuna swali huwa najiuliza sana kwa kipindi kirefu sana katika maisha yangu na bila kupata majibu sahihi ya swali langu, kipi hasa watoto wa kike wanachokitaka, pesa au mapenzi ya kweli.
Mfano utakuta mdada ana mtu wake mwenye pesa lakini bado anakituliza roho chakepembeni na pia utamkuta dada anakituliza roho lakini anahaha kumtafta bwana mwenye pesa sasa huwa naashindwa elewa hasa hawa dada zetu kipi wanataka na je kuna uwezekano mtu kupata vyote.
Namaanisha akawa anapata mapenzi ya kweli na pesa wakati huo huo na kama inawezekana mnijuze na kama inashindikana mnisaidie ni nini hasa hawa dada zetu wanataka hasa kwenye maisha. Maana ukimkuta mwenye pesa anatafuta mapenzi ya kweli na mwenye mapenzi ya kweli anataka na mwenye pesa? Yupo alobarikiwa kupewa yote kwenye maisha.
Naombeni msada wenu katika hili naamini ntajifunza mengi kutoka kwenu,
matusi sitaki wala kejeli maana sijamtukana mtu wala kumkejeli mtu ukiona hulielewi pita tu mbali mzee.
Nawasilisha