Utaratibu wa mwajiri kutoa mkono wa pole(rambirambi) kwa mtumishi wa serikali baada ya kufiwa na mama au baba upoje?

tutunfyekyela

JF-Expert Member
Aug 31, 2021
472
768
Viongozi naombeni kujua utaratibu wa kupatia pole(rambirambi) na mwajiri(serikali) baada ya kufiwa na mzazi. Na kama upo huwa ni shilingi ngapi? Documents zipi zinahitajika ili mtumishi aweze kulipwa?
Naombeni msaada viongozi.
 
Andika barua kuomba hiyo Rambi rambi ambatanisha na death certificate au Tangazo la kifo toka Hospitali alikofia/mwili ulipohifadhiwa.
 
Nadhani haipungui milioni moja, inategemea na taasisi husika; ila ni bora mtu akusaidie/akupe mchango kwenye kuuguza kuliko akupatie pesa baada ya kupoteza mpendwa wako. Ikiwezekana achana na hayo mambo ya kuomba kulipwa, kwasababu haitarejesha uhai wa uliyempoteza.
 
Mtumishi ukifa watatoa laki moja na jeneza. Familia ya mtumishi akifa mmoja wapo watakupa kruza mkongo kusafisha mwili, jeneza na hela ya kuchmba kaburi. Pole ndugu kwa yaliyokusibu.

Nb.
Familia ya mtumish ni mwenzi, watoto na tegemezi walioidhnshwa
 
Back
Top Bottom