Utani wa makabila! Tupia wako

Utani wa makabila! Tupia wako

Kiongozi, unasikia mtu anakwambia kuwa (ashukumu si matusi), nitakukaza, leo nataka kukaza. Nimeishi tanga for 27 yrs hivyo nasema ninachokijua fika. Najua kuna kusema Mkaza mwana-hili siyo tusi ni namna ya kum address mkwe wako, correct kabisa. But upande mwingine wanasema unamtusi mtu hasa mwanamke kuwa "nitakukaza"... kama kuna kutoelewana... ni derogatory word anyway when used in that sense! I stand to be corrected!
Nukta yangu kiongozi, ni kuwa Kukaza haijawahi kuwa tusi Tanga.Hizi lugha kama,nitakukaza,nitakutia,nitakugonga,waliwa nk. si lugha rasmi za Tanga.Haya ni maneno ya Kiswahili yenye maana yake ambayo si hiyo mnayoyapachika kwayo.Kumbuka mkaza mjomba,mkaza hau,mkaza baba yalianza kutumika muda mrefu kabla ya hii tafsiri ya kihuni.Siku hizi kila neno linapewa tafsiri isiyo rasmi.Ila kama mada ilivyo ni utani tu.Huko nyuma mtanipaaa?Kazaneni kwenye mikorosho.
 
Nakubaliana na wewe , nadhani kukaza lilitokana na mkaza mwana etc kama ulivyosema hapo juu. Lakini si ndiyo tunaunda lugha hivyo, vocabrary inapanda/inaongezeka!
 
Watani zangu wapare nasikia wanakula ugali kwa picha ya Samaki hahaaha

cc; NAHUJA
Usisahau na hiki chakula bora cha kina mshana jr na dadaake NAHUJA
87d21a8d.jpg
 
Chakula very common tokea upareni mpaka Singida... Makande na makukuru au kidheri kwa wakikuyu
Ni githeri jombaa linatamkwa getheri. Kwetu ukikuyuni kwenye makande hutakosa viazi! Tunapenda viazi kishenzi utapata hadi viazi vimekaangwa pamoja na spinach afu unaletewa na Ugali pia. Hehe. Hadi kuna Ugali unasongwa na humo humo ndani kuna viazi vilivokaangwa. Unaitwa 'ngunja gutu'. Yaani nichune sikio! Taamu kweli kweli!
 
Back
Top Bottom