kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,008
- 17,383
Hapa ni pale ambapo mambo ya utani sio tu yataonekana bali yataonekana kutendeka. Watanzania wanatumia utani katika kufanikisha na kurahisisha maisha yao, kufikisha ujumbe mzito kule unakotakiwa ufike hata kama uwe mbaya, waaibu au wahatari kiasi gani. Uko utani wa makabila, kisiasa na michezo. Kuna utani pia kwenye matukio ya furaha na huzuni, ilimradi maisha ya watu yawe rahisi na bora.
Nini asili ya utani wa makabila, Simba na Yanga? Mfano, kwanini wanyamwezi ni watani wa makabila mengi ya pwani? Kwanini wasukuma na wahaya ni watani na makabila mengine vipi?
Nini asili ya utani wa makabila, Simba na Yanga? Mfano, kwanini wanyamwezi ni watani wa makabila mengi ya pwani? Kwanini wasukuma na wahaya ni watani na makabila mengine vipi?