Utamaduni wa wamarekani weusi huchangia kuwa nyuma zaidi kimaendeleo, Vitu kama muziki wao wa hiphop sio wa kuendelea kuusikiliza unasambaza sumu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Ni kweli kabisa wamarekani weusi walipitia utumwa lakini sio sababu ya wao kuendelea kuwa nyuma,

Walichobaki kukipigia kelele ni kulipwa fidia za utumwa wa mababu zao ila ni kusubiri maembe chini ya mpera, hata waafrika wenzao weusi wanaohamia Marekani wanazidi kuwachapa gepu.

Shule zipo nyingi sana Marekani lakini wamarekani weusi wamekuwa nyuma mno, Ni wengi sana hata kusoma na kuandika ni shida, mchezaji wa basket ball Lebron James kaanzosha shule kuigharamia mabilioni kaweka swimming pools, walimu wazuri sana, mgahawa wa chakula kizuri sana, n.k. lakini miaka nenda rudi shule hio wamarekani weusi wanafeli wao tu.

Hiphop nayo imechangia sana kusambaza utamaduni wa kiovu kwa wamarekani weusi, wamarekani weusi kutukuza uhuni kuuona ndio ujanja,

vijana wengi wamarekani weusi hupenda kuwa kwenye magenge ya kihalifu.

Matumizi ya madawa ya kulevya nayo yanahamasishwa sana, wamarekani weusi wengi hutumia dawa za kulevya, hata yule George Floyd aliyebanwa shingo na kukosa hewa alikuwa ni mteja wa madawa ya kulevya, na ile siku alipoitiwa polisi baada ya kukataliwa kununua bidhaa kwa noti feki alikuwa katoka kutumia Fentanyl, ni dawa ya kulevya inaongoza kwa kuua watu marekani.

Wamarekani weusi wengi huona njia za kutoka kimaisha ni michezo, sanaa ama uhalifu, hali hii imefanya wengi kuzembea shule, wamarekani weusi wengi wakienda vyuoni husomea maswala ya jinsia, arts, utangazaji, n.k. ni kazi za kawaida sana hizi, waafrika wanaohamia Marekani hasa wanaijeria hawana masihara wanasomea Udaktari, sheria, Uhandisi, IT, uhasibu, n.k. kazi zenye maokoto marefu na heshima, Leo hii waafrika wa Marekani wana vipato vikubwa kuzidi wamarekani weusi kwenye sekta ya ajira.

Wamarekani weusi huona njia ya kusuluhisha ugomvi ama kukabiliana na adui ni risasi, hadi sasa watu wanaoongoza kuua wamarekani weusi ni wamarekani weusi wenzao.
 
wanawakilisha asili ya walikotoka.

hata huku ndugu zao bado tuna hang'over ya ukoloni na utumwa.
 
Back
Top Bottom