Utajiri wa masharti ni mateso

Utajiri wa masharti ni mateso

S

Sasa kama ndio amejichanganya mitaa ya Kariakoo kwa mfano halafu gogo linapiga hodi, gari kapaki mbali itakuwaje hapo na vichaka hakuna?
hapo sasa ndio pagumu,nadhani huyu jamaa hana safari za mjini sana,,,yupo babati-manyara pale,niliwahi pewa stori yake na watu zaidi ya wa3 pale,nadhani huyu bwana hana safari nyingi za mijini na ikitokea anaenda mjini bac lzm aende na gari yake na haezi cheza mbali na gari yake hata akiwa k/koo labda awe ametoka kunya saa hiyo hiyo maana masharti yake anayajua....jina lake linaanza na herufi N kwa wakaazi wa babati pale nadhani wanamjua baadhi yao maana stori zake ni nyingi pale mjini babati
 
kuna mmoja yupo pale Iringa akihisi mkojo anapanda baiskeli anakwenda kukojoa njia panda,Da!!!!!!!!
Matajiri niliokuwa nao karibu lakini walikuwa wanaishi maishi ya shida;
1. Peter Lucas Sanga
2.Galilaya
3.Kiswele

Wote hapo juu hata soda hawajawahi kumnunulia mtu.Walikuwa wanatembea kwa miguu sana.Hawajawahi kutembelea magari ya kifahari nk
 
1.yupo tajiri mmoja hapa uyole ana bonge la kidonda mguuni haliponi miaka yote
2.yupo mwingine ana maduka ya kutosha ya hardwarw na malori aya ya transit na maghorofa lakini ukimuona muonekano wake ni kama ka jamaa flani ivi kanako anza maisha
3.mwingine usiku mzima anazichanga kwenye baiskeli hadi asubuhi
 
Kiswele ni yule aliyekua na bus zinaitwa kiswele?
Matajiri niliokuwa nao karibu lakini walikuwa wanaishi maishi ya shida;
1. Peter Lucas Sanga
2.Galilaya
3.Kiswele

Wote hapo juu hata soda hawajawahi kumnunulia mtu.Walikuwa wanatembea kwa miguu sana.Hawajawahi kutembelea magari ya kifahari nk
 
Wakuu mimi nataka hela za majini au za kutumia ushirikina maana kwa kawaida nimezitafuta nimekosa.
Naomba mwenye uelewa na hizi mishe anicheki PM anipe msaada.
Nipo tayari 100%.
 
Ni bora ukawa na Mia mfukoni lakini umeipata kwa jasho.

Nimetembea hiyo Mikoa yote ni matajiri wachache sana wanaofurahia Pesa zao.

Lakini wengi Pesa zao ni za 'ndagu' zenye masharti lukuki ambayo ni ya kujitesa tu, Usitembee na mwanamke mwingine zaidi ya mke wako, Usivae viatu zaidi ya kandambili, Usinye choo cha nyumbani n.k

Sasa hayo ni mateso ndugu zangu , Raha Pesa uifurahie na sio ikupe Karaha.
Umemuona tajiri gani anava kandambili na je kufurahia maisha ni kutembea na mke wa mtu,ina maana kwa mfano mfalme wa Saudia anayevaa sandals nae ni mwanga au Wazanzibar matajiri wanaoshindia talawanda nao ni watu wa ndago?acha kukariri kama kasuku
 
Waganga ni watu wajanja sana. Kwa masharti hayo umakuwa unabana matumizi ya fedha uliyonayo na itabaki kwenye mzunguko wa biashara tu. Utakosaje kuwa na pesa nyingi wakati unazalisha sana unakula kidogo. Tufunguke akili
Naona umenielewa vema. Basi na wewe kafanye hivyo hivyo
 
Kweli bora upate utajiri wa kibongo Duet/Startlet/bB,Cienta yako na Chumba na sebule kwenye kiwanja cha miguu 15 kwa 15 basi ,hayo mambo ya kuwa na utajiri halafu unavaa ndala kachumbari na kipensi unafunga na kamba ya katani hapana.
 
Back
Top Bottom