Tunachotakiwa kufahamu ni kuwa UTAJIRI HUNUNUA WAFUASI. Kuwa na wafusi wengi wa kutetea bila ya kujibu hoja za msingi ni dalili ya nguvu ya fedha.
Gazeti la DIRA Jumatatu inaonekana limefanya kazi nzuri ya kiuchunguzi. Dondoo halisi za 'UTAJIRI WA DAU NSSF HATARI kwa kadiri ya gazeti hilo ni kama ifuatavyo:
- Utajiri wake ni zaidi ya shilingi bilioni 100
- Utajiri huo aliupata akiwa boss wa NSSF
- Dau ana hisa nyingi katika timu ya mpira ya Uingerezaya Newcastle
- Menejiment ya NSSF chini ya Dau iliipitisha kampuni ya Dau iitwayo Derm Electrics kwaajili ya tenda za kuweka umeme kwenye majengo yote ya NSSF
- Pesa ambazo kampuni hiyo ya Derm Electrics ililipwa na NSSF - Shilingi 136,596,496 (2011), shilingi 178,691,940 (2012), shilingi 228,049,368 (2013), shilingi 343,280,613 (2014)
- Dau aliidhinisha miradi mbalimbali yenye gharama kubwa kwa maslahi binafsi
- Ripoti ya CAG akishirikiana na kampuni ya ukaguzi ya kimataifa Ernest & Young iliibua upotevu wa mabilioni ya fedha kwa mwaka 2014/2015 ndani ya NSSF
- Mtaalam mshauri wa mradi wa Arumeru alilipwa zaidi ya shilingi bilioni 400
- NSSF iliingia ubia na kampuni ya AHEL yenye mtaji wa shilingi milioni 10 (kwa kadiri ya ripoti ya BRELA)
- AHEL ilipewa mradi wenye thamani ya shilingi trilioni 7.18
- Ripoti ilibaini NSSF ilikiuka katika ununuzi wa ardhi yenye thamani ya bilioni 15.159 katika maeneo ya Madale, Mataya, Bagamoyo, Misugusugu, Ngarambe, Kibaha na Mkuranga
- Ripoti iliibua ufisadi wa shilingi bilioni 16.98 katika ujenzi wa jengo la hoteli ya Kitalii Mwanza
- Ripoti iligundua kuwa kwenye mradi wa hoteli ya Mwanza, kampuni mbili zililipwa kwa kazi za aina moja kwa kadiri ya mkataba
- Ripoti iligundua pia ufisadi katika ununuzi wa sare za wafanyakazi kwa gharama ya shilingi bilioni 1.078 kutoka kampuni ya Pink Diamond
Mimi ninaamini kama kuna uwongo kwenye taarifa hizi, Dau au NSSF watachukua hatua ya kukanusha kwa vielelezo kama walivyofanya gazeti la Dira, au kuamua kulipeleka gazeti hili mahakamani. Maana taarifa hii ipo ukurasa wa mbele wa gazeti, na wala haijatolewa kwa kujificha kama walivyojificha watetezi wa Dau ndani ya JF.
Ukimwa wa NSSF na Dau unadhihirisha kuna uwezekano mkubwa taarifa hizi ni za kweli. Tunachosikia zaidi ni kelele za wapambe ambalo si jambo la ajabu maana pesa hununua watu hata kutetea uovu.
Mungu wa kweli awajalie hekima Watanzania ili wauone wema au ubaya wa mtu kwa mtizamo wa kiimani, ambao ni upofu hatari, upofu ambao hata Baba na Babu zetu hawakuwa nao toka uhuru.