Utajiri wa damu

UTAJIRI WA DAMU - 10-

NILIMUAMBIA kuwa hakuna haja ya kuja kunisaidia kwa sababu nilikuwa nimeshamfungua na nikamdanganya kuwa mbwa mwenyewe ni mkali.

Mbwa mtu yule nilimuahidi kwamba nitamsaidia japokuwa nilikuwa sina uhakika kama nilichokuwa nakisema alikuwa akikielewa au la.
Baadaye nilichota maji kwenye kisufuria nilichokikuta ndani ya banda lake na kumuwekea. Mkononi nilikuwa na juisi ile iliyopasuka. Niliona akiiangalia kama vile anataka kusema, ‘nitilie kidogo.’
Nilichukua sinia dogo ambalo linatumika kumuwekea chakula na nikamimina ile juisi pale, haraka sana aliiendea na kuanza kuilamba.
Mbwa mtu yule alitabasamu tabasamu ambalo lilinifanya niamini kwamba yule hakuwa mbwa hawa wa kawaida tuliowazoea, nikawa sina shaka yoyote kwamba huyu ni mtu aliyegeuzwa kuwa mnyama huyo.
“Kwa nini huyu mzee amefanya ukatili huu?” nilijiuliza kimoyomoyo bila kupata jibu lolote.
Nilirudi kwa wale askari na kuwaomba waondoke ili nimpeleke mzee Mitimingi hospitali kwani wakati huo dereva wake alikuwa tayari amefika na gari lake aina ya Range Rover 5.2 .
“Sawa, kwa kuwa afande kasema tukupe ruhusa tunafanya hivyo lakini uje ofisini kesho saa mbili asubuhi bila kukosa,” alisema yule askari wa kike.
Japokuwa hakuwa amevaa sare za kipolisi nilihisi kwamba ndiye mkubwa wao wa kazi kati ya wale askari watatu waliofika kunichukua. Wangekuwa na sare ingekuwa rahisi kuwatambua kwa kuwa vyeo vya askari polisi mwenye magwanda huwa hadharani kwani huvaliwa mkononi au mabegani.
“Chepriska uguza pole,” akasema askari yule.
Alimgeukia mzee Mitimingi ambaye alikuwa ‘anaekti’ ugonjwa akamuaga. “Mzee pole sana, Mungu atakusaidia na kukuponya.”
Mzee Mitimingi anafaa kuwa msanii kwani aliitikia kwa kichwa huku akiachia mdomo, hali iliyomfanya atokwe na udenda.
Nilichukua kitambaa nikawa namfuta udenda uliokuwa ukimtoka na wakati huo huo mlinzi ambaye alikuwa Mmakonde wa kuchanja alifungua mlango wa geti na gari la polisi likatoka.
Baada ya difenda hilo la polisi kutoka mlinzi huyo alifunga geti na kuja haraka sana pale nilipokuwa na mzee Mitimingi.
“ Kwani huyu nzee anachumbuliwa na nini?” aliniuliza.
“Anasumbuliwa sana na malaria na kichomi,” nilimdanganya.
“Dawa ya kichomi ninayo. Nilikuwa nimempelekea ntu mmoja lakini chikumkuta. Ni hii, chungu nitakupa kidogo meza tu uchimung’unye, uminielewa?”
Mzee Mitimingi alimkubalia kwa kuitikia kwa kichwa na baada ya dakika mbili aliinuka na kuingia ndani na ile dawa aliyopewa na mlinzi wa Kimakonde aliiacha pale alipokuwa ameketi.
Alipoingia ndani aliwaza mazungumzo kati ya polisi na Cheprisca.
“Chepriska, huyo mbwa ana nini?” aliuliza yule askari polisi wa kike.
“Ahaa, alikuwa amejifungafunga shingoni na kamba, hivyo akawa anashindwa kugeuka.” alijibu.
“Hajapata madhara makubwa?”
“Hajapata.
“Sasa tuje kukusaidia kumfungua?”
“Hapana.”
Mzee Mitimingi akawa anashangaa jinsi msichana huyo alivyofanya ujanja hadi akafanikiwa kuwalainisha polisi. ‘Hakika huyu msichana ni mwerevu sana na ameniokoa,’ alijisemea kimoyomoyo.
“Chepriska,” aliita.
“Bee baba,” nilimuitikia.
“Njoo ndani mwanangu, uje na hiyo dawa ya Mmakonde.”
Wakati nainuka niliichukua ile dawa na kuifutika kiganjani. Mmakonde ambaye alikuwa getini aliposikia sauti ya mzee akaja mbio.
“Unaona ile dawa inafanya kashi haraka chana. Umechikia ameanza kuchema, mwambie dozi haijakamilika, chacha kesho nitamletea nyingine atapona kabicha,” alijisifu yule Mmakonde bila kujua kuwa dawa zake mzee Mitimingi hakuzinywa.
Sikumjibu lolote nikamuacha kwa sababu angejua lengo letu asingetuletea habari zake hizo.
“Uchimfiche nzee,” akasisitiza.
“Sawa nitamueleza,” nilimjibu huku nikiingia ndani.
“Anasemaje huyo Mmakonde?” aliniuliza.
“Anazungumzia dawa aliyokupa.”
“Achananaye, nitakupa zawadi kubwa sana kwa kunifichia siri kwa polisi.. kuhusu mbwa na mkono wa mtu kwenye friji,” alisema Mwzee Mitimingi huku akiniangalia.
Je, zawadi gani hiyo? Fuatilia Jumatano ijayo.
 

Story nzuri
 
UTAJIRI WA DAMU 11'
Mzee Mitimingi alinipa zawadi nono kutoka mbinguni9.alikuwa yuko happy kwa kuwa nilikeep his secrets...after that nilitoka from his place nikarudi home.
Kurudi home guess wha? nilipigwa na butwaa twa! twa! twa!. ilikuwa almost ni faint
kumbe kale kamtu ka kinyozi kalienda kuniseti kwa majirani ati mimi ni mchawi..usitake jua yaani ilikuwa kidogo nimpige kofi kali ya uso.
Tuliingia chumbani wote, "kwanini unaniharibia jina..si ungesibiri nikupe pesa zako"..yule barber alikuwa mnyonge kweli
"im sorry Chepriska..si u know nilikuwa desperate..i thought ulitaka kunirusha..malaya ka nyinyi ni risky ku do business with"
Damu ilichemka kijasho kilinitoka "unaniita malaya mbwa hii? takataka ya sewage..natena unikomee" nilijipata nikimtukana
Nilimpatia 30000..he apologized
Niliamua kuhama hii mtaa kwani nilikuwa very embarrassed .zile pesa nilikuwa nimepatiwa nimepatiwa na mzee
Miti mingi zilitosha
Nihamie wapi Posta..no its very chaotic there.Upanga..no sipapendi pale Wahindi ni wengi ..Mikocheni ..mmmh moyo ulifurahi sana..most of my life nimeishi kwa nyumba ya udongo tena paa la makuti..
Mikocheni ndio mpango mzima but nilisita hivi nitayaweza hayo maisha..MitiMingi mwenyewe anaishi Ubungo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…