masha deno
Member
- Mar 2, 2013
- 64
- 17
Mzizi mkavu leo si ndio
jumatano???[ nimechukua usukani ..9kwa ruhusa ya Mzizimkavu.9 hadithi isome hapo
Last edited by a moderator:
Mzizi mkavu leo si ndio
jumatano???[ nimechukua usukani ..9kwa ruhusa ya Mzizimkavu.9 hadithi isome hapo
kiongozi ni znuri ila sana ila ni fupi sana jaribu kurefusha wakati mwingineUTAJIRI WA DAMU - 13-
ILIPOISHIA
"Kuna habari kwamba mzee yule anapenda sana ushirikina. Hiyo ni kweli?"
"Hilo mimi silijui."
"Wewe umewahi kuishi pale kwake?"
"Hapana. Mimi huwa namtembelea tu, sijawahi kuishi pale."
"Kwa nini?"
"Kwa sababu mimi nilipoingia hapa mjini kwa nauli ya yule mzee niliamua kujitegemea. Nikapanga chumba. Siku za kwanza alinilazimisha sana niishi pale kwake nikakataa katakata."
"Ulikataa kwa kuwa ulikuwa unajua kuwa huyo mzee ni mshirikina siyo?"
"Hapana, nilipenda niwe huru."
"Kwani ulipofika hapa mjini alikuambia atakupa kazi gani?
SASA SONGA NAYO...
"Aliniambia kazi yangu ni kusimamia magari yake.
"Kwani yule mzee hana watoto au mke?"
Moyo wangu ulienda mbio kwa sababu niliona kama askari yule aliyekuwa akinihoji pale kwenye kituo cha polisi kama alikuwa ananitega.
Lakini pia nilikuwa nawaza kwamba kama wakiamua kwenda kuikagua nyumba ya mzee Mitimingi ni wazi mbwamtu watamuona na kile kiganja cha mtu watakiona.
Nikawa najiuliza ikitokea hivyo moja kwa moja nitaingia matatani. Sikujua hawa polisi waliambiwa na nani kuhusu ushirikina wa yule mzee.
"Kwani nyinyi nani amewaambia kuwa mzee Mitimingi ni mshirikina?" Nilijikakamua kumuuliza yule askari.
Aliacha kuandika, akaniangalia kama vile alikuwa akitafakari kitu. Unajua askari wa upelelezi wana akili ya kwenda mbele zaidi kwa kila kitu.
"Nakuona kama una wasiwasi."
"Wasiwasi wa nini? Nakuuliza ili niweze kujua na mimi, mbona wewe unanihoji."
"Kwa kawaida mtuhumiwa ndiye anayehojiwa polisi na kazi yake kujibu siyo kuuliza tena suala linalohusu alichoitiwa. Unaweza kunihoji ili nikikupa jibu ukwepeshe ukweli."
"Haya endelea kunihoji." Nilisema huku nikibongesha simu yangu ya kiganjani, nilipolifikia jina la mzee Mitimingi nikabofya ili iite, iliita akaipokea. Nilifanya hivyo ili asikie yale mahojiano. Simu yangu nikaiweka kwenye shavu kama vile nilikuwa naitumia kukuna shavu langu.
"Mzee Mitimingi alikuambia kazi yako ni kusimamia magari yake, kwani wewe ni fundi makenika?"
"Hapana, hakuniambia kusimamia mambo ya ufundi."
"Sasa alikuambia usimamie nini kama wewe siyo fundi makenika."
"Mimi kazi yangu ni kukusanya fedha zake, yaani kwenye mabasi na kwenye malori nilikuwa nakusanya fedha na kuzipeleka benki."
"Ahaaa kwani wewe umesomea uhasibu?"
"Hapana. Kazi yangu hiyo nilijifunza nyumbani tu na pale nimepata uzoefu zaidi."
"Sawa. Hujawahi kusikia lolote kuhusu mzee Mitimingi kuua watu?"
"Ningesikia kuwa anaua watu nisingeweza kukaa pale na kufanyanaye kazi."
"Niambie pale nyumbani kwake ni nani hasa wanaopenda kwenda na kwa muda gani?"
"Pale wanaofika ni madereva wake na mara nyingine hawamkuti wananikuta mimi."
"Anakuwa amekwenda wapi?"
"Ana mambo mengi, siwezi kujua labda siku ambazo ananiaga."
"Siku ambazo amekuwa akikuaga, huwa anasema anakwenda wapi?"
"Huwa anasema anakwenda kutembea au anakwenda kwenye mipango yake."
"Mipango gani?"
"Huwa haniambii."
"Mke wa mzee Mitimingi yupo wapi?"
"Aliniambia ni mgonjwa na amelazwa."
"Wapi?"
"Hospitali ya Dk. Mei Chilungoli."
"Kwa nini ameamua mkewe alazwe huko?"
"Daktari yule ni mtu wa kwao, tena ana utaalam wa hali ya juu kwa magonjwa ya akina mama."
"Wewe unamfahamu Dk. Mei?"
"Namfahamu kwa kuwa siku nyingine huwa anakuja nyumbani kumtibia huyo mama."
Baada ya mahojiano hayo yule askari alikwenda kumuona mkuu wake ambaye ni Inspekta Ado.
"Subiri nikamuambie afande haya uliyoyasema tuone atashauri nini."
Aliinuka na kuniacha nikitafakari, kisha nikakata simu.
Baada ya dakika chache niliitwa kwenye ofisi ya Inspekta Ado. Niliingia nikamkuta akipekuapekua lile jalada lenye maelezo yangu.
"Binti nimesoma maelezo yako hapa nadhani subiri tumuhoji mlinzi wenu. Nimetuma askari wamemleta hapa."
Baada ya dakika mbili niliona mzee Chambilecho akiingizwa katika ofisi ile. Shati lake lilikuwa limelowa jasho kama vile alikuwa anafanya mazoezi ya viungo na alikuwa na wasiwasi.
Sikujua kwa nini alikuwa na wasiwasi kiasi kile kama kwamba kaambiwa ana kesi ya kujibu inayohusu mauaji. Aligeuka kuangalia nilipokuwa nami nikajifanya kutabasamu ili kumuondoa hofu.
Hakuonekana kubadilika muonekano wa sura yake kwani bado alikuwa kama vile ananishangaa kuwepo pale. Nilihisi inawezekana yule mzee wa Kimakonde alikuwa anajua siri za mzee Mitimingi.
Je, siri za mzee Mitimingi zitafichuliwa na mzee huyo? Fuatilia alkhamisi ijayo...