Utahamia lini kijijini?

Utahamia lini kijijini?

Ahahahaha.. kuhusu You tube channel, ninkama ulikua kwenye mawazo yangu. I was about to do that ila katika masuala mengine. I am about to start kilimo cha bustan ,ninafanya kama pilot phase so far kwa matumizi ya nyumban tu kwakua niko na vijana kadhaa hapa maeneo so tunakula mboga mboga za shambani ukiachana na kutumia vyuku kama kitoweo 😂
Mkuu huyu muhuni tu story kaandika ya kutunga huoni katumia chat gpt
 
Huyu anafurahisha genge.
Kupambana na Hao wanyama ni shughuli pevu.
Hata hizo sauti za ndege anazosema, ingekuwa nadra sana kweke kuzisikia....mziki wake wa kila siku ungekuwa ni sauti za kitimoto.
Kwa scale ya nguruwe idadi yake kiukwel kupambana nao sio mchezo. Mi ninao 7 ambao sasa wanakaribia kupandishwa, najua wakifyatua watoto mziki wake utachange kabisaaaa gharama za chamula zita shoot, japo kwasasa nawamudi bila rabsha
 
Tangu nilipoondoka mjini na kukimbilia huku kijijini, nimekuwa na maisha ya amani na utulivu mkubwa sana.

Nilifanikiwa kupata shamba la ekari nne, ambapo nilijenga kibanda changu cha kujipumzikia pamoja na mama chanja wangu, pia nikachimba na kisima.

Nikaweka uzio wa mimea kuzunguka hilo eneo lote la shamba, ili mifugo yangu isiweze kutoroka hapa na pale.

Nililigawa eneo kwa makundi (A,B,C,D,E) ili kuweka mifugo mabali mbali.

A. niliweka banda la ng’ombe 5 kwa ajili ya kunipa maziwa kila siku

B. niliweka banda la mbuzi 50 kwa ajili ya kubadilisha mboga

C. niliweka banda la kuku wa kienyeji 200 kwa jili ya mayai na nyama

D. nimeweka banda la kitimoto 50 kwa ajili ya nyama

E. bustani ya mboga mboga, nyanya, vitunguu, mchicha n.k

Pia nikaotesha miti ya matunda kama michungwa, papai, parachichi, migomba, miwa n.k

Mabaki/uchafu unaotoka kwenye mifugo, unakuwa unaenda maeneo ya shambani/bustanini na kuboresha uoto wa mimea.

Kwa ujumla, mazingira haya yameniwezesha kuwa na utulivu wa akili, uchumi, na afya bora; magonjwa ya akaili hayatanipata.

Rafiki yangu mmoja, alikuja kunitembelea huku kijijini kwangu; alipofika tu na kusikia miluzi mbalimbali ya ndege ikipiga pambio, akaniambia, ‘’Equation x na mimi sirudi tena mjini.’’

Nikamuuliza kwa nini? akanijibu, ‘’tangu nimekuja huku, akili yangu imetulia kabisa, naokota matunda nakula, mayai nakula nitakavyo, kachumbari najitengenezea, nyama nachoma nitakavyo, Napata hewa safi, ndege wanakuja na kuniimbia nyimbo mbalimbali; kusema kweli naenda kuuza mali zangu zote mjini na mimi nakuja kuhamia huku kijijini.’’

Nikabaki nacheka tu.

Je, wewe, utahamia lini kijijini?

View attachment 3416701
Mkuu uneyapatia sana maisha.
Aisee kama usemavyo ni kweli hata Mimi umenihamasisha kuhama mjini kwenda village.
Hayo ni maisha ambayo Yana utulivu yasiyo na complications yeyote Ile.
 
CHAI YA BARIDI,
IMEKARIBIA KUGANDA.

Chap chapa nipe consumption ya pumba na maji per day.
Ukiemda chat GBT ukaleta takwim za kupika ntakukamata ambapo hujaeleza kuwa na kibanda cha wafanyakazi, ila umesema ypo wewe na mkeo... wewe na mkeo hamuwez kuhudumia hao wanyama abadan + bustani.

Sasa bosi hao mbuzi, kuku, nguluwe , na ng'ombe ulihitaji kuwa na vijana watatu kama ungefuga kwa mtaji wa vifaa na machine. ... kwakukosa vijana na maelezo thabiti .... Basi hapo umenipa chai.
ni chai tu.
Inaonekana hujawahi kuishi maisha ya kijijini bro.
Nimewahi kutembelea kwa mkwe wangu Singida, Wana ng'ombe zaidi ya 30,mbuzi ,kuku na kanga na wanaishi wanne tu wakwe na shemeji zangu wawili ila Wana manage mambo yote hayo.
Ishu ni kujipangilia tu na namna ya kuwatunza hao mifugo.
 
Mkuu Equation x , hongera, kama haya umeandika ni kweli , lakini TO ME ,this life is real. NIMERUDI NYUMBANI.
BAada ya kumalizana na masuala ya talaka na ndoa kuvunjika, nikaamua kuacha kila kitu na kuamua kurudi mkoani (nyanda za juu kusini).
Hapa ndipo nimezaliwa na kusoma toka chekechea mpaka nahitimu high school Tosa boys miaka 15 iliopita.
Sikutaka kukaa mjini kati, nikasogea pembezoni kabisa mwa mji huko mashambani.
I live a very peaceful life considering the fact kwamba umeme upo, maji ya mamlaka ya maji mkoa pia yapo ya kotosha.

Nilichokifanya ni

  • ku establish my local gym, kwakua ninapenda weight lifting.
  • nimefungua mradi wa kufuga nguruwe, nilianza na nguruwe 7, huu bado naukuza haujaanza ku pay out
  • nikafungua pia mradi wa ufugaji kuku chotara na wa kienyeji. Nina average ya kuku 400 ambao hawapungui mabandani all the time maana hawa tayari nilishaanza kuwauza na for every 3 weeks sikosi kuuza kuku wa wastani wa shilling 800,000/.

Sio mashamba yangu bali ni maeneo ya wazee wangu, ambayo niliona wanayatumia kwa kiasi kidogo sana, nikaona acha niyatumie ipasavyo.

By proffesion, mimi mi software developer na "software As Service" ndio biashara yangu so i continue coding during night to support my clients technically. So am getting paid while being right here , regardless nimelala or what!!

KIukwel ,maisha haya so far yananipa utulivu sana ,niii tafakari my come back (japo najiona kabisa siwezi tena rudi jijini).

I take few trips kusafiri pale ambapo nahitaji kuonana na clients wangu mikoani na jijini lakin most of the time napatikana shambani kijijini, huku ndiko maisha yangu yame base kwasasa..

Napata muda wa kutosha kulala sanaaaa.
Kufanya mazoezi sana pia.
Una wafanyakazi wangapi ? Hakika maisha yako nimeyapenda hao kuku hswakutoi jasho aisee ?

Nunua gari dogo kama corolla uwe unatoka hata jumapili unaingia katika ya mji unakula bata alafu unarudi zako nyumbani
Nimependa sana aisee
 
Mkuu uneyapatia sana maisha.
Aisee kama usemavyo ni kweli hata Mimi umenihamasisha kuhama mjini kwenda village.
Hayo ni maisha ambayo Yana utulivu yasiyo na complications yeyote Ile.
Acha ushamba hii story imeandika na A.I chatgpt sisi wataalamu tunajua how chatgpt behave ikiandika kitu...pia picha kadowload mitandoni Hapo sio tanzania

So calm down sio kila kitu unakiona Mtandoni ni chenyewe story ni kutunga na chatgpt kaja kapaste washamba mnajaa
 
Back
Top Bottom