Utahamia lini kijijini?

Utahamia lini kijijini?

Kuna sehemu nililishwa nyama yake bila kujua, niliitema kwa sababu haikuwa na ladha pendwa.
Hahahah ILA SI anakula majani HUYO kiumbe Hana SHIDA na MTU HUYO , anza na NYAMA yake ya kukaanga au kuchoma ukizoea anza kupiga na supu

Kwishaaaaa
 
My take-wazo zuri,ila umetupanga sana.
Wekeza mjini uwe na income inayoeleweka--lets say unakusanya kodi ya majengo inayofika atleast 3M kila mwezi.
Ndio uhamie kijijini--ila usiuze.
 
Tangu nilipoondoka mjini na kukimbilia huku kijijini, nimekuwa na maisha ya amani na utulivu mkubwa sana.

Nilifanikiwa kupata shamba la ekari nne, ambapo nilijenga kibanda changu cha kujipumzikia pamoja na mama chanja wangu, pia nikachimba na kisima.

Nikaweka uzio wa mimea kuzunguka hilo eneo lote la shamba, ili mifugo yangu isiweze kutoroka hapa na pale.

Nililigawa eneo kwa makundi (A,B,C,D,E) ili kuweka mifugo mabali mbali.

A. niliweka banda la ng’ombe 5 kwa ajili ya kunipa maziwa kila siku

B. niliweka banda la mbuzi 50 kwa ajili ya kubadilisha mboga

C. niliweka banda la kuku wa kienyeji 200 kwa jili ya mayai na nyama

D. nimeweka banda la kitimoto 50 kwa ajili ya nyama

E. bustani ya mboga mboga, nyanya, vitunguu, mchicha n.k

Pia nikaotesha miti ya matunda kama michungwa, papai, parachichi, migomba, miwa n.k

Mabaki/uchafu unaotoka kwenye mifugo, unakuwa unaenda maeneo ya shambani/bustanini na kuboresha uoto wa mimea.

Kwa ujumla, mazingira haya yameniwezesha kuwa na utulivu wa akili, uchumi, na afya bora; magonjwa ya akaili hayatanipata.

Rafiki yangu mmoja, alikuja kunitembelea huku kijijini kwangu; alipofika tu na kusikia miluzi mbalimbali ya ndege ikipiga pambio, akaniambia, ‘’Equation x na mimi sirudi tena mjini.’’

Nikamuuliza kwa nini? akanijibu, ‘’tangu nimekuja huku, akili yangu imetulia kabisa, naokota matunda nakula, mayai nakula nitakavyo, kachumbari najitengenezea, nyama nachoma nitakavyo, Napata hewa safi, ndege wanakuja na kuniimbia nyimbo mbalimbali; kusema kweli naenda kuuza mali zangu zote mjini na mimi nakuja kuhamia huku kijijini.’’

Nikabaki nacheka tu.

Je, wewe, utahamia lini kijijini?
View attachment 3418535
Kitimoto 50 ni mradi mkubwa sanaa sanaa ......kitimoto 1 anakulq kilo 2 hadi 3 kwa siku....kila siku kilo 100.....sio mchezo ....
 
Maisha ya kijijini siyo mazuri kwa watu wote.

Wengi ya waishio kijijini, wanepigika na wanaishia kunywa gongo na kuvuta bangi tu.
Hata ulaya na america, wanaoishi vijijini ni choka mbaya na low IQ.

Kama ni kufuga unaweza lufanya hivyo hata ukiwa mjini.

Mjini sehemu zenye hewa safi na zisizo na kelele zimejaa tele.

Walio vijijini nao wanatamani kwenda kuishi mjini, kwa kuwa mzunguko wa pesa ni mkubwa, tofauti na kijijini.

Kwa kifupi, kijijini hakuna maisha.
 
Inabidi kutengeneza mnyororo wa upatikanaji chakula
 
Maisha ya kijijini siyo mazuri kwa watu wote.

Wengi ya waishio kijijini, wanepigika na wanaishia kunywa gongo na kuvuta bangi tu.
Hata ulaya na america, wanaoishi vijijini ni choka mbaya na low IQ.

Kama ni kufuga unaweza lufanya hivyo hata ukiwa mjini.

Mjini sehemu zenye hewa safi na zisizo na kelele zimejaa tele.

Walio vijijini nao wanatamani kwenda kuishi mjini, kwa kuwa mzunguko wa pesa ni mkubwa, tofauti na kijijini.

Kwa kifupi, kijijini hakuna maisha.
Kwa mazingira haya kijijini, unaonafursa ipi?
zwa.webp
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom