Utafiti: Wanawake hawapendi pesa

Utafiti: Wanawake hawapendi pesa

IMG-20261001-WA5033.jpg
 
Sitaki kuwapotezea muda kwa maelezo marefu. Kila kitu kiko wazi. Tafiti za mahusiano zilizofanywa na wataalamu wa mahusiano zinaonyesha wanawake wengi hawatazami ukubwa wa pochi, bali ukubwa wa muda unaotolewa . Wengi wanasema pesa sio shida bali umakini na mawasiliano ya kweli ndivyo vinavyogusa moyo zaidi.
Wanaume wengi wamezoea kudhani kutoa hela ni ishara ya upendo, kumbe wengine wanachohitaji ni muda wako tu.
View attachment 3681646
MAONI YANGU
Afadhali sasa ule uwongo uliodumu kwa muda mrefu kuhusu wanawake kupenda pesa sasa umepata ufumbuzi. Kuanzia sasa wanaume wanapaswa kutambua kuwa pesa si chochote si lolote katika mahusiano. Mwanamke anahitaji muda wako tu.

Utafiti huu umekuja wakati muafaka kwani wanaume tulishatumia pesa nyingi sana katika mapenzi pasipo kujua. Kwa kuwa sasa ukweli umejulikana, hii ni ahueni kubwa sana kwa wanaume waliokuwa wanadhani wanawake wanapenda fedha kumbe si kweli. Hadi wanawake wanaitwa "gold diggers" pasipo kujua kwamba hawapendi pesa bali wanahitaji muda tu!

Pongezi za kipekee ziwaendee watafiti waliogundua hili jambo mapema kabla mifuko ya wanaume haijatoboka zaidi. Mungu awabariki sana.
​
Kweli kabisa, tumesingiziwa mengi sana😹😹
 
Kuna mmoja zamani kidogo aliwahi kuniambia bila kuona pesa, hata ku- cum ha-cum na suala la kuniimbia na maiki ndiyo nisahau kabisa 🙌

Bora tumezeeka sasa 🤗
Pesa sabuni ya roho. Ukweli ni kuwa ili mmoja ampende mwenzake lazima kuwe na kiunganisho. Ila pamoja na kiunganisho, ndoa au pesa au kazi etc; unahitaji pesa ili akale, akanywe akasafiri na hata kujisopsop. Ndo maana nasema, katika mapenzi, pesa haikwepeki hata kama unadhani anakupa bure. Duniani hakuna kitu kinaitwa Bure. Ukiona kitu ni bure kwako, jua kuna mwenzako anakigharamia.
 
Back
Top Bottom