Duh hapa ni kuwekana mtegoni.
Kwa njia ya elimination huo wa mshkaji tayari nimeutoa.
Kati ya hivyo vitatu na hapa na-factor in mambo matatu; hamu ya chakula niliyonayo kwa sasa, chakula kilichopo kwenye options, na mpishi (maana nahisi ni mojawapo ya vigezo ndiyo maana kuna majina na sio namba).
Kuku, harage, samaki - chips, wali, ugali!
Nina muda mrefu sijala ugali...ninapenda samaki kuliko kuku na maharage kwangu yanachukua nafasi ya mwisho...
Hivyo nadhani ningepiga msosi wa maza kwa kweli.
Ila kidiplomasia unapiga msosi wa maza,
unabakisha nafasi unaenda kupiga paja moja la mpenzi kisha unazuga una hamu na yeye kuliko chakula chake ila unakisifia kweli na kwamba ahakikishe anakihifadhi maana utakila baadaye. Unahakikisha unampiga game ya maana kabisa - 6 X 6 - maana ushapata ugali.
Kisha unaomba ruhusa ya kwenda kunyoosha miguu unamalizia kwa bibi unashushia wali harage smoothly huku akikupigia stori za zamani, yeye na babu na mambo kama hayo. Mnadiskass siasa kidogo kisha unamuaga kuwa mke mwenzake anakuhitaji, unarudi home.
NB: Huyo mshkaji - esp kama ni mshkaji wangu - ataelewa fika kuwa kwake sitofika na msosi wake sitoula.
Ila hii bonge la scenario. Hapo unabidi ufanye assumption wote wanaishi eneo la karibu karibu kwamba unaweza kuzungukia wote. Ambapo on second thought, unaweza pita kwa mshkaji ukala vijiti viwili vitatu huku mkipiga stori za maisha na mipango miji. Kisha jioni unajirejesha kwako kumalizia yule kuku chips!!!
NB: ratiba hii ianze saa tano asubuhi.