Utabiri wangu: Rais Samia awe makini na sakata la Mbowe, litamaliza kabisa kibali kidogo alichobakiwa nacho kwa Watanzania

Umeshamuuliza mbowe kama hakupanga hiyo njama na kuifadhili?
Kama unahisi anaonewa basi subili mahakama iamue.
Mahakamaccm ikiamua kwa nguvu za mungu lazima haki itapatikana lakini mahakamaccm ikiamua kufanya kazi kwa mujibu wa zidumu fikra zisizo sahihi za mtukufu mwenyekiti wa CCM lakini uonevu utawale kupita kiasi
 
Halafu mama kadanganya dunia. Mwaka jana September Mbowe hakuwahi kufunguliwa kesi yoyote ile.
 
Hii Tabia mbovu ya kutumia Polisiccm kwenda kuwapekua wapinzani itaishia lini? Mbona Gwajima na polepole wapo kinyume na fikra za mwenyekiti wa CCM lakini Polisiccm hawajaenda kuwapekua?
 
Jiwe vs Mbowe jiwe chali, sabaya vs Mbowe sabaya chali,samia vs Mbowe tunasubiria majibu.
 
Mwaka 2017 niliandika mada hii Viongozi wa kisiasa kumbeukeni maneno haya; Mene, mene, tekeli, na peresi baada ya kuona kinachoendelea nchini.

Ujio wa Mama uliamsha matumaini makubwa sana ndani ya mioyo ya watanzania, na matamanio makubwa yalikuwa si kuona uchumi unakuwa kwa asilimia 7 wala si kuona ndege na madaraja bali ilikuwa ni kuona utawala wa haki, utawala wa sheria unarejea nchini.

Binafsi naona kibali cha Mama ndani ya mioyo ya watanzania kinaporomoka kwa kasi sana, hasa baada ya kuibuka issue ya miamala, machinga kuanza kusumbuliwa bila kusahau bodaboda.

Kama sakata la mbowe ni la kubambikiza basi Mama ajiandae kubeba lawama zote na kibali kidogo kilichobaki kuporomoka zaidi na simuoni akitoboa katika uchaguzi wa muhula wa pili japo tunajua yawezekana si yeye bali ni utashi wa jeshi la polisi lenyewe.

Sakata hili linaweza kuwa ni last nail on the coffin. Ila kama mashtaka ni ya kweli hiyo inabaki kuwa story ya wakati mwingine.
Bahati mbaya ameamua kutofikiri na amekubali kupelekeshwa na kundi la wahafidhina ndani ya chama chake sambamba na wale wenye dahamana ya yombo vya mabavu (cohesive instruments) ambao siku zote bima ya maisha yao ni kuishi kwa ubabe ili waendelee kuwepo. Mungu anawaona na yana mwisho.
 
Mwaka 2017 niliandika mada hii Viongozi wa kisiasa kumbeukeni maneno haya; Mene, mene, tekeli, na peresi baada ya kuona kinachoendelea nchini.

Ujio wa Mama uliamsha matumaini makubwa sana ndani ya mioyo ya watanzania, na matamanio makubwa yalikuwa si kuona uchumi unakuwa kwa asilimia 7 wala si kuona ndege na madaraja bali ilikuwa ni kuona utawala wa haki, utawala wa sheria unarejea nchini.

Binafsi naona kibali cha Mama ndani ya mioyo ya watanzania kinaporomoka kwa kasi sana, hasa baada ya kuibuka issue ya miamala, machinga kuanza kusumbuliwa bila kusahau bodaboda.

Kama sakata la mbowe ni la kubambikiza basi Mama ajiandae kubeba lawama zote na kibali kidogo kilichobaki kuporomoka zaidi na simuoni akitoboa katika uchaguzi wa muhula wa pili japo tunajua yawezekana si yeye bali ni utashi wa jeshi la polisi lenyewe.

Sakata hili linaweza kuwa ni last nail on the coffin. Ila kama mashtaka ni ya kweli hiyo inabaki kuwa story ya wakati mwingine.
Mama anaupiga mwingi sana, haangalia kibendara cha line man wala hasikii kipenga cha refarii
 
Mkuu nimeoenda Paragraph ya Mwisho!

Kama ni ya Kubambikiza lawama atazibeba

Natamani Uongee kidogo kama Ni ya Kweli Itakuwaje kwa wanaimtetea?

Mimi hapa Nacheka tuu natamani Kujua ukweli ndio maana sitaki kutetea Au Kuulaumu Upande wowote ili nisije kuumbuka Mbeleni!
Kaaa kimya
 
Kama ilikuwa lazima mama azungumzie suala la mbowe angesema tu kesi iko mahakamani tuache sheria ifuate mkondo wake lakini maelezo yake ya ziada yamemuweka pabaya mno. Watanzania wanajua mbowe sio gaidi. Mama anachoshindwa kuelewa au wasaidizi wake wa karibu hawampelekei taarifa ni kuwa ana vita vikubwa na team mwendazake na sio kikundi kidogo, mfano kiduchu amemsikia slow slow , Gwaji anauma na kupuliza lkn ukweli ndio team yenyewe, alipaswa kulinda imani ya wananchi wengi waliokuwa wanamuunga mkono alipochukua madaraka , vinginevyo anaingizwa chaka.
Yawezekana ni swali la ghafla hakulitegemea
 
Back
Top Bottom