Ukitaka unufaike na matatizo yako basi yageuze upande wa pili.
Sakata la bandari limeibua mengi na sasa linaonekana kutaka kuigawa nchi. Niwaambie kitu? Nchi yetu itakuwa imara zaidi baada ya sakata hili.
Kwani tutawajua viongozi wetu vizuri zaidi, tutajua sheria zetu vizuri zaidi, viongozi wa hovyo wataondoka, watanzania watakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kusimamia mambo yao, mikataba mingi mibovu itafikiriwa upya, viongozi wetu watakuwa na adabu zaidi, sheria zetu zitakuwa nzuri zaidi na nchi itaimarika zaidi.
Tutumie nafasi hii kuwapima na kuwawajibisha viongozi wetu. Ni wakati mzuri wa kuondokana na utawala mbovu.
Watanzania tusimame imara kwani viongozi siku zote huwa makini zaidi kama wananchi ni makini kufuatilia mambo yao.
Hakuna nchi au mtu aliyeendelea bila changamoto.
Mungu ibariki Tanzania.