Ujumbe kwa Rais Samia kuhusu Sakata la Lissu na amri za Wanao Bypass Mamlaka yake

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,799
71,220
Ujumbe kutoka mdau huko X (formerly Twitter) kwa mheshimiwa Rais na jinsi Mwenezi anavyo mdharau kwa kutenda bila kufikiri kama asemaye "atanifanya nini".
SOMA:

special letter to her excellence @SuluhuSamia

It is a tradition that we always start with a greeting.

Mama, Umuofia kwenu!

I hope you are doing very great.

Let me introduce myself.

My name is Hoof-man, the worldwide defacto president and spokesman for the paratroopers.

Apparently, the colloquial 'paratroopers' represents the downtrodden class that meets their ends at blood and sweat points. (Sometimes at ngumi point)

I want only to address two issues at your very busy desk mama.

In a bid to grasp mutual understanding, allow me to switch to our mother tang.

1. Leo asubuhi, watanzani tumeshuhudia jambo la ajabu sana kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.

Makamu mwenyekiti wa chama cha upinzani Mh. Tundu Lissu ameshindwa kufanya mahojiano kwenye kituo cha habari cha Wasafi TV tofauti na ilivyotangazwa.

Kinachosikitisha ni kwamba, si Tundu Lissu wala management ya redio hiyo ndio walikuwa sababu ya kipindi hicho kutofanyika.

Inasemwa sababu ni maelekezo kutoka juu.

Nimewasikiliza watangazaji wa kipindi hicho wakionesha kushangazwa kwao na maelekezo hayo. Nakuomba mama ukipata muda pitia video ile kuna ujumbe mkubwa utaupata very directly.

Tundu Lissu hakuridhishwa na taarifa kuwa hakutakuwa na kipindi kutokana na maelekezo kutoka juu.

Akaamua kwenda physically kituoni pale ili ajue bayana ni nani alitoa maelekezo hayo na kwa nini.

Watangazaji wakajito kuwa hawahusiki bali awasiliane na management.

Management ikashindwa kumtaja huyo mtu aliye juu na ikakanusha kuwa hakukuwa na maelekezo hayo.

Management ikamwambia hakukuwa na coordination kati ya manager wa vipindi na uongozi kwenye swala lile kwa hiyo wataangalia njia bora ya kufanya kipindi kingine kwa ukubwa sawa na ukubwa wa Lissu.

Sugar coating!

Mama najiuliza,

Ni kwamba mkurugenzi wa vipindi wa WASAFI hajui wajibu wake au ikiwa kwa upinzani ndipo inatakiwa coordination?

Ni kweli kwamba uongozi wa WASAFI haukuwa na taarifa wakati matangazo ya kipindi hicho yanawekwa kwenye kurasa zao za kidigitali?

Mama hapa jibu ni moja tu!

Ni kweli kuna mkono wa aliye juu kwenye hili.

Natamani kumjua mtu huyo mama kwa sababu nadiriki kusema si wewe.

I know your leniency mama.

Wewe ni mvumilivu wa ukosoaji, upendaye watu watoe mawazo yao kwa uhuru na msikivu.

Hata maandamano ya hivi karibuni ya CHADEMA yanatokana na dhamira yako hii njema.

Mama, Who is overpowering you?

Ni nani anatoa maelekezo yanayokinzana na wewe raia namba moja?

Mama, mimi ni mtaalamu wa Ciphers (Coded language)

Naweza ku encrypt (kufumba) na ku decrypt (kufumbua) mafumbo.

Kuna watu ndani wanaoamini wao wanamaamuzi zaidi. (Sijui kama ni kweli au la)

Lakini si NAPE NNAUYE mwenye dhamana na vyombo vya habari aliyetoa maelekezo haya.

Huyu aliye juu ni nani?

Kama humjui naomba nikujuze

Ni yule CCM 004 anayezurula kujitambulisha wakati KM wake hafanyi ziara za kujitambulisha.

Kwanza anajitambulisha kwa lipi?

Kuwa yeye ni mharifu mwenye bahati zaidi? Nani asiyejua alichokifanya CLOUDS?

Mama umewasikia watangazaji wa WASAFI leo? wametaja jina la mwenezi mara tano.

Mama wewe kama kiongozi wa nchi, maamuzi yako (hasa ya uteuzi) hayapaswi kuhojiwa wala kusahiishwa.

Kibiblia tunasema maamuzi yako yako 'beyond human comprehension'

Nakuomba mama sali kwa imani yako, Mungu akuongoze kufanya tafakari ya kunasua bomu hili.

It's a time bomb

2025 si mbali, Kuna antagonism kubwa sana ndani ya chama na serikali

Usije kushangaa ukiona 'Mugambo wanaruka na kukanyagana' kama hutachukua hatua mapema.

Kumbuka haya yanatoka kwa mtaalamu wa mafumbo. (Sio mafumbo ya fumbo mfumbie mjinga bali utaalamu wa mawasiliano ya uficho)

Mafumbo si ushirikina wala unajimu

Mafumbo ni sayansi.

Mama, nina jambo la pili la muhimu linafata baadae

Mama

Mali sapi chito, Mama

MT.84237 Pte. Buyobe, Gwiji la kukonyeza gizani na kunyatia viziwi.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, kweli Bashite ni time bomb.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Nashangaa hii confidence ya Bashite juu ya huyu mama inatokana na nini? Ni huko anakosema alipendekeza walipokuwa kwenye bunge la katiba kuwa angefaa
kuwa makamu wa Rais tu basi?
Is that the justification to delegate her powers to Bashite the “ Loose Cannon “?
 
Nashangaa hii confidence ya Bashite juu ya huyu mama inatokana na nini? Ni huko anakosema alipendekeza walipokuwa kwenye bunge la katiba kuwa angefaa
kuwa makamu wa Rais tu basi?
Is that the justification to delegate her powers to Bashite the “ Loose Cannon “?

Sema hutakiwi kumsemea mbaya kiongozi aliye na umri wa mzazi. Unaacha heshima yake ibakie.
 
Bila kupepesa macho mtu mwenye tabia za hivi za kuingilia uhuru wa vyombo vingine ni Makonda hakuna mwingine aliyepiga simu usafini wasimrushe lissu ni makonda.

Makonda oe of his poweful tool ni kutrend kwenye vyombo vya habari. Ona toka amepata uenezi amechukua videographer wa millard ayo kila siku wamuandike wamtoe kwenye platform zao zote za you tube, instagram.
 
Bila kupepesa macho mtu mwenye tabia za hivi za kuingilia uhuru wa vyombo vingine ni Makonda hakuna mwingine aliyepiga simu usafini wasimrushe lissu ni makonda.

Makonda oe of his poweful tool ni kutrend kwenye vyombo vya habari. Ona toka amepata uenezi amechukua videographer wa millard ayo kila siku wamuandike wamtoe kwenye platform zao zote za you tube, instagram.
Ningependa kumwuliza Prof. Mkenda, Waziri wa Elimu kama anajua wastani wa IQ ya Mtanzania ni ngapi atuambie na kama imeshuka ni kwa kiasi gani katika muda wa miaka 15 iliyopita? Au mitaala inabadilishwa bila tafiti zinazoonesha viwango tulipofikia kabla mitaala mipya kuanzishwa ili tuweze baadaye kupima ufanisi "bench marking"?
 
Mimi naona nchi kama Haina viongozi wakututoa kwenye umasikini hata wa mawazo.
 
Tuspende kuuficha ujinga makonda anataka turudi alikotufikiaha kipindi Cha baba yake jiwe hatukubali tena tuyakata Mambo ya shetani na shetani mwenyewe.
 
Nashangaa hii confidence ya Bashite juu ya huyu mama inatokana na nini? Ni huko anakosema alipendekeza walipokuwa kwenye bunge la katiba kuwa angefaa
kuwa makamu wa Rais tu basi?
Is that the justification to delegate her powers to Bashite the “ Loose Cannon “?
Naanza kudhani kuwa ile picha ya enzi za bunge la katika waliyopiga wamekaa na kukumbatiana aliisambaza mwenyewe ili kutengeneza ka drama na woga fulani kwa wengine kuwa yeye na #1 wanaukaribu usio wa kawaida.
Huyu kijana ni mshenzi, siku watakapo gundua kuwa ana mbinu chafu watamgawana nyama. Nashindwa kuelewa kweli wazee wa kaunda suti wameshindwa kumng'amua na kumshitua #1?

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Ingelikuwa wapinzani na wanaharakati wa Twitter wanamsifia kwa kumteua Makonda na anachofanya labda huyo mama ndio angeshangaa nakujiuliza mara mbili.

Tofauti ya ‘bi tozo’ na wanasiasa wengi, huyu mama ni tactical kwenye moves zake za siasa she is well coached (the same can’t be said kwenye kuwaletea wananchi maendeleo).

Makonda ana kazi maalum ya ‘charm offensive’ kwa niaba ya mwenyekiti wake kuelekea uchaguzi wa mwakani na anaitekeleza kwa umahiri kipimo ni kila siku mikutano yake inavyozidi kujaza for the right reasons sambamba na mikakati ya ‘bi-tozo’.

Shida ya mbadala wa CCM ni kutoelewa vita mbinu, hivi unadhani Makonda atatolewa hapo kirahisi wakati kuwekwa for strategic reasons whilst he is executing his task splendidly.

You people live in your own world, mnadhani watu wote wana akili ndogo hawajui wanachokifanya wana bahatisha bahatisha tu mambo kwenye maamuzi yao.
 
Back
Top Bottom