Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,892
- 3,196
Asalaam Aleykum.
Bila shaka wote mko vizuri na mnaendelea na kazi za ujenzi wa Taifa letu.
Leo ninao wosia kwa viongozi wa nchi yetu kuwa makini na raia wao, maana ni ukweli usiopingika kwamba Watanzania wengi ni wanafiki. Mnafiki ni mtu anayejifanya vile asivyo. Kwa maneno mengine, mnafiki ni mtu kigeu-geu.
Hili linaweza kuthibitishwa na mtizamo wa Watanzania kwa sakata la mkataba kati ya Serikali na DP World. Watanzania wanaohudhuria mikutano ya upinzani wote wanaonekana kuupinga mkataba huo ilihali wale wanaohudhuria mikutano ya chama tawala huonekana kuunga mkono 100%!
Nimekaa nikatafakari kwamba, siyo kweli kwamba wote huwa wanakubaliana na aidha viongozi wa chama tawala au upinzani, bali wengi huwa wanataka kuwaridhisha tu viongozi wao wanaoendesha mikutano hiyo.
Kwa kawaida huwezi kutenganisha uoga na unafiki. Hivyo, kwa sababu Watanzania wengi ni waoga, basi hujikuta wanakuwa wanafiki automatically kwa sababu tu ya kuonekana kuwa tofauti na viongozi wao hasa hasa wa chama tawala.
Hivyo, kwa kuhitimisha, nawaomba viongozi wa serikali wawe makini sana na hawa Watanzania hasa wanaoonekana kukubaliana na mkataba kati ya DP World na serikali pamoja na mapungufu yake.
Muda ukifika, wanaweza kujikuta wanashangaa kuona wamegeukwa na raia hasa baada ya kutoka madarakani.
Mungu wabariki viongozi wetu wafanye maamuzi bora kwa ajili ya ustawi wa raia wote wa nchi hii. Pia naomba uwasaidie raia wa nchi hii kuondokana na uoga pamoja na unafiki. Wawaambie viongozi wao ukweli. Wawasifu viongozi wao pale wanapotenda vyema, wawakosoe pia pale wanapokosea; maana hata wao ni binadamu pia.
AMIN.