Utabiri: Rais ajaye Tanzania (2015) ni Mwanamke

Utabiri: Rais ajaye Tanzania (2015) ni Mwanamke

Hivi ni kwanini tusiweke mazingira sawa(level ground play) kwa wote kushindana kupata kiti chochote haya mambo ya kuwabeba nadhani kwanza ndio yanayowarudisha nyuma siku zote tuache mambo ya kujaribu kwa suala nyeti kama hilo kama mtu anaweza anapaswa kuchuana na wenzake bila kupewa upendeleo wa aina yoyote ile na kama hawezi atatuharibia tu haina haja ya kumbeba.
 
Hivi kwa umri ule yule babu DR SLAA bado ana ndoto za urais. Anyway atachaguliwa na kanisa lake

Haya na wewe jiandae kumchagua huyo rais mwanamke uliyetabiriwa
 
HAYO NI YAKO WE HUMJUI YULE MKE WA KAMBO WA MZEE DIGITAL SIJAHALA!? Baada ya tuhuma za ukanda (North) wanataka kufanya hivyo nadani ya cdm nyota iliwaka kwa Mdee lakinoi kwa kuwa alishamtolea nje M'Kigoda hana lake (Sasa wapi)? ZIWA. Nani (MRS) ili kutokupeleka mbali fikra POTOFU ZA DIGITAL
Na ww hueleweki....weka wazi...puzzle za nini??????
 
Badala ya kutaja sifa za Rais ajaye watu wanataja majina! Au "uanamke" nayo ni sifa ya Kikatiba ya kuwa Rais jamani? Wengine wamethubutu kutaja hata "maeneo," kwamba Rais wa safari hii atatokea eneo fulani! Kwa kweli nchi haina mwelekeo kwa sasa!

Hapa ndipo tulipofikia kwa sasa, yaani inaudhi mno. Ninachoona mimi hapa ni kuwa kuna watu wachache sana (Mafisadi?) wanaokaa na kutuamria wengi ni nani awe kiongozi wetu na katika ngazi ipi na nadhani unakumbuka vizuri yaliyotokea wakati wa kumpata spika wa bunge la sasa. Na huu ndo mwanzo wa vituko vingi vitakavyofuata manake naona wanaanza kutuchota akili taratibu.
 
Kwa taifa hili ambalo raisi ni zaidi ya katiba iongozwe na mwanamke? Hawa tunaowaona ni wanaume hawawezi utasikia mafisadi tukiwachukulia hatua nchi itayumba, na bibi kiroboto amewaangusha wanawake wote kwani ameshindwa kuendesha bunge
 
Dah, nchi hii Urais umekuwa rahisi mpaka unatabiriwa kirahisi tu! Kweli hili ni janga!
 
Hili siyo taifa la wachawi!!!! Hatuonzwi na piga manyanga, maana hata ikulu kumekuwa hakuishi wale wazee wapiga manyaga.
 
mmh sasa prezdaa akiwa mwanamke mumewe tutamuitaje wadau....mi hapo utata m2pu
 
Itakuwa staili design ya iliyomuengua Sitta kwenye Uspika? Ambapo king maker Rostam alitoa amri bi Kiroboto ndiyo zamu yake kuwa spika, mzee mzima Sitta akajikuta anasalimu amri kuutema uspika kwa kuwa alishindwà kujigeuzà kuwa mwanamkè kama ambavyo magamba waliweka kama sharti ili uukwae uspika!

It might b
 
Mtabiri maarufu ametabiri kuwa Rais ajae Tanzania atakuwa ni mwanamke. Utabiri huo utakuwa umewakata maini Mh Laigwanani na Mh wa Mambo ya nje.

Source: Magazeti ya leo kama vile Majira na Jambo Leo


Sijaelewa kwani Chadema wamesema mgombea wao ni mwanamama?:crazy:
 
Taifa hili bado sana kuwa na rais mwanamke

Mzee usiseme hivyo ............ maana wao pia wana haki ya kugombea. Nakumbuka 1995 kuna mama anaitwa Maghembe alijitosa kugombe............. nasikia Nyerere alimtoa machozi kwenye usaili!! Sijui aliishia wapi huyu mama?? maana hata ubunge hatujamsikia!!

Anyway, so far sioni mwenye uwezo!! Sema JK kuupata Urais imetupa imani kuwa kila mtu anaweza kuwa Rais!!
 
Kuna Taifa tukufu usawa huu.Mtu kiongozi wa dini kabisa na haruhusiwi kuzini ila unakuta ana watoto kibao mtaani.
Taifa letu limenajisiwa nanyi kwa Kuchoma Makanisa na kujaribu kuua viongozi wa Dini
 
Mtabiri maarufu ametabiri kuwa Rais ajae Tanzania atakuwa ni mwanamke. Utabiri huo utakuwa umewakata maini Mh Laigwanani na Mh wa Mambo ya nje.

Source: Magazeti ya leo kama vile Majira na Jambo Leo

.
Watu wakiambiwa kuwa hii nchi inaongozwa kishirikina mnakataa. Ona magazeti yalioandika front page huu uchawi. Gazeti la majira nalo siku hizi limo katika list ya walamba bahasha wakuu.
.
 
Jamani ke au me tusianzie kwenye urais au uspika,chagueni mwenyekiti wa chama chenu mwanamke au katibu mkuu au makam mwenyekiti au naibu katibu mkuu au katibu mwenezi msifanye majarîbio kama mlivyofanyakwenye uspika,kama wapo anzeni kuwaamini kwenye uenyekiti au umakam mwenyekiti,sio kwenye jumuiya zaàkina mama.Onesheni imani zenu kwao ndani ya chama kwanza.
 
Mtabiri maarufu ametabiri kuwa Rais ajae Tanzania atakuwa ni mwanamke. Utabiri huo utakuwa umewakata maini Mh Laigwanani na Mh wa Mambo ya nje.

Source: Magazeti ya leo kama vile Majira na Jambo Leo
Shehe yahaya amefufuka...au nini
 
Back
Top Bottom