Ni kweli tupu mkuu
tumekuwa taifa la hovyohovyo mpaka inatia kichefu chefu. Lakini sisi
kama wananchi ambao tunatambua hali hii tunawajibu wa kujaribu
kuibadilisha .NAAMINI UWEZO TUNAO!
Lakini mimi sishangazwi sana na tabira za namna hiyo, kwani ndo burudani
ya mkuu wa nchi yetu. Yeye ana-entertain sana mambo hayo.....inaelekea
ni mfuasi mzuri wa ishu hizo hapo.
Si hivyo tu, nina amini kuwa huo ni mpango wake wakutumia watu wa aina
hiyo ili kuuaminisha umma kuwa sasa ni zamu ya WANAWAKE (si
imetabiwriwa!),ili kesho akiibuka na kusema hivyo hadharani tusishangae!
Huu naamini ni mpango wake kwa sasbabu imeshazungumzwa huko nyuma kuwa
anamuandaa Dr Asha-Rose Migiro kuwa mrithi wake,akiwa na lengo la
kumpoteza kabisa swahiba wake EL.
Pia anaamini kwa sasa mtu pekee wa upinzani ambaye ni presidential
material,anayewatia hofu CCM na mwenye nafasi kubwa ya KUSHINDA ni Dr
SLAA, na wao kama chama hawana mtu (mwanaume) wanayeweza kumsimamisha
kupambana naye, hivyo anaamini njia pekee ni kuja na kigezo cha JINSI
(ZAMU YA WANAWAKE)
Hivyo ndo anaiandaa jamii kisaikolojia,KAMA WALIVYOFANYA KWENYE UCHAGUZI
WA SPIKA!