Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,507
Tanzania ni nchi ya ajabu kweli.
Siamini kama habari hii inaweza kupewa kurasa za mbele za magazeti karibia yote ya kila siku katika nchi ambazo wananchi wanaamini sifa ya rais siyo jinsia na hapatikani kwa matunguri bali kwa sanduku la kura.
Magazeti hayo hayo yanasahau yalichokiandika jana. Kuna mwanasiasa mmoja hapa nchini aliongelea maswala ya matunguli na mbio ya urais, magazeti hayohayo yalikuwa ya kwanza kumnanga kwa imani yake ya matunguli huku wananchi wakichagiza na kumuona kama ni mtu aliyepitwa na wakati, leo hao hao wananchi wamechotwa na habari ya mtabiri na kukubali kama matunguri yana nafasi katika kumpata rais.
Mwelekeo wa Taifa hili uko wapi kama hatuwezi hata kujua nchi inahitaji rais wa aina gani.