Utabiri: Rais ajaye Tanzania (2015) ni Mwanamke

Utabiri: Rais ajaye Tanzania (2015) ni Mwanamke

Mtabiri maarufu ametabiri kuwa Rais ajae Tanzania atakuwa ni mwanamke. Utabiri huo utakuwa umewakata maini Mh Laigwanani na Mh wa Mambo ya nje.

Source: Magazeti ya leo.

Kumbe CCM imeshampata mrithi Wa sheikh Yahya!

Ujinga mtupu!
 
hivi sijui humu jamvini watu huwa tunaamka na viroba vya jana??
hili nalo ni jambo la watu makini kulijadili?? watutunaamini ramli kuliko uhalisia??
 
Mtabiri maarufu ametabiri kuwa Rais ajae Tanzania atakuwa ni mwanamke. Utabiri huo utakuwa umewakata maini Mh Laigwanani na Mh wa Mambo ya nje.

Source: Magazeti ya leo.

Badala ya kutaja sifa za Rais ajaye watu wanataja majina! Au "uanamke" nayo ni sifa ya Kikatiba ya kuwa Rais jamani? Wengine wamethubutu kutaja hata "maeneo," kwamba Rais wa safari hii atatokea eneo fulani! Kwa kweli nchi haina mwelekeo kwa sasa!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ni ubaguzi tu wa kifikra na haulengi kusaidia chochte katika juhudi za kumpata Rais ajaye iwe kwa CHADEMA, CCM au CUF. Nitashangaa sana endapo tunaanza kugeuzwa kuwa taifa la kufanya mambo kwa kufuata watabiri. Inasikitisha kuwa pamoja na juhudi za mashirika na taasisi mbalimbali bado kuna watu wanamtaja mwanamke kana kwamba ni kiumbe cha tofauti na binadamu wengine. Kama lengo ni kuwavuruga wananchi basi hata hiyo nia inaweza isifikiwe! Tujaribu kuwa na mitazamo yenye kujenga zaidi kuliko kujikita kwenye udhanifu uso tija! Muda utaamua....
Mtabiri maarufu ametabiri kuwa Rais ajae Tanzania atakuwa ni mwanamke. Utabiri huo utakuwa umewakata maini Mh Laigwanani na Mh wa Mambo ya nje.

Source: Magazeti ya leo.
 
Na kama ccm watamtoa mgombea mwanamke basi cdm watashinda kiulaini
 
Nashangaa magazeti ya TZ yanaweka utabiri front page. Mimi niliposikia nilidhani ni kiongozi wa kitaifa katoa tamko hilo, kumbe ni wale wale akina Yahya.

Mkuu, wageni pamoja na wale walio nje wanatushangaa kwa vioja tunavyofanya! Maana hii ni marketing over proffesionalism (Journalism)!

Pili iweje badala ya kutangaza 'utabiri'! 'utabiri'..mkuu kumbuka mambo yale ya mafuriko, kikombe cha 'babu' wa Loliondo and the like!

Nchi yetu inakuwa na vioja visivyo mfano!Sasa baada ya hapo utaona debate itayokuwa katika vyama vya siasa...halafu pale "utabiri" usipotimia, mtabiri kusema "walimuelewa vibaya"...Hii ndiyo Tanzania!
 
Tumeona kwenye nafasi kubwa ya Uspika imekuwa ni kosa kubwa lililofanywa na CCM na sasa wanataka na Uraisi!! tusifanye michezo kwenye nyanja Muhimu Uraisi hauhitaji roho Nyepesi
 
Kazi moja ya shetani ni kujifanya unatabiri kumbe umetumwa useme
 
hivi sijui humu jamvini watu huwa tunaamka na viroba vya jana??
hili nalo ni jambo la watu makini kulijadili?? watutunaamini ramli kuliko uhalisia??

Haishangazi kwa nchi inayoongozwa na rais anayelindwa na majini, na hii ni kwa mujibu Hayati Sheikh Yahya, kauli ambayo haijawahi kukanushwa na Ikulu.
 
Akiwa mwanaume huyo mtabiri anyongwe. Kwanza anadhallilisha dini yetu ionekane hatujaenda shule.
 
Shekh Yahaya amefufuka tena? Naye alitabiri hivi hivi lkn alipochuka Vasco, akageuza kibao eti "si mnamuona anasura nzuri kama demu!" Hovyo kabisa taifa linaloendeshwa na magagula!
 
Itakuwa staili design ya iliyomuengua Sitta kwenye Uspika? Ambapo king maker Rostam alitoa amri bi Kiroboto ndiyo zamu yake kuwa spika, mzee mzima Sitta akajikuta anasalimu amri kuutema uspika kwa kuwa alishindwà kujigeuzà kuwa mwanamkè kama ambavyo magamba waliweka kama sharti ili uukwae uspika!

Hata hivyo mshindi wa jumla kati ya 6 na Rostam ni ambaye mpaka sasa ni mbunge. Kwa sababu yale mapambano yalipelekea king maker akubali kuwa ameshindwa na hivyo akaachia ngazi. Ila hii propaganda ya kutumia watabiri safari hii itashindwa, kwa sababu itapata upinzani wa kutosha hata ndani ya chama cha magamba. Tumeshaona watu washaanza kupanga safu za mashambulizi 2015, nakuhakikishia hoja ya "zamu ya wanawake" safari hii haitafanya kazi na kama wataendelea kung'ang'ania basi huo ndo utakuwa mwanzo wa mpasuko wa chama chao.
 
Mwalimu wangu mmoja aliwahi kuniambia ukisafiri na ukifika nchi yoyote ya kigeni kitu cha kwanza baada ya kukamilisha taratibu za kuingia kwenye nchi hiyo anza kusoma magazeti na kufuatilia vyomba vya habari vya nchi hiyo, humo ndio utajua wenyeji wako ni watu wa aina gani,ukianza kusoma habari za ujambazi,habari za wanawake kubakwa,habari za ushirikina na mambo ya uchawi utajua taifa hilo ni taifa la aina gani,vilevile ukisoma habari za teknolojia,uvumbuzi wa vitu na habari nyingine za maendeleo ya watu pia utajua taifa hilo ni taifa la aina gani.

Leo hii mtu akifika Tanzania na kusoma magazeti yetu na kukutana na habari za utabiri wa kuwa na rais mwanamke baada ya uchaguzi mkuu ujao atajikuta ana maswali mengi ambayo hatayapata majibu yake pengine mpaka atakapoondoka,baadhi ya maswali ni haya:

1.huo uchaguzi utafanyika lini?maana huwezi kujua huyo mwanamke kama ataendelea kuwa hai mpaka 2015,kwa sababu huo utabiri ni lazima awepo mtu mahususi anayetabiriwa.

2.je, kila mwanamke anafaa kuwa rais wa nchi hii?

3.je watanzania wana imani za ushirikina kiasi cha habari hiyo ya kipuuzi kupewa nafasi kwenye vyombo vya habari?

na maswali mengine mengi.

Taifa letu limekuwa ni taifa la uchaguzi kila siku habari za urais haziishi kwenye midomo ya watu na kwenye vyombo vya habari hasa magazeti yanatuongoza sana kwenye ujinga huu,na baadhi ya watu nafikiri wanaliona taifa hili ni la ovyo sana kiasi kwamba kila mtu anaweza kuwa rais,badala ya kuchapa kazi sisi tunawaza urais,wakati wenzetu wanawaza jinsi gani watakavyotuibia gesi,dhahabu,almasi.tanzanite,meno ya tembo,makaa ya mawe na maliasili nyingine sisi tunawaza urais ambao ni miaka mitatu ijayo.

hii ni aibu yetu na ujinga wetu,tubadilike na wahariri wa vyombo vya habari mtuongozo kwenye njia sahihi.
 
Magamba wanajaribu kutupima kama tunamkubali Migiro,lakini hana uwezo wa kuongoza nchi kwa sasa.
 
Mtabiri maarufu ametabiri kuwa Rais ajae Tanzania atakuwa ni mwanamke. Utabiri huo utakuwa umewakata maini Mh Laigwanani na Mh wa Mambo ya nje.

Source: Magazeti ya leo kama vile Majira na Jambo Leo

Utabiri wa kichawi huenda kichawi chawi na kimafumbo mafumbo. Anaposema Rais atakuwa mwanamke hana maana atakuwa na jinsia ya kike, ana maana atakuwa na tabia za kike; yaani mambo yake atayafanya kike kike.... tumeelewana hapoooo????!!! kazi ni kwenu!
 
Back
Top Bottom