Utabili wangu ni huu, Jiandaeni Kisaikolojia

Utabili wangu ni huu, Jiandaeni Kisaikolojia

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
3,976
Reaction score
12,600
Wakuu, kutoka kwa mdau.

Na Emily Mwakilembe

Baraza la Mawaziri linaenda kufumuliwa lote, kuondoa mabaki na kufuta nyayo zake. Si unajua huyu Bwana ni jasusi? Lazima akiacha mayai kwenye mfumo! šŸ˜„

Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanaenda kufanyiwa ā€œmagazijutoā€; yaani kutoa mabano, kugawanya, kuzidisha, kujumlisha kisha kutoa. Wale waroho wa madaraka, sasa tumbo moto!

Wakurugenzi nao wajiandae kisaikolojia. Hapo si kwa ukubwa sana, lakini mchezo umeanza kubadilika.

Mfumo wa Jeshi la Polisi, jiandaeni kisaikolojia! Mambo ni moto, isee. Bado joto lipo nyuzi 37°C. Ikumbukwe hii ni 2026, bado mwaka haujaisha tangu waapishwe. Bado sana!

Ninachoweza kusema kwa ukweli ni kwamba tunapitia wakati mgumu sana. Jamii haina umoja, Serikali haina umoja, vyama havina umoja, dini hazina umoja! Kila mtu anasema lake. Taasisi hazina umoja, wastaafu hawana umoja, kila mtu anasema lake. Kwa ujumla, nchi haina umoja.

Kama tukiendelea kuyaacha haya yakue na kuzeeka pasipo maridhiano, nakuhakikishia tutafika mahali tukose hata mzee mmoja anayeweza kutuliza mawimbi ya hasira na chuki kwenye kasia ya nchi yetu. Maana hata wazee wanabaki kwenye makundi yao, wengine wanasema hili, wengine lile.

Sijui... ngoja niendelee kutazama mwisho wake ni upi. Maana hapa hata mbwa amepoteza uwezo wa kunusa, sijui kama atakumbuka kwao! šŸ˜‚

Utabili wangu nimeuweka mezani. Muda ndio utasema kama nilikuwa nabashiri au nilikuwa nasoma alama za nyakati.
 
Uzi wa kipumbavu wenye kuleta taharuki, sisi watanganyika tunapitia vipindi vigumu tangia uhuru ..Wanaopitia icho kipindi kigumu sasahivi ni ass kissers wa CCM na CCM wenyewe..Sina huruma na mshirika yeyote wa CCM na serikali Yao dhalimu Tena ikiwezekana wote wapigwe radi ya mafungu wafie mbali
 
Back
Top Bottom