Usiri ajira TISS

Usiri ajira TISS

Jeshi halitoi ajira, isiyo ajira na hakuna mshahara lakini wanapata malipo, wanalipwa.

Ukijiunga na jeshi unakua umejiandikisha kulinda na kutetea katiba.
Kulinda mipaka ya nchi etc, ikibidi hata kwa gharama ya uhai wako.

Sasa kuna ajira gani duniani muajiriwa anakuwa tayari kufa? Kama wajua itaje.
Underground mining
 
Inategemea neno 'ajira' na 'mshahara' unatafsiri kwa mtazamo upi..

Kwa kuwa tuko huru kujadili kwa mitazamo mbalimbali, inawezekana ukawa sahihi pia!!
 
Sio ikibidi ukijiunga jeshi wewe moja kwa moja unakua umesaini mkataba wa kifo, maana unaenda kucheza na vyuma vya moto na vile vyuma vinauwezo wa kukufanyia Mambo mawili pekee ima vitakuua au kukutia ulemavu wa kudumu, ushaelewa mkuu
Hapa hoja yako ni ipi mkuu wangu?

Ni kazi gani ambayo mtu akiifanya atakuwa ameepuka kifo?
 
Kama wanaorithi wanaubora stahiki wacha iwe hivyo.

Sawa boss. Vipi kama kuna wengine wenye ubora kama wao au zaidi na hawamo kwenye mnyororo wa kurithishwa japo nao ni Watanzania na wanahaki ya kulitumikia taifa lao kupitia nafasi hiyo?
 
Usalama taifa mnavyowachukulia mnawapaisha sana.

Hao hadi polisi wana hadhi ya juu kimamlaka, hao ni watumwa wa ikulu na rais aliyepo madarakani.

Ila kiutendaji wapo kila kona.

Wenye nchi yao ni hayo majamaa ya bakabaka ndiyo yaliyopewa nguvu ya ulinzi wa nchi.

Madogo wa usalama wanatishia sana raia wema.
Hawa jamaa kitendo cha kutopewa Power ya ku enforce Law ni Kitendo Kizuri sana wangetuumiza mtaani
 
Jeshi halitoi ajira, isiyo ajira na hakuna mshahara lakini wanapata malipo, wanalipwa.

Ukijiunga na jeshi unakua umejiandikisha kulinda na kutetea katiba.
Kulinda mipaka ya nchi etc, ikibidi hata kwa gharama ya uhai wako.

Sasa kuna ajira gani duniani muajiriwa anakuwa tayari kufa? Kama wajua itaje.
Ajira ya kuchimba madini watu wako tayari kufa. Jeshi ni ajira na wanalipwa mishahara mizuri sana hasa Maafisa.
 
Hata viwandani, kwenye uchimbaji madini na udereva watu wanakufa au kujeruhiwa.
Sio ikibidi ukijiunga jeshi wewe moja kwa moja unakua umesaini mkataba wa kifo, maana unaenda kucheza na vyuma vya moto na vile vyuma vinauwezo wa kukufanyia Mambo mawili pekee ima vitakuua au kukutia ulemavu wa kudumu, ushaelewa mkuu
 
Hii tabia watu wengi sana hata vilaza kabisa huwa wanayo, hiki sio kigezo au skill muhimu na ya kipekee kupewa kazi ya ujasusi.
Kuwa extrovert sio tiketi ya kazi/ajira ya ujasusi.
Mkuu mimi huwa nina tabia ya kujichanganya sana na watu tofautitofauti na napata taarifa nyingi sana, kwani nina iwezo mkubwa sana wa kusikiliza na kupata taarifa nyingi hasa nikiwa nakula bia zangu
 
Labda tuanzishe kampeni: freeTiss

1.TISS iwe taasisi huru isiyofungamana na upande wowote....CCM ama upinzani,

2.Pawepo na sheria kali za kuzuia political institutions ( hadi rais) kuingilia TISS,
3. Wafanyakazi wa TISS wapewe kinga ya kuepuka kuwa persecuted na politicians hasa watawala
4.Pawepo na TUME ya kibunge iliyokula kiapo ya kufuatilia utendaji wa TISS..(Hii itafanyakazi kama tuna bunge la wananchi, sio la sasa)
5.Mkurugenzi mkuu wa TISS ateuliwe na Rais lakini apitishwe na Bunge

6.TISS isiwe idara chini ya ofisi ya Raisi au Ikulu:TISS iwe agency iliyoseparate kabisa..Inapokuwa idara Ikulu ni rahisi sana Rais (Mwanasiasa) kuigeuza ifanyekazi kwa mtazamo wake.

7.TISS ipewe nguvu za kuuma: Kukamata na kuweka maabusu maalumu za kwao zinazojulikana kisheria.

8.TISS isishughurike na kulinda maslahi ya watawala na kuhakikisha wanabaki madarakani, TISS ijikite katika kulinda maslahi ya TAIFA na wananchi wake wote bila kujali itikadi za kidini, kiuchumi n.k.

9.TISS itengeneze ikague na kuhakikisha mihimili mingine ya dola inatenda haki..na wawawajibishe ipasavyo wanaoenda kinyume: Mfano Polisi,Magereza

10.Madawa ya kulevya, Rushwa, Ufisadi viwe vitengo chini ya TISS. Kwa kuwa TISS itakuwa na access ya taarifa sahihi ni rahisi kushughurika na hayo masuala ambayo yanahatarisha usalama wa wananchi na Taifa.

11.Sheria ipitishwe na iwe kosa kudisclose member wa TISS kwa namna yoyote ile: Kama unamjua kaa kimya tu..tunza kifuani.

12.Members wa TISS wale kiapo kizito sana cha utii kwa Taifa na wananchi na waape kulinda KATIBA ya nchi.. kwa akili zao zote, utashi wao wote, uwezo wao wote etc....

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom