Habari wakuu
Twende kwenye mada.
Kama ww ni me uko na mpenzi wako na anaonyesha mapenzi yote kwako, anakujali, anakupenda yaani ile kwelikweli..., nakusisitiza rudisha upendo kwake na muoneshe kumjali kama anavyokujali.
Mwanamke anaweza akawa anakutumia text hauzijibu, anakupigia unapuuzia kupokea na pengine huoneshi upendo kwake, unajali kazi tu na kutafuta pesa, my dear huyo mwanamke siku akija kubadilika akaamua kutazama pembeni ndugu yangu huwa ni ngumu sana kumfanya arejee... it is very hard thing.
Mwanamke akiamua kupenda anawekeza kila kitu, hisia, maisha yake na cha muhimu kingine anachowekeza ni muda wake pia..., ni vizuri kama una malengo nae ukamuonesha upendo pia.
Daah inauma..
Yaani nilikuwa najifanya niko bize na kazi, simu zako sipokei si asubuhi, sio mchana usiku ndo kabisaa nakuwa nimechoka balaa nikifika home naishia kulala hoiiiii... ila sijilaumu ni nature ya kazi yangu. asubuhi nakuta ulinitafuta jana yake daah naishia kukupigia tunaongea dk 2 then napotea daaaah siamini kumbe ndo nilikuwa nakupoteza.
Nilijiamini kwamba hutoweza kuniacha kwa jinsi nilivyokuwa nakujali, niliamini vile vizawadi nilivyokuwa nakuletea siku mojamoja visingekufanya ubadili mawazo...
Ilianza kama utani inapita siku mbili mara tatu mara wiki bila kunitafuta mmh nafsi ikaguna maana nilizoea kuona missed calls zako. Yaani siamini leo hii mm ndo nakutafuta hata simu yangu hupokei daah hata text hujibu duuh.
Sasa ndo nimeelewa communication ni kiungo muhimu sana kwenye relationship.
Leo yapata miezi miwili ndo nimeamini rasmi umeniacha duh.
Wakuu mapenzi sio pesa namaanisha mapenzi ya kweli sio pesa, ukiwa na mwanamke anaekupenda kweli pesa inakuwa haina thamani yoyote.