Usia wangu kwa Zitto na washirika wake

Usia wangu kwa Zitto na washirika wake

zitto mshirikina sana aliondoa mkono wa kulia wa mudhihir mudhihir kisa alimkomalia atimuliwe bungeni...naona na mkono wa dr slaa aliukosa kos sababu slaa ana Mungu. kweli uyu muha kaaga kwao.
Hehe, Matumbo bwana, kwani kwenu Iringa hakuna haya mambo ya kukata mikono ya watu kwa njia ya uchawi?
 
Ukiwaondoa hao itawaweka akina nani? Kila uzao wa kizazi cha mfumo huo kimeoza. Suala la muhimu ni kutokomeza mfumo mzima, ambao wewe mwenyewe, watoto, wazazi wako mpo ndani. Kwa maama nyingine inabidi uikane nafsi yako bila hivyo unapoteza muda wako.
 
Tuwachukie wao lakini kamwe sio watoto wao. Tukiuchukia mfumo na kama unahusisha na usultani, basi kwa kuufumua mfumo na kuweka tuutakao hiyo ya watoto itajisort. Mambo ya kupatiliza wana maovu ya baba zao sio fair game.
 
Ukiwaondoa hao itawaweka akina nani? Kila uzao wa kizazi cha mfumo huo kimeoza. Suala la muhimu ni kutokomeza mfumo mzima, ambao wewe mwenyewe, watoto, wazazi wako mpo ndani. Kwa maama nyingine inabidi uikane nafsi yako bila hivyo unapoteza muda wako.

Nimekuwa nikisema hapa kwa muda sasa, watu wanataka sijui kuvunja muungano, kubadili katiba, kuondoa CCM waweke CHADEMA, wakati tuna matatizo ya kina kirefu zaidi ya muungano, katiba na CCM.

Ingawa sitaki kuyadhalili maswla taja hapo juu, naona pia kwamba tuna matatizo ya kiutamaduni yaliyopita kina cha vyama, katiba na muungano.

Na kama hatutaweza kuyabadili haya, kamwe tusifikiri kwamba tunaweza kutatua matatizo ya nchi yetu kwa kubadili vyama, katiba au muungano.

Migogoro ya sasa ya CHADEMA ni kithibitisho kwamba tuna safari ndefu.
 
Vijana wa chadema amabo wote mnashutumiana na kujipaka kinyeshi miili yenu tumewasikia wote na tumewaelewa vizuri sana. Sisi wananchi ambao kila siku tunahangaika na maisha magumu, shida ya umeme, shule mbovu, barabara mbovu ufisadi utawala mbovu hatukuwapenda ili mtuletee haya.

Naomba niseme wazi mmesaliti umma wa Watanzania ambao tumekuwa tukijitolea mida yetu, mali, kuhakikisha chadema inakuwa mkombozi wa kweli wa Mtanzania.

Bila shaka tamaa yenu ya madaraka fedha roho mbaya, hila fitina, kujikweza nk ndio inawafanya mnashindwa kuelewana na kupenda ukubwa.

Mmeonyesha wazi vijana bado hamjapipikika na kweli bila shida hamfai wote mliotajwa hapa sio tu kuwa viongozi hata wa vitongoji hamfai. Nina hakika kila mlipo kama ni kazini, ndani ya chama mna migogoro mingi na wenzenu. Tamaa ya madaraka bila subira inawaponza.

Kwa sababu chama kimejengwa chini ya msingi mkubwa sana wa nguvu ya umma sitaki tena kuona watanzania wanasoneka eti kwa sababu ya kajikundi kadogo.

Mijadala yote hii inayoendeshwa na akina Ben, mamuya, Shoza, Habibu, ZZK, Kitila nk iishe sasa. Ukiendeleza mijadala hii ni afadhali urudishe kadi ya chama halafu tujue nia yako ni nini.

Wakati mijadala hii inakoma naomba chama kiwaite wote mliotajana hapa mueleze matatizo yenu ni nini ndani yachama.

ZZK unahudhuria vikao vyate vya chama shauri kundi lako mtumie vikao vya chama mueleze matatizo yenu kama ni Uraisi mseme, kama ni uenyekiti mseme, kama ni Bavicha mseme.

Narudia tena kwa msukomu wa moyo wangu, kwa mapenzi makubwa niliyonayo kwa Watanzania, kwa uchungu mkubwa nilionao kwa umasikini wa watu wangu, na mapenzi yangu kwa chama na heshima kwa viongozi wote waliojitolea kwa hali na mali bila tamaa ya madaraka kujenga chama nawaasa ifike mwisho.

Atakaye endelea nitatangaza mgogoro naye na chama cha demokrasia na maendeleo. naomba mjue wazi huo ugomvi wenu unawahusu ninyi wenyewe na tamaa zenu na ukosefu wenu wa hekima na matumizi bora ya elimu. Chadema ni ya wananchi na tumechoshwa na vituko vya CCM na tumechoshwa sasa na vituko vyenu, tuacheni wananchi tupumue. Huo ugomvi wenu ni umasikini tu wa mali akili na kutokuwa na malengo.

Leo hii wote mnaonekana wasaliti, wajinga, majuha, wehu, wazandiki, tamaa mbaya, wachawi, walevi wa madaraka na vijana msiojua maana ya uongozi na sifa za kiongozi wote hamna.

Nasema tena mjadala wa kurushiana nuclear umefungwa Rasmi.
Demokrasia ikivuka mipaka ni ukichaa .

Chief Mkwawa
Dhambi ya makundi haiishi kila kundi litakuwa na kajikundi. nakujikundi kajikundi mpaka wote msamaratike. Fanyeni kazi kwa bidii na mafanikio mtayaona acheni tamaa mbaya.
 
Natoka Kigoma... Nimeaga kwetu... Nitakufa kwa amri ya Mungu... Siogopi kufa. ..Iwapo kifo changu kitatokana na mkono wa mtu, sidhani kama kwa mtu huyo kama hata panya atabaki nyumbani kwao. (Zotto Kabwe - Mbunge Wa Kigoma Kas 2012).
 
Huyu binti anayeitwa Juliana wala huwa sielewi alipataje uongozi wa CHADEMA, maana uwezo wa kujenga hoja ni ziro kabisa. Wote tunamwona Heche kila leo anazunguka mikoani kwa shughuli ya kujenga chama, anaiacha familia yake na shughuli zake. yet watu wanaona laki saba ni hela asiyostahili. Ni mpuuzi tu atakayesikiliza hoja za Juliana na kuzikubali.

Kumbe na wewe wale wale tu wewe upo upande wa Ben, wala huu siyo usia ni muendelezo wa mapambano yenu ya kijinga.
 
Nashawishika kuamini kuwa ujasiri wa Zitto umejengwa juu ya nguvu zake za Sangoma (kama anavyotuhumiwa) na wanamikakati wake.
tetere,
Hapo kwenye bold, sio kwamba anatuhumiwa kwa ugagula, ameandika mwenyewe kwenye ile thread anayomjibu Ben Saanane, kwamba "AMEAGA" huko alikotoka. Wewe ni mtu mzima, unajua 'KUAGA' ni kitu gani.
 
Last edited by a moderator:
Kwikwikwikwikwikwi,Ejhoooooooooo mama weeeeeee nipo nacheka kwa staili hii CHADEMA Ikulu mtabaki mnaisikia tu!
 
Hukumu ya Lema vipi jamani? Moshi mweupe haujaanza kuonekana mlioko Dar.
 
Kitu kinachojitokeza katika malumbano haya ni jina Zitto.
Hakuna anayeleta mashtaka, anajitetea au anayetuhumu aliyeandika bila kumtaja Zitto.

Hakuna shaka kuwa Zitto alikuwa anajua wazi kabisa kuwa kuna hujuma ndani ya chama. Akiwa naibu katikbu mkuu, Zitto hakuchukua hatua za kukinusuru chama.

Zitto ametajwa tena kwa ushiriki wake na Kafulila. Ni Kafulila huyo huyo aliyeanzisha gogoro la ndani ya CDM.
Alipoondoka akasema ni chama cha ukabila. Hakuna mahali ambapo Zitto amewahi kukana kauli za mshiriki wake.

Kauli ya Zitto kuhusu ushirikina na tuhuma tunazosoma za watu kwenda kula amini mbele ya masangoma hazina shaka kuwa ZZK ni mshiriki mzuri wa kundi hilo.

Kuna jambo linajitokeza pia. Hussein Bashe ambaye ni mshiriki mkubwa wa Lowassa naye aliwahi kushiriki mkutano wa uasi. Hii maana yake ni kuwa tayari watu wa CCM wanaoona CDM kama kikwazo hasa Dr Slaa walishaingia katika ulingo.
Lakini pia kama Bashe aliingia ni kwa lipi litakalomshinda Nape hasa tukizingatia kuwa kauli zake ndizo zimeibua sehemu kubwa ya tafrani?

Ilishadaiwa kuwa Zitto alilishwa sumu na kulazwa Agakhan. Ingawa alikana madai hayo ni wazi kuwa madai hayo yalitokana na washirika wake au yeye kupitia washirika wake ambao leo tunajua wana madai ya kumtuhumu aliyeasi kwa kuwa na mkakati wa kuwekewa sumu.

Kwa uchache tu ni kuwa ushiriki wa Zitto katika tuhuma hizi ni mzito sana. Japo ni tuhuma ushahidi wa kiamzingira haumruhusu Zitto kuendelea na nafasi ya unaibu katika chama.
''Mke wa mfalme akituhumiwa kuzini hata kama tuhuma hazijathibitishwa basi hafai kuwa mke tena''

Ni wazi kuwa nguvu iliyokuwa nyuma ya Juliana Shanzo tuliyoipigia kelele sana sasa inajulikana.
Juliana amepoteza hadhi na heshima ya uongozi ndanii ya CDM na anatakiwa ajiuzulu samba mba na Zitto.

Ninarudia wajiuzulu pending to investigation by independent organ. Simaanishi wafukuzwe kwasababu natural justice inataka watu wote wasikilizwe.

Ushauri wangu kwa CDM ni kuwataka Zitto na Juliana wajiuzulu au washurutishwe kujiuzulu kwanza ili kutoa nafasi ya justice kutendwa na si kutendwa tu bali ionekane inatendwa.

Utetezi wa Zitto hapa jamvini umeonyesha bila kificho kuwa hana hoja and he is an 'epicentre' of this fracas.
Watetezi wake na wanaomtuhumu wote kwa pamoja wamedhihirisha bila mashaka kuwa Zitto ni mshiriki mkubwa na mtu muhimu sana katika mgogoro huu.

Zitto na Juliana wamepoteza sense of propriety, legimacy to lead, moral authority na leadership quality.
Hawa wawili ni lazima kwanza waanze kukinusuru chama na ikibidi chama kijinusuru kwa kupitia wao.

Zitto kama kiongozi anatakiwa apime endapo tuhuma hizi ni muafaka kwa chama chake na mustakabali wake kisiasa siku za usoni. Nasema hayo kwasababu moja, tuhuma zote ziwe za upande huu au ule zinamtaja kiongozi mkubwa sana kama mshiriki.

Baada ya hapo ndipo tutaeleza nini kifuate. Bila Zitto na Juliana kujiuzulu chama kinaelekea kubaya sana.
 
Hebu twende next level ya uchambuzi wako. Hawa jamaa wanaotajwa wanavyanzo gani vya mapato? Walau nimemsikia Mwampamba kwenye uzi mwingine akilalamika kuwa kwenye cdm wapo wanaokula kutumia kodi za wananchi, ruzuku za chama....na mipango ya hilo kundi imeghalimu kiasi gani kisha tujue kwenye njia za kipato zinazofahamika kama wao wanaweza kufadhuli ama kuna mtu mwengine kuliko saa8 na wengine ndani ama nje ya cdm wanaofadhili mvurugano huo.
Tatu, Mchange anasema, Ben alikuwa anamtafuta Zitto ili akifadhiri kikundi, wakati mstari wa Nne, wakati Mchange na Mwampamba wakidai kwamba Ben ndiye aliyekuwa analifadhiri kundi la kukihujumu chama na kuwachafua viongozi wa chama. sasa hawa vilaza mbona wanajichanganya kwy kauli zao, mara waseme ben ndio ana fadhili, mara anamtafuta zitto ili afadhili kikundi. sasa tuwaelewe lipi au ndio kuchanganyikiwa? chama chukue maamuzi magumu hawa ni kuwafukuza tu hakuna cha mchange, mtela, shonza, nyakarungu, gwakisa wote ni kuwa sack out.
 
Hata mimi siungi mkono mpango wa kufukuzana. Ila yataka moyo kumvumilia mtu kama Mwampamba. Kwa kweli hoja zake zile zina utata mkubwa sana. Bado naona kwamba Mchange anaweza kuonywa na akabadilika na kuwa mwanachama mtiifu kabisa kwa CHADEMA, lakini sina uhakika na Mwampamba, Juliana na wengine ambao bado hawajatoa utetezi wao. Ukisoma hoja za Mchange, unaona kabisa ni mtu anayejutia kosa lake, lakini si hoja za Juliana na Mwampamba.

Mkuu Lukolo, huyu Mwampamba ni janga kwa CHADEMA! Mwampamba mwaka 2010 aligombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki, wananchi kwa hamu ya ukombozi wa kweli tulimpiga kura kwa uaminifu mkubwa, ikiwa imebakia kata moja kura kuhesabiwa Mwampamba alikuwa anaongoza kwa kura 10,000 lakini cha kushangaza Mwampamba aliziuza kura zetu kwa Godfrey Zambi wa ccm.
 
Ndugu zangu,
Watanzania tuna usemi usemao “Mungu hamfichi mnafiki”. Usemi huu umethibitika kupitia malumbano ambayo yamekuwa yakiendelea kwa siku kadhaa hapa JF. Kwa muono wa haraka haraka tunaweza kutambua kwamba wote wanaolumbana ni wasaliti kwa CHADEMA na wamekuwa siku zote wakijipambanua kama wapiganaji wakati kwa hakika walikuwa ni wanafiki na wasaliti wakubwa wa watanzania wanaiangalia CHADEMA kama chama mbadala kwa ukombozi wa nchi yetu. Nashawishika kuamini kwamba CHADEMA ina Mungu, na Mungu hajataka hawa akina Ben na kundi lake waukwamishe mpango wa Mungu. Hatimaye ameamua kuwaweka peupe na kuwafanya wafarakane wao kwa wao. Kwa hakika hii ni hatua mhimu sana katika kuelekea kuwa na CHADEMA yenye umoja na malengo ya aina moja ya kushika dola na kuwakomboa watanzania. Maana kama hawa wanafiki wangeendelea kuwepo hadi 2014, ni dhahiri wangekwamisha juhudi nyingi za kuiwezesha CHADEMA kuchukua madaraka katika serikali za mitaa na hata nchi mwaka 2015.
Nimezisoma kwa umakini mkubwa sana hoja zote za upande wa Ben, na ule wa akina Machange. Na nina mambo kadhaa ambayo nimeyaona hapa, na ningependa niseme machache kutokana hoja hizi.

Katika mabandiko ya Ben na Mamuya, wote kwa pamoja wanakubali kwamba Ben alikuwa ni mmoja wa waasi na alishiriki kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza mipango na mikakati ya kukihujumu chama na hasa uongozi wa juu wa chama (mwenyekiti na katibu mkuu wa chama), lakini baadaye akajiondoa kwenye hili kundi na kuanza kulipinga. Katika bandiko la Mchange na Mwampamba wao kwa pamoja wanaonyesha kwamba Ben ndiye aliyekuwa mwanzishaji wa hili kundi lililolenga kukivuruga chama. Na inaonekana alifanya hiyo kazi kwa kutumia kiasi kikubwa sana cha pesa. Lakini hawasemi baadaye ilikuwaje na ni kwa vipi walishindwa au walifanikiwa kutekeleza hiyo mipango ya Ben Saanane. Lakini hoja hizi zinaonekana kuwa hazina uzito kwa kuwa tayari Ben alishakiri kwamba alikuwa ni msaliti kwa chama. Kwa hiyo Ben amewawahi (pre-empty) akina Mwampamba katika hili kwa kuwa tayari tunafahamu ushiriki wa Ben katika haraka za kumhujumu Heche na hata uongozi wa juu wa CHADEMA.

Lakini la pili, ukisoma kauli za akina Mchange, Juliana, Mwampamba na mtu anayeitwa Taswira, inaonekana kwamba Ben Saanane alikuwa anatumwa na Dr Slaa kwenda kuunda hilo genge la kukihujumu chadema na uongozi wa juu wa CHADEMA. Hii hoja haileti maana kabisa. Sidhani kama hata mtoto mdogo anaweza kukubaliana na upuuzi huu kwamba Dr. Slaa alimtuma Ben akaandae kikundi cha kumhujumu yeye Dr. Slaa. Huu ni ulimbukeni uliopindukia. Na katika hili, nafikiri ant-Ben, wamekoboa. Hawana hoja ya msingi hapa. Ni wazi kwamba Dr. Slaa anatamani kubaki na jina lililosafi mbele ya jamii na atakuwa ni mwendawazimu iwapo ataamua kuandaa kundi la kuchafua yeye mwenyewe. Hapa hamjanishawishi bado. Mkatafute sababu nyingine.

Tatu, Mchange anasema, Ben alikuwa anamtafuta Zitto ili akifadhiri kikundi, wakati Mwampamba anasema Ben alikuwa anamtafuta Zitto ili ampe sumu. Hapa kuna mchanganyo tayari. Inaonekana hata hamjajipanga na kuelewa ni nini mnataka kukiwasilisha kwa jamii. Katika hili Napata hofu kwamba hili kundi la akina Mchange lilikuwa linamlisha Zitto maneno ya fitina na uchonganishi dhidi ya Ben kwa kuona kwamba Ben amejitoa kutoka kwao. Zitto, ni vema ukayachunguza kwa umakini mkubwa maneno ya hawa akina mchange na mwampamba. Anayetaka kukulisha sumu hawezi kufanya kazi ya kukutafuta mchana kweupe. Atatumia njia nyingine yoyote lakini siyo kuja uso kwa uso anakutafuta. Hivi unataka kusema kama Ben alikuwa amepewa pesa ya chama ya kuhakikisha anakuua angeshindwa kukutafuta popote? Hata Dodoma angekufuata ukiwa bungeni. Kama hawa jamaa zako walikuwa wanakuambia haya, ni dhahiri yana walakini.

Nne, wakati Mchange na Mwampamba wakidai kwamba Ben ndiye aliyekuwa analifadhiri kundi la kukihujumu chama na kuwachafua viongozi wa chama. Ushahidi wa kimazingira unaonyesha kwamba Tuntemeke and company walikuwa wapo busy kuzunguka kwenye mitandao ya kijamii (facebook, jf etc) kumchafua Dr Slaa kwa maneno ya hovyohovyo, na kuwauzia akina Nape siri za ndani za chama na za Slaa, ili kumfanya Slaa adharirike na kupoteza mvuto ndani ya chama na kwa jamii kubwa ya watanzania. Lakini ni bahati mbaya kubwa kwamba hakuna popote nilipoona Ben akimkashifu kiongozi yeyote, si Zitto wala Slaa au kiongozi wa juu wa CHADEMA. Kama kwa hakika Ben ndiye aliyekuwa analifadhiri hili kundi la uasi ni vipi tena kundi hili likaifanya kazi ya Ben kiufasaha, na kumsafishia Zitto njia ya kuelekea kwenye Uraisi ilihali halikubaliani na hoja za Ben. Hapa kimantiki haiwezekani. Hili kundi lilikuwa linafanya kazi ya mtu mwingine, tofauti na Ben Saanane.

Tano, ukiuangalia mwanzo wa migogoro hii yote ni Zitto kuutaka urais. Na hili kundi linaloongoza propaganda za kumchafua Slaa na kumsifia Zitto lina nia moja tu ya kumuwezesha Zitto kupata Urais. Hili kundi linamwona Slaa ni tishio ndani ya chama kwa nafasi ya urais, na hivyo linajaribu kuibua kila aina ya propaganda ili kumfanya Slaa aonekane hafai kwa nafasi hiyo ya urais. Kama tatizo siyo urais, kwanini kundi hili halimchafui Tundu Lissu au Mabere, au Prof Safari, au Mnyika au Mbowe? Tatizo ni Slaa kwa kuwa ana potentials za Urais. Kwa ushahidi wa kimazingira, Zitto ndiye anayelifadhiri hili kundi la akina Mwampamba, Mchange na wenzake wanaoendesha propaganda mbaya dhidi ya Dr. Slaa, ili kumuwezesha yeye Zitto kukubalika zaidi kwa wanachama. Katika hili hamuwezi kujinasua.

Sita, namfahamu Zitto tangu akiwa kiongozi wa DARUSO pale UDSM, ninamfahamu kama ni mtu mwenye misimamo na asiyeyumbishwa na kitu chochote. Ni mtu anayejiamini, asiyemwogopa mtu wala matokeo ya misimamo yake. Lakini pia namfahamu kama ni mtu mpenda madaraka sana. Na hili limejionyesha pale alipoanza harakati za kuutafuta uenyekiti wa CHADEMA, na baadaye kuutafuta urais. Ni dhahiri akibahatika kuwa Rais wa Tanzania atautaka pia Urais wa Africa Mashariki, Africa na hatimaye urais wa dunia kama utakuwepo. Mimi sipingani na uchu huo wa madaraka ilimradi anaamini kwamba anao uwezo wa kuongoza, maana hiyo ndiyo demokrasia. Lakini sikubaliani na approach yake ya kuutafuta urais, wenzake wote wanaoutafuta urais hata wale wa ndani ya CCM hadi hivi leo hawajajitangaza, yeye amejitangaza ili kiwe nini kama si kwa nia ya kujenga haya makundi ya akina Mchange? Zitto usipokuwa makini, hata kama utapata urais, unaweza kuwa Rais mbovu kumshinda hata Kikwete. Na unaweza ukaua kabisa matumaini ya watanzania dhidi ya vyama vya upinzani.

Lakini zaidi ya yote, Zitto una bahati mbaya sana kwamba watu uliowachagua kukupigia debe au kukubeba kuelekea huko unakotaka kufika ni weupe mno katika uwezo wa kuchambua mambo. Hili nimeshakuandikia mara kadhaa. Hivi watu kama akina Mchange, Mwampamba na Juliana utawalipa fadhira gani utakapotokea kuwa Rais? Nadhani hata kwenye nafasi ya ukuu wa wilaya tu hawawezi kufit, kwa jinsi wasivyojua kupembua mambo. Hawa watu uliowatuma wakupigie debe na kumkashifu Dr. Slaa ili apoteze mvuto mbele ya jamii na akose sifa ya kugombea Urais ili wewe ugombee, wamekosa maarifa ya kufanya kazi hiyo. Badala ya kukupigia debe wenzako wanakisambaratisha chama. Ni mwendawazimu tu atakayeanza kulivunja daraja kabla hajavuka mto. Wewe unautaka urais halafu daraja la kukupeleka kwenye urais unawatuma akina Mchange na kundi lake walivunje. Kwanini usingetulia, ukashirikiana na wanachama wenzako, mkajenga umoja wa chama, mkakitangaza na kukikuza chama kwa bidii, na baadaye watu wakuone kwamba unaweza, na wakupe hiyo nafasi? Kwanini usifanye mambo mazuri ndani na nje ya chama ili sisi tukuone kwamba unatufaa kuwa rais? Rejea kauli ya Butiku pale Nkurumah.

Zitto, kwa sasa huna sifa za kuwa Rais. Ukishaona unajiandaa kuingia kwenye mpambano halafu mpinzani wako anakusifia, basi ujue huna kitu wewe. Ni ajabu sana kwamba akina Nape, Le Mtuz na January Makamba wanakusifia wewe na kumkashfu Slaa. Kwa mazingira haya tu, ni dhahiri kwamba Slaa ndiyo tishio kwa CCM na si wewe. I am sorry, lakini huo ndiyo ukweli. Nadriki kusema kama nia ni kupata Rais kijana, basi John Mnyika au Tundu Lissu wanaweza kuwa macandidate wazuri zaidi kwa nafasi ya urais kuliko wewe. Ni vema ujitafakari, na uangalia misimamo na determinations za hao niliowataja, halafu jilinganishe na wewe.

Mwisho, napendekeza kwamba, kwa kuwa unafiki wenu umeshawekwa wazi, basi yavunjeni haya makundi mliyoyaunda ya kummaliza Dr Slaa kisiasa, mrudi chamani mkaombe radhi kutokana na ushiriki wenu wa kukihujumu chama na

umejitahidi kuandika kile unachozani kuwa ni sahihi lakin ukwel unabaki palepale,hayo ndo majungu na unafiki wa kubase upande mmoja
 
pamoja na maelezo yako uliyoyatoa bado naona unausifu upande mmoja na kuukandamiza upande mwingine kweli huyo ndo Mungu alivyo?unayemsema ww?mm naona wote sio wasafi,kwahiyo acha unafiki wa kuegeme upande mmoja bila hata aibu.
 
THIS SCANDALS WILL SLOW DOWN OUR SPEED AND POWER TO OVERTHROW CCM, AND THEY MIGHT WIN 2015 ELECTIONS
​

GUY'z, am very disappointed by this fellow Tanzanians who always make 1 step ahead then makes 3 backwards, I wasn't born politician but my principles guides me to what I need from politicians, Just to share my small Idea to fellow Tanzanians who also might be like me or not.., If you like it take it and we will make Tanzania a better place, otherwise, we wont help in anything by just sitting back and claim that politics is a dirty game.

Since Nape brought this issue up of hon. Dr Slaa owning CCM card,I've been trying to add my few minutes to my politics break at least to figure out the thinking capacity of Tanzania's. And also I have managed to go through this thread in jamii forums that mentions how some groups within and out of CHADEMA might be involved and how some of the BAVICHA leaders in district level may be playing a great part to make sure they succeed in there plan of overthrowing DR. from his position.
Its o.k, but FEW LINE NEXT, POINTS TO A KIND OF DECISION WE TANZANIA'S SHOULD HAVE NOW.

*************************************************************************************
CCM has leaded has for so long enough(HAVE MENTIONED THIS WITHOUT BLINKING OF EYES), lets make changes by putting another person from a different party in 2015 election. Nothing new in CCM can be implemented to save TANZANIA. We are tired of repeating issues just because of poor governance. Let me just give a simple example from the country that we are North Eastern bordered to. Take a look how fast the economy of KENYA is growing, check what is their dream in 2030. And this speed of economy growth in Kenya has been facilitated by the political situation in the country, Look the changes they have made in politics, look how they play politics, due to this changes the leaders are working hard to provide good to there citizen that they may maintain there positions. For us we will remain making noise under stagnant thinking and pointing fingers to one another.
Fine you may say am wrong, then tell me why KENYAN economy is higher and growing faster than OURS?

TIME HAS COME , LETS MAKE CHANGES...... lets don't care who from a strong opposition party (CHADEMA) may be the president, Lets focus on overthrowing CCM from that position, lets try with another party there and If also they fail we keep on changing, this is the meaning of a MULTIPARTY country,the presidential seat wasn't made for one party forever. LETS KEEP ON CHANGING, and if possible, every after 5 years, we have a party change in the seat,but keeping on with this scandals will lower our power to overthrow CCM and they will take seat again in 2015.

This is my view in my political break,
 
Poor analysis and one sided.....Lukololo uwezo wa uchambuzi wako katika mambo ya kiintelijensia nina shaka nao.Kabla sijaingia kiundani hebu jaribu kugoogle 'Too fast..too furious Mexico Guns' utatambua hata nchi huwa zinapandikiza watu wake kutenda kitu ili kuwakamata waarifu.Nirudi kwenye hoja sasa, ni kweli Slaa anaweza kupanga huo mpango ili kuweza kuwatambua maadau wake, na ni jambo la kawaida katika ulimwengu wa espionage.Pili Dr.Slaa si tishio kwa Zitto hata kidogo na nataka ninukuliwe vizuri watu wengi wanaomfuata Dr.Slaa si watu wenye fikra pevu kwa kuwa Dr.Slaa hapendi kupingwa anapenda umungu mtu na kwa sababu hiyo Slaa ni tishio kwa slaa mwenyewe. Kuhusu uhusika wa Zitto nahisi huu ni wakati wa muafaka wa kudeal na zitto kama ni kweli amekosea avuliwe vyeo vyake katika chama na afukuzwe kabisa, ni zaidi ya miaka 5 tunasikia kasheshe za Zitto na kwa nini achukuliwi hatua?, kwa uelewa wangu kuna sababu mbili moja-hizi kashafa za zitto ni za UWONGO kuna watu ndani ya chama wanataka kumfanya jamaa aonekane mbaya na wananchi wasimwamini kabisa (smart move) na pili labda CDM inamuogopa bwana Zitto wanajua wakimuondoa Zitto litakuwa pigo kubwa kwao kama chama (Stupid Move). nI LAZIMA MAAMUZI MAGUMU YACHUKULIWA SASA HIVI.
 
Nadhani kwa ugomvi huu kumalizika naona CHADEMA IMARA inakuja.Uzuri wa demokrasia ni kuongea hata kama una utumbo hasira ikiisha kila mtu ataona ubaya na uzuri wa jambo alilolifanya.Hakuna sababu ya kuwafukuza uanachama bali kuna sababu ya kuielimisha jamii ya vijana kuwa upinzani siyo uadui na kama malengo ni kuleta mwaendeleo basi tupigane kwa maneno yatakayoleta ufumbuzi wa matatizo yetu kama watanzania.
 
THIS SCANDALS WILL SLOW DOWN OUR SPEED AND POWER TO OVERTHROW CCM, AND THEY MIGHT WIN 2015 ELECTIONS
​

GUY'z, am very disappointed by this fellow Tanzanians who always make 1 step ahead then makes 3 backwards, I wasn't born politician but my principles guides me to what I need from politicians, Just to share my small Idea to fellow Tanzanians who also might be like me or not.., If you like it take it and we will make Tanzania a better place, otherwise, we wont help in anything by just sitting back and claim that politics is a dirty game.

Since Nape brought this issue up of hon. Dr Slaa owning CCM card,I've been trying to add my few minutes to my politics break at least to figure out the thinking capacity of Tanzania's. And also I have managed to go through this thread in jamii forums that mentions how some groups within and out of CHADEMA might be involved and how some of the BAVICHA leaders in district level may be playing a great part to make sure they succeed in there plan of overthrowing DR. from his position.
Its o.k, but FEW LINE NEXT, POINTS TO A KIND OF DECISION WE TANZANIA'S SHOULD HAVE NOW.

*************************************************************************************
CCM has leaded has for so long enough(HAVE MENTIONED THIS WITHOUT BLINKING OF EYES), lets make changes by putting another person from a different party in 2015 election. Nothing new in CCM can be implemented to save TANZANIA. We are tired of repeating issues just because of poor governance. Let me just give a simple example from the country that we are North Eastern bordered to. Take a look how fast the economy of KENYA is growing, check what is their dream in 2030. And this speed of economy growth in Kenya has been facilitated by the political situation in the country, Look the changes they have made in politics, look how they play politics, due to this changes the leaders are working hard to provide good to there citizen that they may maintain there positions. For us we will remain making noise under stagnant thinking and pointing fingers to one another.
Fine you may say am wrong, then tell me why KENYAN economy is higher and growing faster than OURS?

TIME HAS COME , LETS MAKE CHANGES...... lets don't care who from a strong opposition party (CHADEMA) may be the president, Lets focus on overthrowing CCM from that position, lets try with another party there and If also they fail we keep on changing, this is the meaning of a MULTIPARTY country,the presidential seat wasn't made for one party forever. LETS KEEP ON CHANGING, and if possible, every after 5 years, we have a party change in the seat,but keeping on with this scandals will lower our power to overthrow CCM and they will take seat again in 2015.

This is my view in my political break,
Well umesema mengi kuhusu disadvantage za kuendelea kuwa na chama kimoja na unatumia mfano wa Kenya katika ukuaji wa uchumi etc. Lakini hujasema popote kwamba tufanyeje kuweza kufikia huko kwenye kubadilisha uongozi. Ukizingatia kwamba hao wapinzani ndiyo wapo kwenye minyukano.
 
Back
Top Bottom