SOURCE:
VIJANA WANAOMHUJUMU DR. SLAA HAwa HAPA
VIJANA WANAOTUMIWA KUMUHUJUMU DR. SLAA.
Nimesikitishwa sana na vijana wenzangu kutumika kisiasa kiasi cha kuudhalilisha utu wao. Kijana aiitwaye EDO MWAMA LALA, aliyekuwa katibu wa BAVICHA mkoa wa Mbeya na Adam CHEGULANI (diwani wa jiji la mwanza aliyenyanganywa kadi),wote hawa walifukuzwa Chadema kwa kutokuwa waadilifu. Wapo kwenye kibarua haramu cha kuhakikisha wanawashawishi vijana (hasa BAVICHA)kutoa matamko ya kumhujumu Dr. Slaa kisiasa kupitia vyombo vya habari.
Na wameanza mpango wao na kwa kiasi kikubwa wameanza kufanikiwa, kwani wamefanikiwa kumshawishi katibu wa BAVICHA mkoa wa MWANZA, ndugu SALVATORY SHUKURU MAGAFU kutoa tamko kwenye vyombo vya habari kuomba chama kimfukuze Dr. Slaa chamani. Pia leo hii tayari wanaye kijana mwingine maarufu wa chadema, atakae toa tamko muda wowote kuanzia sasa, kijana huyu wamemlipia hoteli moja maarufu iliyopo hapa jijini na kumpa fedha za kutosha ili atoe tamko kali la kumlaani Dr. Slaa.
Wengine ni: Usiwasahahu Juliana Shonza, Grayson Nyakarungu, Habib Mchange, Ben Saanane
tunawafahamu wote na mtu wanayemtumikia ndani ya Chadema
acha hao kina Nape!!
Kwasbabu lengo sio kulumbana wenyewe kwa wenyewe, wakae tu wakifahamu tunawafahamu na muda ukifika kuhangaika nao tutahangaika nao!!!!@ Alex by SeriaMtoto WikiLiks Tumainiel
Wenye nia ya dhati watabaki
wenye nia ovu watajionesha hadharani na wataungwa mkono na waovu wengine!!
Kwa huu mpango (walioupa jina la MWISHO WA SLAA) ulivyo watajitokeza vijana wengi sana watakaotoa matamko kumlaani Dr. Slaa kwa kutumia mwavuli wa BAVICHA imesema. Kwa akili zao zilivyofupi kama maisha ya funza wanadai wanadhamiria kumuua kabisa Dr. Slaa kisiasa. Na vijana wengi wamekuwa wakishawishika na upumbavu huu wa EDO na ADAM kwasababu ya fedha nyingi wanazopewa baada ya kukamilisha kazi hiyo.
Mpango huu unaofanywa na EDO MWAMALALA na CHAGULANI nyuma yake unafadhiliwa na BERNARD MEMBE, MWIGULU NCHEMBA, NAPE NNAUYE, kwa taarifa nilizo nazo na za kuaminika vijana hawa wanalipwa fedha nyingi sana na viongozi hao waandamizi wa CCM na SERIKALI ambao wamekosa sera na kuamua kuingia kwenye siasa za taarabu.
Kwa Binafsi yangu napenda nitoa tamko rasmi la kulaani kwa nguvu zote vijana wote wa BAVICHA wanaoendekeza njaa mbele na kuweka masilahi ya chama kando kuacha mara moja mchezo huu mchafu. Waache kuwa na akili za Samaki na hatimaye wajitegemee kisiasa. Na niwaombe viongozi hawa wa CCM waache kutumia tatizo la umasikini wa vijana hawa kuwarubuni na kuwatumia wenzao kama mipira ya mapenzi.
Ili kuepuka siasa hizi zisizo na tija kwa jamii niwaombe viongozi wenzangu wa BAVICHA kuachana na kujibizana na hawa wapumbavu, kwani ukijibizana na mpumbavu na wewe pia utakuwa mpumbavu, dhumuni lao tutumie muda mwingi kujibizana nao na tupuuze kujadiliana mambo ya msingi kwa mustakabali wa TAIFA.
CHADEMA tutaendelea kuwa na nguvu na kamwe hatuwezi kupunguzwa nguvu na siasa laini kama hizi. Kinachoshangaza ni kuona anayefadhili ushenzi huu ana ndoto za kuwania Uraisi katika nchi yetu, kweli kwa siasa laini hivi uraisi atauweza?
Imekuwa ni kama tabia yake ya kuwatumia vijana kutimiza malengo yake, kwani ni wazi katika mkutano mkuu wa CCM uliofanyika mkoani Dodoma alituhumiwa na wajumbe wenzie kutumia vijana kusambaza vipeperushii vilivyokuwa vikiwaomba wajumbe wa mkutano huo kumkataa Mwenyekiti wao kwa kisingizio cha kumpunguzia majukumu.
Sasa kashindwa huko anakuja kuingilia siasa za CHADEMA kwa kuwatumia vijana wetu wasiokuwa waadilifu; nimwambie kwa upendo tu kwamba CHADEMA TUKO IMARA KAMA CHUMA.
Na. Alex Nicholaus Thomas MUSHI,
Mjumbe wa Baraza kuu la CHDEMA-Taifa,
Mjumbe wa kamati tendaji BAVICHA-Taifa.
UONGOZI WA CHADEMA MAKAO MAKUU IFANYE UCHUNGUZI WA KINA NA KUCHUKUA HATUA KALI NA MWAFAKA JUU YA WANAOTAJWA HAPO JUU INAONEKANA HAO HAWATUMIWI NA CCM TU INAONEKANA WENYE UCHU WA MADARAKA NDANI YA CHADEMA WANAOTAKA KUGOMBEA URAIS 2015 WANATAKA KUGAWA CHAMA KTK VIPANDE KWA KUMDHOOFISHA DR. SLAA KWANI WENYEWE WANAMUOGOPA, KUWA NDIYE MGOMBEA BORA WA CHADEMA WAKIHOFIA KUWA CHAMA CHAKE KITAMSIMAMISHA TENA 2015 KM ILIVYOKUWA 2010 NA AKATULETEA USHINDI MNONO WANACHADEMA.
BAVICHA PIA IWE MACHO MPAKA SASA SIJASIKIA MATAMKO ILIYOTOLEWA NA BAVICHA KUPINGA NA KUDHIBITI UTOMVU HUU WA NIDHAMU UNAOFANYWA NA VIJANA TENA WENGINE WAJUMBE NA VIONGOZI WA BAVICHA WANAOTUMIWA KM CONDOMS NA WAGOMBEA WA URAIS 2015 KUTOKA KTK VYAMA MBALIMBALI WAKIPEWA HELA CHAFU!!