Usia wangu kwa Zitto na washirika wake

Usia wangu kwa Zitto na washirika wake

Huko kukosekana kwa ushahidi ndio kunakopaswa kumsukuma Zitto kuresign, Zaidi ni kwa faida yake Binafsi, sababu baada ya haya yote kumwagwa wazi namna hii atakuwa ni mtu wa ajabu sana kama ataendelea kutegemea kwamba viongozi wenzake watakuwa na imani nae tena achilia mbali wanachama na wapenzi wa CHADEMA.
Nakuunga mkono mkuu. Tusubiri tuone Zitto atachukua uamuzi gani juu ya hili.
 
I find hard to trust Zitto

Lugha kama huijui lazima uandike? si uwaulize wanaoijuwa kwanza. Jivunie lugha yako ya Taifa, au Kiswahili kinakupiga chenga pia? bora ungeandika hata kichagga.
 
Huko kwenye vikao wataongea kitu gani kipya? Hakuna walichobakiza, yote wameshayaongea humu. Iliyobaki ni wao kukutana kwa mara nyingine, waende kwa sangoma wao wakavunje Kamati. Bila kuvunja kamati wataendelea kushambuliana mitandaoni!

Hebu Kidogo nigusie nini uchawi ili kila mtu ajue ni kitu gani Mr. Zito Zuberi Kabwe anachojivunia na kutishia watu. Nini maana ya uchawi? Ni kitendo cha kujikurubisha na shetani na kwa msaada wake (shetani), Au uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli. Ama "uchawi ni kuidhirisha batili katika sura ya haki". Kwa lugha nyepesi, ni kila jambo lililofichika sababu zake, linalotokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake mna hadaa. Kuna baadhi ya mambo ambayo mchawi anafanya: 1.mchawi huvaa msaafu miguuni na kuingia nao chooni. 2. Anaandika baadhi ya aya za qurani kwa damu ya hedhi. 3.wanaandika aya za Quran kwenye nyayo za miguu. 4.kuandika suratul Fatiha kinyumenyume. 5. Wanasali bila ya udhu. 6.kuchinja mnyama bila ya kulitaja jina la M/Mungu kisha amtupe mnyama huyo mahali maalum. Hayo machache yanatosha kwa leo.
 
KWA TAARIFA HIZI ZA KUNDI LA MASALIA KUPITIA KWA MWANACHAMA HAI WA CHADEMA BEN SAANANE KWA USHAHIDI HUU WAAWALI WA KIMAZINGIRA WAO KAMA VIONGOZI WA CHADEMA WANAOTAKIWA KULINDA NA KUISIMAMIA KATIBA YA CHAMA MPAKA SASA WAKWISHA KIUKA BAADHI YA VIPENGELE VYA KATIBA KAMA TUTAKAVYOONA HAPA CHINI.

Sura ya Kumi ya Katiba.
10:0 Maadili ya Viongozi,Sifa Mahususi za Viongozi na Maadili ya Wanachama

10:1 Maadili ya Viongozi.

(i)
Kila kiongozi anatakiwa kuwa na kuwa na tabia amabayo ni mfano wa kuigwa na wanachama na jamii kwa ujumla.

(ii)
Kila kiongozi anatakiwa kulinda siri zote za Chama

(iii) Kiongozi yeyote asijihusishe na vikundi vyenye msingi ya ukabila,udini,au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya chama au miongoni mwa jamii kisiasa au kijamii

(ix) Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi au vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya Uongozi wa Chama au Wanachama wake.

(
xi) Kiongozi anatakiwa kutii na kutimiza maagizo anayopewa ana viongozi wa ngazi ya juu au vikao halali na kama hakubaliani na maagizo hayo aeleze hivyo kwa kupitia taratibu na ngazi zilizowekwa kwenye Kanuni.

(xii) Itakuwa marufuku kwa Kiongozi wa CHADEMA kukashifu Chama,Kiongozi au Mwanachama yeyote wa Chama au Vyama vingine,au Viongozi wa Kiserikali.
Ni muhimu viongozi wa CHADEMA waelewe tofauti ya kashfa na ukosoaji wa kisiasa
.

SEHEMU A:

KANUNI ZA KUSIMAMIA SHUGHULI,MWENENDO NA MAADILI YA WABUNGE WA CHADEMA-KATIBA-2006. 2.0.

d.Mbunge anawajibika kutumia hadhi,uwezo,wadhifa na nafasi aliyonayo kama Mbunge kukijenga Chama ndani na nje ya Bunge e.Mbunge anatakiwa kuwa na tabia ambayo ni mfano wa kuigwa katika jamii.

3.0 NIDHAMU
Bila kuathiri maadili na taratibu za kinidhamu zilizopo katika Katiba ya Chama,makosa yafuatayo yatahesabiwa kuwa ni makosa ya kinidhamu na yatastahili adhabu:-

3.0 f. Mbunge kuchochea mgawanyiko ndani ya Chama.

Mbunge atakayefanya makosa haya atakuwa ameonyesha mwenendo usioendana na itikadi, fafsafa,madhumuni,kanuni na maadili ya Chama.

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama Ibara ya 5:4:3 Mbunge huyu atastahili adhabu.

Ibara ya 5:4 KUKOMA KWA UANACHAMA

5:4:3
Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama,kwa mujibu wa katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo usioendena na Itikadi,falsafa,madhumuni ,kanuni,maadili, na sera za Chama.
Mwanachama atakuwa na haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na adhabu hiyo.

5:4:4 Bila kuathiri kifungu cha 5:4:3 cha Katiba ,Kamati Kuu inaweza kumwachisha ama Kumfukuza mwanachama yeyote kwa utaratibu utakaopangwa na Kanuni za Chama.

Baada ya kuona misingi ya katiba na maeneo mengine ya Kanuni inayosimamia Chama kwa kadri mgogoro na taarifa hizi za kundi la MP-7/Masalia ndani ya Chadema na Ushahidi huu wa kimazingira dhidi ya Mheshimiwa Zitto Z. kabwe(Mbunge) na Juliana Shonza Makamu Mwenyekiti-BAVICHA. Kuna ulazima sasa Chama kifanye Uchunguzi ilikubaini ukweli wa jambo hili na kulishughulikia kwa haraka ili kujengea Chama na kuondoa wasi wa wanachama. Ukimya huu wa mara kwa mara wa Makao Makuu ya Chama dhidi ya uvunjifu wa Katiba kwa baadhi ya Viongozi unaweza kuibomoa Chama kama hatua haitachukuliwa dhidi ya wahusiaka.

Niimani yangu kuwa ndani ya CHADEMA kupitia Wanasheria lazima kuna watu wamekwisha nga'amua uvunjifu huu.Nichukue mfano mzuri wa Mhe.Lissu. Naomba kumkumbusha kuwa kazi nzuri huanzia nyumba,kama tunalalamika Raisi anavunja Katiba huku tunaacha wenzetu wakiichezea Katiba yetu wenyewe hatutapata uhalali mbele ya jamii kwa kushindwa kwa Chadema kusimamia taasisi ndogo kama Chama.
 
Partly nakubaliana na wewe, lakini hilo la kujiuzuru nafikiri lifikie iwapo tu hawatakubali kuomba msamaha kwa chama na wanachama wa CHADEMA. Kama wakitubu sioni sababu maana tatizo litakuwa limeisha, lakini kama wataendelea na jeuri walizonazo sasa kama ile ya Juliana, basi hatua zaidi zinaweza kuchukuliwa dhidi yao.
Lukolo, nadhani unanielewa vibaya.
Sijasema AFUKUZWE uanachama, nimesema aachie nafasi za uongozi katika chama.

Kwanini nashauri hivyo!
1. Kwanza, Zitto amehusishwa na kashfa chafu ya kudhuru chama.
Amethibitisha kuwa pamoja na mambo mengine anawafahamu wanachama wa M7. Hakuna shaka alijua mpango huo.

Ni ngumu kwa kiongozi yoyote ndani ya chama kukaa na kumuani Zitto katika masuala nyeti na hata ya kisiasa.
Tuhuma tu zimemuondelea uanifu kwa wenzake.
Pengine ndio maana hata katika mkakati wa kuimarisha chama Zitto anaonekana kwenda ''Solo''.

Pili, tuhuma hizi za kukihujumu chama ni nzito sana na hivyo anapaswa akae pembeni apishe uchunguzi halali utakaomuosha au kumhumu. Kwasasa anabaki kuwa mtuhumiwa namba moja katika genge linalojidhihiri kuwa linataka kuua chama.

Kwa vile ni mtuhumiwa namba moja ni ukiukwaji wa sheria kama kuna hatua zitachukuliwa kwa watuhumiwa 2, 3 n.k. ambao si viongozi. Kwahiyo Zitto anatakiwa avue vyeo vyake ili asimame mbele ya sheria sawa na watuhumiwa wengine. Vinginevyo nafasi yake itamtetea hata kabla ya mashitaka.

Kama hakutakuwa na fairness basi tutarudi kule kule kwa Juliana Shonza. Huyu aliachwa abalehe(-Kitila) huku madiwani vijana wakipitiwa na mapanga kama si mashoka. Tulisema double standard zitawafunga mikono CDM.
Sasa unaona Juliana pamoja na kukiri kuwa hana kazi pale CDM, bado wameendelea kumshikilia kama makamu mwenyekiti.

Huyu naye katika vurugu hizi anapaswa kuachia ngazi
1. Amekuwa chanzo cha mitafaruku ndani ya chama
2. Anaweza kutumiwa hata kudhuru wanadamu kwasababu utayari wa kutumwa anao
3. Amekiri hana kazi
4. Amezusha uongo kwasababu kwa umri na uchanga wa kisiasa hana sababu ya kupigwa vita zaidi ya majungu.
5. Ameonekana kulindwa kwa masilahi nje na ya kisiasa.
Hiki ni chama cha kisiasa siyo mkusanyiko wa wanamuziki, wachezaji wa filam au wafanyabiashara halali na haramu.

Kama CDM wanataka kuanza na healing process, ni lazima waanzie hapa kwa watuhumiwa wakuu wawili.
Kuwapunzisha kazi si kuwafukuza ubunge au uanachama, ni kutoa nafasi kwa chama kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.

Nasisitiza
Mhe Zitto Zuberi Kabwe na Juliana Shanzo
Endapo mnapenda maendeleo na kukipenda chama chenu, basi mnapaswa kujiuzulu nadhifa zenu haraka ili kupisha mkondo wa sheria ufanye kazi yake.

Mtabaki kuwa watuhumiwa hadi itakapothibitika vingenevyo.
Ni utuhumiwa huo ndio unawaondelea maadili, haki, uhalali na uaminifu ndani ya chama chenu.
Kisadieni chama au la Chama kifanye maamuzi ya kukisaidia chenyewe
 
Mbona long time alishavunja sana hizo sheria,sasa akachukue uchawi na matunguli akawe mganga na si Rais kupitia CDM.
 
Ni kukaa kimya na kuwa maliza taratibu, hatua zikichukuliwa sasa mabwana wao CCM watasambaratisha chama chetu
 
hao vijana wote ndani ya CDM hawatakiwi,kama uliweza kutaka kuanzisha kundi ndani ya chama hata kama baadae ulitaka kulivunja bado haionyesha kuwa huwezi kufanya hivyo mbeleni,kama ningekuwa ni kiongozi ndani ya CDM hakuna ambaye angesalimika,maana vijana hao wote walikuwa na malengo ya kukisambaratisha chama na ndio maana ktk nchi yeyote ile usalama wa taifa ukihasi na eti uka amuwa kuacha uasi huo usitegemee kuwa utaachwa hata kama uliomba radhi,kwani tabia haina mbadala wake.na tabia husomei ni kitu kipo cha kuzaliwa nacho.
mimi nikiwa ni kiongozi siwezi kukupa nafasi mtu ambaye ulikuwa na dhamira ya kuleta mgawanyo.
 
Mjadala huu napenda uwe chachu kuelekea kushikana mikono kwa hawa vijana ambao wamekua wakichafuana na kukichafua chama na viongozi kwa ujumla.

Napenda usaulishe vidondo vyote vilivyotokea wakiitwa meza moja moja wasiwe na chuki wala uhasama bahati mbaya sana leo sikumuona ben mahakamani ningemuona ningempa huu ushauri nakumbuka alikuja na bandiko la wasaliti wote wafukuzwe ndani ya chama nilimpinga kwa hoja kwamba nisingependa hawa vijana wafukuzwe bali waitwe wawekwe chini wamalizwe.

Sasa ukaja huu utoto wamechafuana wewe lakini wamekipa chama damage kubwa tukubali tukatane sio leo wala kesho kutwa damage hii itaondoka niseme wazi tusiitane wasaliti ndani ya chama kama kweli hawa vijana wana nia ya kuendelea waombe msamaha wasamehewe wachukuliwe kama vijana ambao wengi hawajafika 30 wako kwenye mihemuko ya ujana.

Wengi hatujamjua vizuri Zitto:
Niweke wazi nishafanya mijadala ya wazi kwenye twitter na mh zitto mingi ilikua ya kujenga nchi kuona wapi tunafika zaidi ya hapa tulipo sasa kumuita zitto msaliti bado tunakosea sana wana chadema kwanini leo ndo akisaliti chama wakati alikitumikia miaka yote hiyo ya mwanzo kabla hajawa mbunge bila kukisaliti.

Tuwe wakweli bila baadhi ya michango ya zitto chama kisingekuwa hapa kilipo hata siku chama kishika madaraka atakua ameplay part kubwa sana kuanzia kwenye operation sangara mbona alishiriki hakukua na maneno.Najiuliza kitu zitto ameulizwa kuhusu kushiriki M4C amesema amepangiwa kanda ya Singida muda wake haujafika kwenda hiyo kanda ukifika atakwenda ni zitto huyu aliyeenda Rombo kwenye uchaguzi wa udiwani ni Zito huyu aliyeenda Karatu ni zitto huyu huyu aliyeenda Tanga kwenye operation ya Katani.

Hoja za ben saanane kwa zitto kuwa ni msaliti kupita kikundi chao inavyoonyesha ben alikua na mawasiliano ya simu tu na zitto na hata kwenye msg zinaonyesha zitto angekuwa na msaidizi ya kuweza kuzijenga sera za chama Chauma kwenye gas na mafuta tunajua zitto hakufurahi kufukuzwa kwa kafulila na vijana wenzake tulipoteza seat 4 bungeni kufanya mamuzi ya haraka.

Tuache yote hayo yaliyopita si ndwele tugange yajao kujenga chama chetu kiwe na mfumo imara tuingie 2013 tukiwa tumemaliza tofauti zetu siamini zitto anaweza isaliti chadema na sitaamini bado ninamuona ni kijana imara kama ilivyo kwa dr slaa hata mwenyekiti wote mbowe.

Suala la zitto kutangaza kugombea uraisi:
Zitto kama mshamsoma ni kiongozi ambaye akishapanga kitu hata kama kina negative effect kwake huwa haangalii nyuma atakwenda nacho ukishamuelewa kiongozi wa aina hii wala usipate nae shida jaribu kujenga hoja lazima atarudi.

Zitto ametangaza kuwa atagombea uraisi mwaka 2015 pia Shibuda naye alitangaza hivyo hivyo kuwa atagombea uraisi mwaka huo zitto kuiongezea hoja yake mashiko akasema yoyote atakayepitishwa na chama yeye atamsupport hatagombea ubunge tena atarudi kufundisha chuoni watu wakapayuka anaharibu chama je angekaa kimya bila kutangaza angezunguka nchini kuweka mamuliki kujipigia kampeni ili apite mwaka 2015 tungesemaje.

Zitto ameonyesha nia ya kuutaka uraisi kwa kipindi hiki wana jf na watanzania wote tumpime uadilifu wake na utendaji kazi wake je atafaa kuwa raisi wetu na sio kumvunja moyo sijui mamluki anatumia na wana ccm kisa yuko rafiki na makamba na jk unapokua mwanasiasa unayetafuta kuingia ikulu lazima ujichanganye na watu wote wale watanzania kwa sababu wewe utakuja kuwa kiongozi watu wanaleta picha alizopiga na jk sio ishu picha kitu cha kawaida sana.

Kipindi hiki chadema kingemjenga Zitto:
1.Wazee wangemuita na kupunguza hasira kumpa ushauri usingeona jibu la kutishia lile la majuzi

2:wazee wangemuambia sasa ni wakati wa wewe kuwa na mwenza wako hatuwezi kuwa na kiongozi muhuni tu ikulu

3:wazee wangemjenga na kumsimamisha imara

4:muda huu tungetumia kuchunguza mali za zitto je ana mali haramu yoyote muda huo tungemjenga zitto zaidi kwenye media na yoyote yule atakaye tangaza anautaka uraisi

5:muda huu zitto angezunguka na chama na M4C nchi nzima hapa namlaumu zitto hazunguki aanze sasa kuzunguka

Hakuna kuita mtu msaliti chama si cha demokrasia kama zitto kweli anakubalika ndani ya chama ungeitishwa uchaguzi huru ashindanie nafasi na watakao jitokeza na mshindi mmoja apatikane apeperushe bendera ya chama.

Nakuja kwa MaMuya na BEN Saanane:
Nyie ni vijana kwanini haya malalamiko yenu mlishindwa kupeleka kwa chama mmesababisha mmekivua chama nguo hapa na kukitia aidu hakika hii itatutafuna je mmekubali mlipanga mbinu chafu hapo mwanzo?? Na je mshakubali makosa na kuomba msamaha chama kiendelee mbele zaidi kusahahu yaliyopita tujenge chama imara zaidi.

Swali dogo kwa ben hivi ungekua ndo mwenyekiti wa Bavicha sasa ungeunda kile kikundi chenu?

Kwanini haya hukuyapeleka kwenye chama mapema??

Kwanini sasa ndo mmeyatoa tena hadharani je ni kweli ben unakitakia mema chama cha chadema kuanikana hadharani??

Kwanini msingekuatana na viongozi mkayamaliza kuliko kutuletea sisi na dunia nzima sasa mnaitana wasaliti??

Habib Mchange:
Wewe ni kijana imara sana uligombea ubunge mwaka 2010 ukiwa mdogo sana je ungekua mwenyekiti wa bavicha ungekubali kuunda kikundi cha uasi??

Lakini kama unakipenda chadema kweli kwanini hukupeleka malalamiko yako ndani ya chama mapema??

Kama kweli zitto alitaka kuuliwa kwanini hakupeleka kwa polisi na kwa chama??

Je uko tayari kuomba msamaha kuanzia kwa kina john mrema,dr slaa na viongozi wote mliwachafua kwenye social network??

Je uko tayari bila kinyongo kusamehana na wenzako na mjenge chama bila kuleta vinyongo vya ajabu mbeleni??

Juliana Shonza:
Wewe ni kijana mwanamke mwenye uwezo tu mzuri msomi naweza kusema kiongozi wa chama makamo mwenyekiti,je ni kweli wewe kujiunga na hiki kikundi ni uchungu heche kulipwa 700000 na wewe haulipwi kitu.

Je uko tayari kuomba msamaha kwa viongozi wote mlivyo wachafua na tugange yajayo?

Mimi wala simlamu dr slaa kukuweka pembeni aliona inafaa kubali kosa kijana tujenge chama

Huyu dada tatizo hapa ni heche kulipwa hela tunarudi yale yale siasa kuwa chanzo cha ajira vijana wetu hawa lazima wapate matatizo.

Mtela mwamapamba:
Wewe kijana hapana tena ukamtukana kabisa hapa kiongozi wako je una chuki naye ipi?

Je uko tayari kusamehe yote yaliyopita na mjenge chama kwa nguvu moja?

Je ungekua mwenyekiti wa Bavicha ungejiunga na kikundi chenu cha uasi?

je uko tayari kuomba viongozi wote ulioshawahi kuwatukana na tujenge chama sasa?

Pili fanyia kazi kwenye uandishi huwezi kuandika kitu ukiwa na hasira.

Mwisho:
Matatizo ya hawa vijana wote kwanza walifanya siasa kuwa ajira sasa baada ya kuingia ndani ya siasa na kukuta hamna pesa na wachache ndo wanapewa pesa ikabidi waanzishe movement za kupiga pesa hawa wote wasitudanganye lengo lilikuwa ni pesa tu.

Vijana wengi wanaingia kwenye mapambano haya wakijua watapata kitu sasa wanagombea nafasi fulani wakikosa wanakua hawana kingine cha kufanya kinabaki kupiga majungu mtaani na kutafuta pa kutokea kisiasa.

Vijana hawa wawekwe chini wote kuanzia kina ben,mtela,juliana,mchange wapewe onyo kali na watubu maovu yao yote chama kianze upya sitafurahi nasikia kuna kina kafulila wengine bungeni wameingia kupitia chauma mambo ambayo tulishindwa maliza ndani ya chama.

Je chama kifanye nini haya mambo yasirudie:
1.Chama kiwaite bavicha wabuni miradi ya kukiingiza chama pesa nilitoa wazo la maduka ya bidhaa za chadema makao makuu,arusha,dodoma,kilimanjaro,mwanza haya maduka unaweza kuwa mradi wa bavicha wausimamie wajue chama kinauza combat ngapi kwa mwezi na kinapata sh ngapi

2.Miradi mingine kama radio nk

Ukishakua na hii miradi ni rahisi vijana wanakosa nafasi kwenye chama kuwaingiza na kuwapa ajira fupi huku wakijipanga zaidi.

NARUDIA TENA HAKUNA MAPAMBANO HUKU UKIWA NA NJAA utanunulika tu lazima.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo naomba moderator wasiunganishe uzi huu tuwasikie ben na wenzake wanasamehana hapa hatuhitaji majibishano tena tumekesha siku zaidi ya 3 hakuna cha suluhisho.ni wakati nyie vijana kuamuana kama mtakiokoa chama chenu mpatane.

Na tusiitane wasaliti tena atakayekuja kuchangia humu wala mamuluki tuwe wastaarabu tujenge chama.

Sitamaliza bila kutoa pongezi kwa makamanda wote tulikuwa mahakamani leo heche,lissu,mbowe,lema,myika,kiwelo na wengine wengi mshikamano daima.

Hakika tutoke hapa tukale sikukuu za kumaliza mwaka tukiwa wamoja mwakani turudi na M4C ya nguvu ambapo kina shonza na mchange na ben watasimama pamoja wakiendeza sera za chama kuwaamsha watu nyumba hadi nyumba.

Tusiposamehana sasa tuna muda mchache sana kabla ya uchaguzi mkuu 2015 siamini katika kufukuza kijana siamini kabisa waombe msamaha kuteleza sio kuanguka turudi tujenge chama.

Mapambano yanaendelea

Fred Kavishe.

yoyote aliye CCM asingependa masalia yafukuzwa najua unajua kwanini
 
Lukolo, nadhani unanielewa vibaya.
Sijasema AFUKUZWE uanachama, nimesema aachie nafasi za uongozi katika chama.

Kwanini nashauri hivyo!
1. Kwanza, Zitto amehusishwa na kashfa chafu ya kudhuru chama.
Amethibitisha kuwa pamoja na mambo mengine anawafahamu wanachama wa M7. Hakuna shaka alijua mpango huo.

Ni ngumu kwa kiongozi yoyote ndani ya chama kukaa na kumuani Zitto katika masuala nyeti na hata ya kisiasa.
Tuhuma tu zimemuondelea uanifu kwa wenzake.
Pengine ndio maana hata katika mkakati wa kuimarisha chama Zitto anaonekana kwenda ''Solo''.

Pili, tuhuma hizi za kukihujumu chama ni nzito sana na hivyo anapaswa akae pembeni apishe uchunguzi halali utakaomuosha au kumhumu. Kwasasa anabaki kuwa mtuhumiwa namba moja katika genge linalojidhihiri kuwa linataka kuua chama.

Kwa vile ni mtuhumiwa namba moja ni ukiukwaji wa sheria kama kuna hatua zitachukuliwa kwa watuhumiwa 2, 3 n.k. ambao si viongozi. Kwahiyo Zitto anatakiwa avue vyeo vyake ili asimame mbele ya sheria sawa na watuhumiwa wengine. Vinginevyo nafasi yake itamtetea hata kabla ya mashitaka.

Kama hakutakuwa na fairness basi tutarudi kule kule kwa Juliana Shonza. Huyu aliachwa abalehe(-Kitila) huku madiwani vijana wakipitiwa na mapanga kama si mashoka. Tulisema double standard zitawafunga mikono CDM.
Sasa unaona Juliana pamoja na kukiri kuwa hana kazi pale CDM, bado wameendelea kumshikilia kama makamu mwenyekiti.

Huyu naye katika vurugu hizi anapaswa kuachia ngazi
1. Amekuwa chanzo cha mitafaruku ndani ya chama
2. Anaweza kutumiwa hata kudhuru wanadamu kwasababu utayari wa kutumwa anao
3. Amekiri hana kazi
4. Amezusha uongo kwasababu kwa umri na uchanga wa kisiasa hana sababu ya kupigwa vita zaidi ya majungu.
5. Ameonekana kulindwa kwa masilahi nje na ya kisiasa.
Hiki ni chama cha kisiasa siyo mkusanyiko wa wanamuziki, wachezaji wa filam au wafanyabiashara halali na haramu.

Kama CDM wanataka kuanza na healing process, ni lazima waanzie hapa kwa watuhumiwa wakuu wawili.
Kuwapunzisha kazi si kuwafukuza ubunge au uanachama, ni kutoa nafasi kwa chama kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.

Nasisitiza
Mhe Zitto Zuberi Kabwe na Juliana Shanzo
Endapo mnapenda maendeleo na kukipenda chama chenu, basi mnapaswa kujiuzulu nadhifa zenu haraka ili kupisha mkondo wa sheria ufanye kazi yake.

Mtabaki kuwa watuhumiwa hadi itakapothibitika vingenevyo.
Ni utuhumiwa huo ndio unawaondelea maadili, haki, uhalali na uaminifu ndani ya chama chenu.
Kisadieni chama au la Chama kifanye maamuzi ya kukisaidia chenyewe
Well said mkuu. Napenda nikubali kwamba kwenye post ya awali sikukupata vema. Sasa nimekuelewa vema. Nauunga mkono hoja, wajiuzulu kupisha uchunguzi. Ikithibitika vinginevyo wanaweza kurudi kwenye nafasi zao.
CC Zitto, Juliana Shonza
 
Last edited by a moderator:
hao vijana wote ndani ya CDM hawatakiwi,kama uliweza kutaka kuanzisha kundi ndani ya chama hata kama baadae ulitaka kulivunja bado haionyesha kuwa huwezi kufanya hivyo mbeleni,kama ningekuwa ni kiongozi ndani ya CDM hakuna ambaye angesalimika,maana vijana hao wote walikuwa na malengo ya kukisambaratisha chama na ndio maana ktk nchi yeyote ile usalama wa taifa ukihasi na eti uka amuwa kuacha uasi huo usitegemee kuwa utaachwa hata kama uliomba radhi,kwani tabia haina mbadala wake.na tabia husomei ni kitu kipo cha kuzaliwa nacho.
mimi nikiwa ni kiongozi siwezi kukupa nafasi mtu ambaye ulikuwa na dhamira ya kuleta mgawanyo.
Sijui katiba ya chadema inasemaje kuhusu hili, lakini badala ya kuwafukuza tungeweza kuwapiga stop kugombea nafasi yoyote ndani ya chama kwa muda fulani. Lakini nimeona Ben saanane yupo tayari kufukuzwa, na amesema amejiandaa kwa hilo. Tusubiri maamuzi ya chama, kama kweli wataamua kulichukua hili serious. Lakini wakiamua kuliignore kama wanavyofanya kwenye mengine basi tusitegemee mabadiliko makubwa sana.
 
Ni kukaa kimya na kuwa maliza taratibu, hatua zikichukuliwa sasa mabwana wao CCM watasambaratisha chama chetu
Hili nalo ni neno. Lakini kuna hoja ya Nguruvi3 anayependekeza watuhumiwa wote wajiuzuru nafasi yao. Kukaa kimya hakutamaliza tatizo kwa kuwa bifu litaendelea. Kukaa kimya kunaweza kupelekea watu kuuana kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Well said mkuu. Napenda nikubali kwamba kwenye post ya awali sikukupata vema. Sasa nimekuelewa vema. Nauunga mkono hoja, wajiuzulu kupisha uchunguzi. Ikithibitika vinginevyo wanaweza kurudi kwenye nafasi zao.
CC Zitto, Juliana Shonza
kwa nini iwe hao uliowataja,je haowengine hawakuwa na jambo ktk hiyo mikakati? hatakama si viongozi hata kusimamishwa uanachama pia yatosha,
 
Hebu Kidogo nigusie nini uchawi ili kila mtu ajue ni kitu gani Mr. Zito Zuberi Kabwe anachojivunia na kutishia watu. Nini maana ya uchawi? Ni kitendo cha kujikurubisha na shetani na kwa msaada wake (shetani), Au uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli. Ama "uchawi ni kuidhirisha batili katika sura ya haki". Kwa lugha nyepesi, ni kila jambo lililofichika sababu zake, linalotokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake mna hadaa. Kuna baadhi ya mambo ambayo mchawi anafanya: 1.mchawi huvaa msaafu miguuni na kuingia nao chooni. 2. Anaandika baadhi ya aya za qurani kwa damu ya hedhi. 3.wanaandika aya za Quran kwenye nyayo za miguu. 4.kuandika suratul Fatiha kinyumenyume. 5. Wanasali bila ya udhu. 6.kuchinja mnyama bila ya kulitaja jina la M/Mungu kisha amtupe mnyama huyo mahali maalum. Hayo machache yanatosha kwa leo.
Mkuu unatupiga shule ya kuwa wakali wa gizani au? nimevunjika mbavu---- una maana ZZK ni mkali? Ninamkumbuka jama mmoja Mudhihir mudhihir bungeni alianzisha hoja ya kumtoa ZZK mjengoni kilichompata ule mkono alionyosha kuomba kuongea ULIKATIKA!! Belief nyingine!!
 
kwa nini iwe hao uliowataja,je haowengine hawakuwa na jambo ktk hiyo mikakati? hatakama si viongozi hata kusimamishwa uanachama pia yatosha,
Nafikiri idea ni kwamba kwa viongozi wajiuzuru ili ufanyike uchunguzi huru usio na influence ya kiuongozi. Kusimamishwa uanachama nafikiri ni hatua ya juu sana ya kimaamuzi. Labda tusifike huko kabla ya kufanyika uchunguzi na kujiridhisha kwamba walikuwa na nia ya kukiua chama.
 
I am not interested in focusing to discussing people's issues when it comes to our politics, we have to change this illness if we want to progress in this modern world we have to change our entire political mentality to ISSUE BASED, RESULT BASED AND DEMOCRATIC ACCOUNTABILITY, we are totally going against it.....heading in the wrong side of history.....

Leo na kila siku tunaona watu wanazungumzia issue zisizo na msingi kabisa na maendeleo ya WATANZANIA.....yanayohusu watu flani flani ....mara eti Slaa ana kadi ya CCM, mara Nape ana Kadi ya CCJ, Mara Zitto hatakiwi kutangaza nia ya kugombea Urais utakuta eti kwa sababu ooooh ni mapema oooh anapenda madaraka ooooh blah blah, which is totally wrong we are incubating this wrong mentality and we are going to totoa the wrong kifaranga...... chuki, fikra dumavu, siasa uchwara..... why arent we talking for instance KIONGOZI GANI AMEKUA MTETEZI WA WATANZANIA? KIONGOZI GANI AMEKUA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERA ZENYE MASLAHI YA WATU? NANI AMEJITOA MUHANGA KINAGA UBAGA KUSIMAMIA MISINGI THABITI YA UONGOZI NA KULINDA MASLAHI YA WATANZANIA, KIONGOZI GANI ANAEONEKANA KUELEWA DYNAMICS OF REGIONAL AND INTERNATIONAL ECONOMIC, POLITICAL AND SOCIAL ISSUES KIASI KWAMBA ANAWEZA KUSAIDIA TANZANIA KUJIZATITI KATIKA DUNIA HII YA USHUNDANI....... I am not sorry to say that based on issue based politics and the democratic system that we all stand for I see ZITTO ZUBERI KABWE to be one of Tanzania's finest politicians. Besides he is fearless, ambitious and determined, and accountable..... we need this calliber in this times more than in anyother, we also need to encourage it... i dont see the other way arround

Yaani kila mtu siku hizi anajifanya Kingmaker, we have systems of democracy in our political systems, let them tell us who can vie for what position, be it at a party level or country.... If Zitto, Lowassa, Slaa, Sita or Mbowe wants to become president let the system tell us based on those credible criteria for the Greater Good for all Tanzanians..... tusichakachue mfumo... mfumo utatuchakachua....
 
mkuu mimi nazungumnzia kina sanane na wenzake,maana mmewataja zitto na huyo dada,je hao wengine hakuna cha kufanya?
 
mkuu mimi nazungumnzia kina sanane na wenzake,maana mmewataja zitto na huyo dada,je hao wengine hakuna cha kufanya?
Zitto na Juliana ni viongozi ndani ya CHADEMA, lakini hao akina saanane, mchange na kundi lake si viongozi wa chama kwa sasa, kulingana na uelewa wangu.
 
I am not interested in focusing to discussing people's issues when it comes to our politics, we have to change this illness if we want to progress in this modern world we have to change our entire political mentality to ISSUE BASED, RESULT BASED AND DEMOCRATIC ACCOUNTABILITY, we are totally going against it.....heading in the wrong side of history.....

Leo na kila siku tunaona watu wanazungumzia issue zisizo na msingi kabisa na maendeleo ya WATANZANIA.....yanayohusu watu flani flani ....mara eti Slaa ana kadi ya CCM, mara Nape ana Kadi ya CCJ, Mara Zitto hatakiwi kutangaza nia ya kugombea Urais utakuta eti kwa sababu ooooh ni mapema oooh anapenda madaraka ooooh blah blah, which is totally wrong we are incubating this wrong mentality and we are going to totoa the wrong kifaranga...... chuki, fikra dumavu, siasa uchwara..... why arent we talking for instance KIONGOZI GANI AMEKUA MTETEZI WA WATANZANIA? KIONGOZI GANI AMEKUA NA MCHANGO MKUBWA KWA SERA ZENYE MASLAHI YA WATU? NANI AMEJITOA MUHANGA KINAGA UBAGA KUSIMAMIA MISINGI THABITI YA UONGOZI NA KULINDA MASLAHI YA WATANZANIA, KIONGOZI GANI ANAEONEKANA KUELEWA DYNAMICS OF REGIONAL AND INTERNATIONAL ECONOMIC, POLITICAL AND SOCIAL ISSUES KIASI KWAMBA ANAWEZA KUSAIDIA TANZANIA KUJIZATITI KATIKA DUNIA HII YA USHUNDANI....... I am not sorry to say that based on issue based politics and the democratic system that we all stand for I see ZITTO ZUBERI KABWE to be one of Tanzania's finest politicians. Besides he is fearless, ambitious and determined, and accountable..... we need this calliber in this times more than in anyother, we also need to encourage it... i dont see the other way arround

Yaani kila mtu siku hizi anajifanya Kingmaker, we have systems of democracy in our political systems, let them tell us who can vie for what position, be it at a party level or country.... If Zitto, Lowassa, Slaa, Sita or Mbowe wants to become president let the system tell us based on those credible criteria for the Greater Good for all Tanzanians..... tusichakachue mfumo... mfumo utatuchakachua....
Nimekupa "like" lakini nimetoka kapa! Hata sijaelewa unaongea kitu gani? Kwenye thread ya msingi hakuna anayesema Zitto ni kiongozi mbaya. Hizo sifa zote za Zitto ulizozitaja zipo kwenye thread ya msingi. Lakini kumeelezwa pia mapungufu yake, na ameshauriwa kwamba akitaka kuvuka mto asianze kuvunja daraja kabla hajapita. Wewe unalisemeaje hilo. Kwa kuwa Zitto ni kiongozi wako wa mfano, basi anayo ruhusa ya kuharibu chama? Kikishakufa, yeye atafikiaje hizo ndoto zake?
 
Back
Top Bottom