gollocko
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 2,945
- 2,281
Lotus posture si mchezo...
Ni kweli kabisa.
Kukaa Lotus pose inasaidia sana damu kuzunguka sehemu ya juu ya mwili mpaka kwenye ubongo, inaweka uti wa mgongo katika mpangilio maalumu wa Chakra, na pia inakupa shape ya pembe tatu, ambayo ni shape nzuri kuchukua cosmic energy. Pia ni mkao ambao mtu akiuzoea anaweza kukaa muda mrefu bila kuhama. Wapo ambao wanakaa kwenye meditation kwa siku nzima mpaka zaidi ya siku bila kuhama wala kubadilisha mkao.
Ni mkao mgumu kuuzoea lakini unazoeleka taratibu kutokana na kukaa kwenye meditation kwa muda mrefu.
Pia mtu anaweza kuanza na mkao wa kawaida tu na taratibu Lotus pose itakuja.
The prezident hii meditation yako ni nzuri inaleta relief kwenye mwili ila mara unapoimaliza kiganja cha kulia huwa kina joto kuliko cha mkono wa kushoto na vilevile naona kama inaondoa appetite.
Kufanya Meditation Bila Muongozaji Sawa Na Kumjazia Mtoto Au Mtu Anaeanza Kujifunza Kusoma Vitabu Vya Kusoma Bila Kumwambia Aanze Na Kipi Na Aanze Vipi Sana Sana Ataviangalia Tu.... Get A Teacher To Guide You And After One Month You Can Lead Yourself...
Rakims
UNACHOKISHAURI HAPO JUU NDIO MEDITATION YENYEWE kweli ujinga ni bahari ya mwerevu-BULLSHITIts bullshit you're just wasting your time, omba Mungu, ingia chumbani kwako piga magoti, mweleze Mwenyezi shida yako atakupa unachotaka... Meditation!?? Bullshit
Mkuu, inamaana unaweza ukaanza na crossed leg, halafu lotus posture ika jitengeneza yenyewe...?!
Mkuu umetoa ufafanuzi mzuri sana kabisa. Mimi binafsi mengi katika uliyoeleza hapo juu kama faida ya meditation nimeyapata lkn si kwa meditation bali kwa kutenga muda wangu kila siku asubuhi na jioni kwa ajili ya kutafakari utakufu wa Mwenyezi MUNGU. So unaweza ukatenga muda kwa ajili ya mola wako mlezi na utapata faida maradufu ya kufanya meditation pekee. Au meditate katika neno la Mwenyezi MUNGU, usimeditate katika vitu usivovijua.Lengo la Meditation ni simple. Lakini faida zake ni nyingi. Faida zake ni kutoka katika lengo moja. Na kila faida inaweza kuleta faida nyingine. Kuna faida kuu au lengo kuu ambalo matokeo mengine hutokea kama matawi. Ni kama mti na matawi. Lengo ni kuweza kutoa mshikilio uliopo akilini ambao kwa kawaida huonekani kwani tumezoea hali ya kushikilia akili zetu na hatuifahamu nature ya akili yetu.
Sio lengo ni kupata vipaji, sio kuwa na utajiri, sio kupata nguvu za ajabu, au jinsi wengi wanavyofikiri. Kuipata furaha ya kweli, kujitambua, kudhibiti hisia, mazoea, tamaa, hasira, chuki na ubinafsi, na kuweza kuiongoza akili yako. Hayo ni matokeo tu na faida za meditation zinazotoka katika faida kuu. Na faida hizo zinaweza kuzaa nyingine zaidi kama vile kuwa na tabia njema, kuacha mazoea mabaya, kujifahamu na kufahamu akili na ufahamu wa watu. Na faida hizo zinaweza kuleta faida zaidi kama kuwa na maisha mazuri kwani unaweza kujithibiti na unaishi vyema kwa akili na busara, unaweza kushirikiana na watu, unaweza kujidhibiti na kujitawala na kuwa mtu wa haki na msimamo. Pia unakuwa mwepesi kuisikia nafsi / intuition.
Kinachowarudisha nyuma wengi ni kuwa hawapitii kwanza maelezo ya mwanzo ya kuyafahamu kama vile akili ni nini, ina nini, ufahamu ni nini, una nini na nini. Akili ipoje na Ubongo? Ubongo na milango ya ufahamu vimeungana vipi na ufahamu? Chanzo cha mawazo ni nini? Ufahamu upoje na akili? Akili na mwili vimeunganika wapi? Wazo ni nini? Kulala ni nini? Nini kitatokea usipolala? Ndoto ni nini? Baada ya kupitia introduction kidogo ya kufahamu sayansi hiyo ndipo utatambua meditation ni nini na kwanini kuna meditation. Wengi huanza kusomea meditation bila kufahamu maelezo ya mwanzo katika kujifahamu na kufahamu ufahamu na akili ni nini.
100% true. Nina miezi kadhaa tangu nianze mtiririko huu exactly kama ulivosema. Cha ajabu ni kuwa nimebadilika sana kitabia na kimwenendo katika maisha ya kila siku. Hata mahali ambapo watu wamekata tamaa mm nimekuwa nikijikuta bado nina tumaini kubwa. Siri kuu ni kumtanguliza Mwenyezi MUNGU mbele, Kutafakari (meditate) maneno yake na kutenda sawasawa na maneno yake. Kutenda bado sijafanikiwa 100% but namshukuru Mwenyezi MUNGU kwa mengi amenionesha. Zamani nilikuwa nadhani nina mapungufu mawili tu lakini mara baada ya kutafakari maneno ya Mwenyezi MUNGU nikaanza kugundua madhaifu yangu ya day to day na kisha kuanza kukomaa kueliminate moja baada ya jengine. Sio kazi rahisi, lazima ujitoe. Hiyo ni meditation kwa mtizamo wa maneno ya Mwenyezi MUNGU. Hata shetani ana meditation, tuwe makini tusijefuata nyayo za shetani maana wapo wengi wanafanya mediation ktk mtindo ambao ni ibada kamili ya kishetani bila wao kujua kumbe wanawasiliana na roho wa kuzimu.kaka naomba ni kusaidie nini maana ya meditation.
Kwa kiswaili ni (kutafakari)
inafaida kubwa sana kama utazingatia siku zote. Faida yake ipo hata kwenye mambo ya kiroho. Ukitaka uwe mtu mwenye ufahamu mkubwa juu ya mambo ya Mungu. Basi meditation mambo ya Mungu na maneno yake.alafu uyatende yale unayo yasoma. Utakuwa na uwepo wa Mungu siku zote.
Tuje kwenye eneo la maisha ya kila siku Meditation ni msingi wa mwanzo wa mafanikio yako.
Huwezi kufanikiwa kama wewe si mtu wa kutafakari yaani (meditation)
hapa ndipo wazungu wanapotushinda siku zote. Cm unayoitumia wazo la kutengeneza cm lilitokana na meditation.
Matajiri wote unaowajua mwanzo wa mafanikio yao au wazo la biashara au makampuni wanayo ya miliki. Yalizaliwa kutokana meditation.
Mimi labda ni kupe mbinu ambazo mimi nazitumiaga na zimekua na faida nyingi sana katika maisha yangu ya kibiashara.
1 kumcha Mungu.
2 maisha ya maombi.
3 kutenga muda usiopungua saa 1 kila siku kutafakari.
Naomba ni zungumze eneo la 3 yaani tafakuri.
Tafuta sehemu ya utulivu isiyo na makelele. Jizoeshe kila siku kukaa hapo peke yako. Kwa muda usiopungua masaa2.
Haza kutafakari shida za watu. Na jinsi utakavyozitatua. Zama kwa undani juu ya mambo ambayo hayapo na fursa zilizo kuzunguka.
Anza hapo mtaani kwenu unapo kaa. Yatafakari mazingira na ni nini unachokiona hapo mtaani kama kero.
Anza kubuni miradi. Chukua kalamu na karatasi. Andika kila wazo. Linalo kujia. Au fursa unazoziona hapo ulipo.
Hesabu gharama. Itakugharimu mtaji wa kiasi gani. Utapata faida kiasi gani. Chemsha. Akili yako ifanye izunguke itafute majawabu.
Ukisha maliza. Sasa rudi kwa Mungu hapa na zungumzia. Maombi mwombe Mungu. Akuongoze. Akupe hekima. Na Nguvu ya kuyatenda yote uliyoyapanga.
Na kuhakikishia maisha yako hayatakua kama yalivyo kuwa sasa. Lazima utajiri ukujie ndugu yangu.
Asante kwa kunisikiliza:
Kuonesha kuwa ukweli unafunuliwa, hata kukua kwa teknolojia ni moja ya kufunuliwa; Tukumbuke miaka elfu iliyopita hivi mtu angejua kuwa kuna kitu kinaitwa Skype kitatokea au watu wangesafiri angani???. Nakubaliana na ww kuwa ukweli bado unaendelea kufunuliwaInatubidi tuweke dini zetu pembeni kwa sababu zimefunga ukweli usijulikane kwa kuuwekea limit kwa kuonyesha sisi tuliobaki hatuwezi na kuwafanya wale wazamani waliojitambua kama miungu jambo ambalo sio.
Hapa namaanisha kwamba ukweli haupo ndani ya wakristo tu au wahindu tu au wabudha tu au waislam tu. Ukweli unaendelea kufunuliwa mpaka sasa.
Kuhusu kutumia neno mkuu tafakari mwenyewe utakuta sio sawa.
Nimejifunza kitu kaka. Mimi ni muislamu lakini hilo neno la Zaburi 1: 1-3 nimelishika kwa magego yangu na sitaki linitoke kinywani mwangu. Ni neno ambalo ukilitafakari ni lazima utaenda mbele zaidi na kutaka kuijua sheria na kuitekeleza kwa vitendo kisha utashangaa maajabu ya jinsi utakavostawi na kushamiri ktk maisha yakokaka ni kweli kabisa kumeditate sio jambo rahisi kama wengine wanavyofikiri.
Mimi ilinigharimu 1 kuyalazimisha mawazo yangu ya kubaliane na kile ninacho kikusudia.
Haikua kazi raisi kaka wala halikua jambo la siku 1. Ilinichukua muda mrefu mpaka kuanza kuzoea hiyo hali.
Labda ni kupe mbinu iliyo ni saidia kwa uraisi.
Mimi ni mkristo.
Na ninapenda sana kutumia muda mwingi kufanya ibada na Mungu wangu.
Napenda sana kusoma neno la Mungu. Na kutafakari Neno la Mungu. Ihi ilinisaidia sana kwanza kuflash mawazo yote yasiyo na utukufu wa Mungu juu ya maisha yangu.
Hapa ndipo ili kua mwanzo wa kuanzia. Na neno lililo ni shep ni (Yoshua 1:8 na Zaburi 1:1-3)
Neno linasema:
- KITABU HIKI CHA TORATI KISIONDOKE KINYWANI MWAKO, BALI YATAFAKARI MANENO YAKE MCHANA NA USIKU, UPATE KUANGALIA KUTENDA SAWA SAWA NA MANENO YOTE YALIYO ANDIKWA HUMO, NDIPO UTAKAPO IFANIKISHA NJIA YAKO NA KUSTAWI SANA:
katika maneno haya ni kachukua:
1 - kujikiria mambo mazuri.
2 - kumeditate
3 - kujifunza
uho ndio ulikua mwanzo wa safari yangu ya mafanikio. Kwa kuwa eneo la maisha yangu kiroho liko vizuri.
Nikaamishia baadhi ya mambo katika eneo langu la uchumi kupitia mfumo ule ule wa kumeditate. Mambo ya kimaendeleo.
Na neno lililo ni sukuma zaidi lilikua (Mithali 21: 5)
- MAWAZO YA MWENYE BIDII HUUELEKEA UTAJIRI:
hapa sasa ni katenga chumba changu maalum. Ni kawa kila siku kuanzia saa 1 - 2 usiku. Nakaa peke yangu na kuanza kutafakari vitu ambavyo ni kivifanya vinaweza kunibariki na kubadilisha maisha yangu. Kutoka kwenye umaskini kwenda kwenye utajiri.
Nilikua na daftari langu na kalamu yangu. Nikaanza kutafakari shida mbali mbali zinazowakabili watu.na ni nini solution yake.
Na mimi nikajiweka kama mtatuzi wa hizo kero au shida za watu.
Gafla mawazo ya miradi ikawa inakuja kama maporomoko ya mto upitishao maji.
Ni kaanza kuandika miradi. Na kupiga hesabu - gharama na faida. Nikajikuta nimefungua miradi mingi na inayoniingizia pesa nyingi sana na kuagana na umaskini.
Sifanyi biashara kama sijui faida yake ni kiasi gani na nitawekeza kiasi gani. Ihi imenijengea tabia ya kujua ni faida kiasi gani nitapata kwenye kila uwekezaji ninao kusudia kuufanya.
Siwekezi bila kufanya tathimini kwanza. Haya yote ni faida ya Meditation.
Ukiamua yote yanawezekana.