Ushuhuda wa ukweli kuhusu meditation

gollocko

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
2,945
2,275
Wanajamvi,

Hebu nisaidieni kufahamu faida za hii meditation katika maisha yetu ya kawaida. Nimejaribu kuifanya kwa miezi mitano sasa sijaona tofauti yeyote ya maisha yangu kabla ya meditation na sasa ninapoendelea nayo.

Nimewafuatilia sana Pasco, Rakim na mshana jr lakini naona patupu. Hebu waliofanikiwa nisaidieni(kama mtakuwepo), toka muijue hii meditation imeeasaidia nini na kwa njia zipi?.
 
makosa yako
1)"Nimejaribu"
2) umekuja kutangaza humu
3) huna uvumilivu/imani

NB: you lack 'self di
scipline'
Mkuu kama unaweza nieleza uvumilivu na imani kikomo chake ni kipi itakuwa vizuri.pia sijaja kutangaza hii meditation na mifano yake nimeifahamia humuhumu jf sio kosa kuiulizia hapahapa jamvini. Self discipline unayoizungumzia ni ipi? Kutaka kuifahamu viziri hii meditation?
 
Its bullshit you're just wasting your time, omba Mungu, ingia chumbani kwako piga magoti, mweleze Mwenyezi shida yako atakupa unachotaka... Meditation!?? Bullshit
Ukiwasoma akina Pasco,Rakims na Mshana jr, unaweza kuona kama kunamanufaa ila kiukweri mpaka sasa sijaprove kitu.
 
Una hakika gani kuwa hiyo unayofanya ni meditation labda unakosea je???
Una mwalimu aliekuongoza siku za mwanzoni au unafanya tu mwenyewe??

Ulitegemea kupata faida gani??? (Pesa au??) maana kulingana na swali lako ni kama ulitegemea kupata kitu flani mara tu ilipoanzia kufanya taamuli.

Pia faida kubwa ni kujitambua sasa we kulingana na huu uzi wako ni kwamba bado hujajitambua.... Unahitaji kujitambua zaidi mkuu ili niweze kupata faida za taamuli kimwili na kiroho pia.
 
Meditation inafaida kubwa sanaaa katika kimwili kiakili na kiroho pia.....kwa kufanya meditation unaweza pata solution za vitu mbalimbali katika maisha endelea kufanya meditation mala kwa mala at least mala mbili kwa siku...

Mkuu ndio nataka unishuhudie hizo solution mbalimbali ulizozipata kutokana na hizi meditation.
 
PHP:
Una hakika gani kuwa hiyo unayofanya ni meditation labda unakosea je???
Una mwalimu aliekuongoza siku za mwanzoni au unafanya tu mwenyewe??

Ulitegemea kupata faida gani??? (Pesa au??) maana kulingana na swali lako ni kama ulitegemea kupata kitu flani mara tu ilipoanzia kufanya taamuli.

Pia faida kubwa ni kujitambua sasa we kulingana na huu uzi wako ni kwamba bado hujajitambua.... Unahitaji kujitambua zaidi mkuu ili niweze kupata faida za taamuli kimwili na kiroho pia.

Hayo maswali yako mawili ya mwanzo yote jibu ni ndio. Kwa kufuata maelekezo niliyopewa na thread za meditation hapa jamvini ninauhakika hii ninayofanya ni meditation.

Kuhusu kutojitambua inawezekana unavyosema ni kweli, ila ninachotaka kufahamu ni kuwa wewe uliojitambua, umejitambuaje?
 
Acheni msifanye kazi bakini na meditation zenu hzo. Wenzio waleeee......

Senior boss, kwa mujibu wa waliotoa hizi mada za meditation au ukifuatilia mitandaoni, hii kitu imeanzia hukohuko kwa wenzetu
 
Siri ya utajiri ni kazi ( working smart ) na ubahili baaas. Hakuna uchawi, miujiza, sijui meditation wale dada yake nani.

Aisee umenivunja mbavu, ila sijasema nataka utajiri.Ninachotaka ni wale waliofaidika nayo ndiyo wanieleze ili nami nifaidike na maelezo yao. Manufaa sio lazima upate pesa nyingi.
 
Hahaha wengi ndio wanafsiri mafanikio hvyo....Bob mi hayo ma vitu hata sijisumbui. Tehe

Yawayo mafanikio yoyote, iwe pesa,iwe vipawa mbalimbali au hata ule utofauti tu waliouona kabla na baada ya meditation
 
Tafuta sehemu wanayofundisha uwe unahudhuria vipindi vyote ili kujenga ufahamu wako. Na uende pale kujifunza mafanikio yatakuwa matokeo ya mafunzo.
Ukifika umweleze mwalimu wako haya malalamiko yako yeye atakusaidia zaidi.

Cc: [MENTION=17550]mshana Jr Pasco Appolo

Kila LA heri
 
Last edited by a moderator:

Akhsante jibu murua hili, vipi wewe huwezi angalau nielezea mafanikio yako katika hii nyanja?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom