Lengo la Meditation ni simple. Lakini faida zake ni nyingi. Faida zake ni kutoka katika lengo moja. Na kila faida inaweza kuleta faida nyingine. Kuna faida kuu au lengo kuu ambalo matokeo mengine hutokea kama matawi. Ni kama mti na matawi. Lengo ni kuweza kutoa mshikilio uliopo akilini ambao kwa kawaida huonekani kwani tumezoea hali ya kushikilia akili zetu na hatuifahamu nature ya akili yetu.
Sio lengo ni kupata vipaji, sio kuwa na utajiri, sio kupata nguvu za ajabu, au jinsi wengi wanavyofikiri. Kuipata furaha ya kweli, kujitambua, kudhibiti hisia, mazoea, tamaa, hasira, chuki na ubinafsi, na kuweza kuiongoza akili yako. Hayo ni matokeo tu na faida za meditation zinazotoka katika faida kuu. Na faida hizo zinaweza kuzaa nyingine zaidi kama vile kuwa na tabia njema, kuacha mazoea mabaya, kujifahamu na kufahamu akili na ufahamu wa watu. Na faida hizo zinaweza kuleta faida zaidi kama kuwa na maisha mazuri kwani unaweza kujithibiti na unaishi vyema kwa akili na busara, unaweza kushirikiana na watu, unaweza kujidhibiti na kujitawala na kuwa mtu wa haki na msimamo. Pia unakuwa mwepesi kuisikia nafsi / intuition.
Kinachowarudisha nyuma wengi ni kuwa hawapitii kwanza maelezo ya mwanzo ya kuyafahamu kama vile akili ni nini, ina nini, ufahamu ni nini, una nini na nini. Akili ipoje na Ubongo? Ubongo na milango ya ufahamu vimeungana vipi na ufahamu? Chanzo cha mawazo ni nini? Ufahamu upoje na akili? Akili na mwili vimeunganika wapi? Wazo ni nini? Kulala ni nini? Nini kitatokea usipolala? Ndoto ni nini? Baada ya kupitia introduction kidogo ya kufahamu sayansi hiyo ndipo utatambua meditation ni nini na kwanini kuna meditation. Wengi huanza kusomea meditation bila kufahamu maelezo ya mwanzo katika kujifahamu na kufahamu ufahamu na akili ni nini.