USHUHUDA: Nilizaliwa na Virusi vya UKIMWI

USHUHUDA: Nilizaliwa na Virusi vya UKIMWI

Ulikuwa huugui mara kwa mara?
Kabla sijaanza kutumia ARV nilikua naugua mara kwa mara, haipiti miezi miwili bila kuumwa t ila tangu nianze kutumia ARV hali hiyo imepungua naumwa ila sio mara kwa mara, na nikiumwa huwa naumwa sana, Kwa kweli ni Mungu tu Mwenyewe tu mpaka sasa mie kuwa hai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla sijaanza kutumia ARV nilikua naugua mara kwa mara, haipiti miezi miwili bila kuumwa t ila tangu nianze kutumia ARV hali hiyo imepungua naumwa ila sio mara kwa mara, na nikiumwa huwa naumwa sana, Kwa kweli ni Mungu tu Mwenyewe tu mpaka sasa mie kuwa hai

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante

Umesema hujawahi kufanya mapenzi

Kama binadamu najua mwili una matamanio

Unakabiliana vipi na tamaa ya mwili?
 
Ukimwi inaelekea siku hizi hauui. Zamani mtu akipata maambukizi anaishi nao kwa miaka tano tayari imemmaliza.... Lakini siku hizi watu wako vizuri tu na afya tele. Kuna jirani yangu tangu mi niko shule mwanzoni mwa miaka ya 2000 yeye alikuwa anahudhuriaga semina kwenye NGO yao fulani. Wakati huo yuko flat ila sahivi amejaa anakitambi anapiga kazi vizuri amejiendeleza sana.
Zamani tatizo lilikuwa

1. Elimu
2. Ukosefu wa dawa
 
Kwa nini unasema hivyo mkuu.

Si naskia vijidudu vinaongezeka na ikifika muda vinakuwa vingi hata kuushambulia mwili na kukosa kabisa ulinzi ndani ya mwili...?

Hebu nipe darasa hapo kiongozi ipi bora kukaa bila ya kunywa hizo dawa au kukaa ukiwa unakunywa hizo dawa mkuu. Na pia, labda ni kipindi gani mtu anatakiwa kunywa hizo dawa coz mtoa mada ameishi kwa zaidi ya miaka 20 bila ya kunywa hizo dawa, it means hawezi kuacha right...?

Nipe darasa coz tunaishi na ndugu na jamaa huku mtaani hivyo tunaweza kuokoa maisha yao wakaendelea kuishi kwa njia moja au nyingine mkuu.

Thanks a lot kiongozi.
Kwa ufahamu wangu nasikia mtu aliyezaliwa na maradhi anaweza kuishi muda mrefu kuzidi aliyepata ukubwani sababu mfumo wa kinga unafanana na wa vijidudu, akizaliwa nao kinga na vidudu vinazoeana havishambuliani ila anayepata ukubwani vijidudu vikiingia tu cell zinaelewa kaingia adui inakuwa vita
 
Daaah rest in peace to her, cha msingi ni kujikubali tu,harakati zimeanzia jamii forum ila nina mpango wa kuanza kuposti Facebook kisha Instagram na ikitokea sponsor wa kwenye Tv station pia nitafanya hadi kwenye tv pia
Kuna swali umekwepa huko kwa kuhofia kujulikana sasa huko kwingine kama kwenye tv utafanyaje
 
Wapi Mkuu tuanze kununua tuweke stock just in case? Naamini ikipatikana madukani watu wengi watainunua bila hata kupima afya na wengine wataji overdose
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Finally, kutooa au kutozini haina maana yoyote tafuta mtu wa hali yako ufurahie maisha

Kufurahia maisha ni jambo la msingi huwezi kusema unatenda dhambi kwa kutooa ila dhambi ni unaoa/unazini na nani?
 
Cd4 kushuka inasababishwa na vitu vingi baadhi ni kupata milo duni,kufanya ngono zembe,kuwa na msongo wa mawazo(stress)na kutotumia dawa za Arv
Kwa upande wangu kuanzia mwaka jana nilianza kuishi mwenyewe hivyo nikawa nakosa mlo kamili uliojitosheleza ukijumlisha na kutotumia Arv ni lazima Cd zishuke mkuu ila nashukuru sasa zimepanda kwa kiasi kikubwa mno na ninazingatia mlo kamili hata iweje bora nikose vyote lakini sio kukosa milo mitatu yenye nguvu
Hapa ndio napata majibu kwanini watu masikini hufa haraka wa ukimwi.
Hukosa milo kamili na msongo wa mawazo.
 
Nina mama yangu mdogo ana HIV alioata mwaka 1989, hadi leo. Ukimuona kila siku anakuwa binti tu.
Anasema dawa za asili zinamsaidia sana kushusha madhara ya ARV. Anatumia dawa hizi
1: anakunywa vitunguu swaum kila siku vile vichane viwili, asubuhi na jioni
2: anakunywa maji kama kichaa
3. Anatumia Asali, mdarasini na tangawizi ( anachemsha tangawizi na mdalasini , vikishapoa anaweka kijiko cha asali). Amemuajili mfanya kazi kwaajiri ya kumtengenezea hizo dawa tu. Kwa hiyo kila siku lazima azinywe.
Yani ukimuona utadhani mimi ndio mzee. Wakati anaeeza kunizaa kabisa.
 
yaani ukiona umejikubali kwa kiasi hicho hasa katika jamii yetu hii inayotuzunguka, jua ni kwa neema tu, make most of them hutoa koment wanazozijua wenyewe, big up sana bro I swear God is great KAMA HUTO JALI NAOMBA TUFAHAMIANE KIONGOZI, yaan mpaka hapo Una uwezo wa ziada Mungu kakutunuku. All glory to the Allmighty God.
 
Back
Top Bottom