USHUHUDA: Nilizaliwa na Virusi vya UKIMWI

USHUHUDA: Nilizaliwa na Virusi vya UKIMWI

positive is normal

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2017
Posts
520
Reaction score
978
Habari wakuu,

Natumaini mko poa na Christmas na hata kama uchumi hauko sawa yapaswa kushukuru MUNGU maana kikubwa ni uzima na afya tu.

Dhumuni la uzi huu ni kuwapa moyo wale wote wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wajione kama watu wa kawaida na kuwa na virusi vya UKIMWI sio mwisho wa maisha.

Mimi ni kijana jinsia ya kiume, nilizaliwa na Virusi vya UKIMWI miaka 24 iliyopita na mpaka leo niko mzima wa afya na ukiniangalia kwa macho hutofikiria kama naishi na Virusi.

Waathirika wote msikate tamaa na wala msihuzunike, kila kitu kinatokea kwa sababu fulani.

Natanguliza shukrani kwenu na muwe na Christmas njema.

Mwenye maswali au maoni nitamjibu hapa hapa
 
Mara ya kwanza kupima 2007, nikapima 2009, halafu nikapima 2015.

Nyakati zote nilikua uncomfortable kusubiri majibu. Ile moment haizoeleki.

Mleta uzi nakupa hongera kwa attitude yako, samahani sikupi pole unastahili pongezi
Ahsante Mkuu, Ukimwi upo mkuu na wenye Virusi tupo pia mtaani ila kwa macho ni vigumu kututambua,nina afya nzuri tu,sifikirii kusambaza kwa mtu mwingine yoyote yule,pongezi na kwako pia
 
Vp mpk leo na miaka yako iyo 24 ushakutana na wadada wangapi na je unatumia kinga ay ndo ivo tena kifo cha wengi furaha
Sijawahi kuzini na msichana yoyote yule ,nimewahi kutongozwa mara kadhaa ila niliamua kukataa si vyema kuusambaza ugonjwa huu naamini dawa ya ukimwi ipo siku itapatikana
 
Back
Top Bottom