USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.
Wahusika fanyieni kazi taarifa... na wazo la kutoa zawadi kwa mtoa taarifa zitakazowezesha kukamata mafisadi na wahujuku linapaswa kuangaliwa. Iko mifano mingi kwa mataifa ya nje na hasa makubwa kama USA kuna sheria ya kitu kinaitwa "whistle blowers Act " Hii humzawadia mtu yeyote atayetoa taarifa zozote zitakazo ibua, fichua au kuimarisha usalama wa nchi.
Dole Magufuli kutimiza siku 100 kwa azima ya kubadili heshima ya nchi kutoka utajiri wa kifisadi kuelekea ujira halali kwa kazi halali ya kuutumikia umma wa watanzania.
 
Uko detailed Ndugu! Naungana na wewe kwenye ushauri wako kwa Mh. Rais. Intelligence & Security Services wanatajwa sana kwenye ukwapuaji siku hizi! Miaka hii wapo maafisa wa Idara hiyo wanaoona sifa kujulikana hata pale inapokuwa si lazima. Hii ni kwa sababu wanaona fahari kujulikana na kuogopwa kitu ambacho kwa kiasi kikubwa ni kinyume na sheria inayosimia kazi na uwepo wao!
Kama watatumika kumpa rais taarifa ni wazi kuna maeneo taarifa zao zitakosa usahihi kwa sababu ya maslahi binafsi.
Ni vizuri kiongozi wetu akaitazama vizuri taasisi hiyo na kuisafisha kwa umakini ili imsaidie kuwa na taarifa za kutosha katika utekelezaji wa majukumu yake!
 
Asante kwa taarifa Mkuu tunahitaji watu wazalendo kama wewe tunajua wakati ule wa Mkwere ata ungejitokeza ukayasema haya kwa uwazi ungeambiwa hakuna ushahidi na hakuna ambaye angekuelewa.
 
Unefanya kitu cheap lakini ni kikubwa sana kiongozi,

Umetujuza ni vipi mambo yalivo .... Usalama wa taifa wanataarifa tayari .. Au tuseme kuwa ssisi tunajua kama wao usalama wanajua alafu hawafanyii kazi.....!!!

Kwa jinsi watz tulivo na imani na jpm, ikiwa wana taarifa halafu hawafanyii kazi iyo itakuwa balaa....!
 
Hi stori ina walakini sana. Ni stori ya kusadikika zaidi.
Sasa hivi Hizi kampuni hazileti meli za mafuta.
Utaratibu unaotumika ni kuwa kila quarter kuna bulk importer mmoja ambaye analeta mafuta. Sio oil com wala world oil au babake yoyote anae agiza mafuta kutoka nje.
Utaratibu uliopo ni kuwa bulk impoerter analeta mafuta na yanashushwa yote kwenye deport ya tipper.
Huyu anaye shunda tenda ndie anaelipa ushuru kwa mafuta yote ysnayo ingia.
Na tangu utaratibu huu kutumika hakuna local company ilo shinda tenda hii..
Makampuni ya ndani yananua mafuta kutoka muagizaji mafuta ambayo yameshalipiwa ushuru wa kuingiza wao hawahusiki na hizo taratibu za kubadilisha Jet na diesel.
Utaratibu huu ndio ulowezesha EWURA kuweza kuweka bei ya mafuta kwa mlaji kwa sababu wote hawa wananunua bei ile ile kutoka kwa bulk importer...serikali inachukua chake yakkingia tu.
Hivyo ni uongo wa mchana kusema kuna meli imeagizwa na oil com au babako nani...
Hizi ni chuki kwa warabu kwa sababu ndio umetanguliza hayo.
Na world wenyewe ni wwswahili walo amka wachapa kazi.
Mafuta yanayo enda nje ya nchi huagizwa na nchi husika na makampuni ya hapa hushughulika na usafirishaji tu.
Hivyo stori sijui alikua ashushe meli diesel lakini imeandikwa jet 1 ni yauongo.

Kama kuna ulaji katika mita basi mchezo anacheza bulk importer ..usiootoshe watu kwa sababu za chuki binafsi
bopwe wacha kutufanya wote tu wajinga,we unaambiwa wizi huu ulikuwa unamuhusisha mpaka Masamaki mwenyewe mkuu wa ushuru wa forodha halafu we unataka kuleta maneno yako??
Kwamba jamaa ana wivu na waarabu sijui wahindi??There is a thin line btn racism and patriotism!!OILCOm si ndio yule mbunge wa kanda ya Ziwa?mwenye asili ya Asia?nyie acheni kutuletea mchezo nyie,watu wamezima pump miaka 5 iwe hiyo ya kukwepa utaratibu?unadishi wako tu unaonyesha umetumwa uje utetee,thread toka asubuhi ndio mnajipanga kuleta utetezi saa hizi
 
Habari kama hizi tulikua tunazipata kupitia magazeti kama Mawio lakini Mungu ni Mnene! Sasa hivi zimo humu live bila chenga!
 
Ndio maana watt wa kiarabu usku walikua wanatusumbua sana mitaa ya Coco na magari yao ya mabilioni kasorobo? Mamamaayee zao, anko Magu zaa nao hawa mbere kwa mbere.....
 
Hi stori ina walakini sana. Ni stori ya kusadikika zaidi.
Sasa hivi Hizi kampuni hazileti meli za mafuta.
Utaratibu unaotumika ni kuwa kila quarter kuna bulk importer mmoja ambaye analeta mafuta. Sio oil com wala world oil au babake yoyote anae agiza mafuta kutoka nje.
Utaratibu uliopo ni kuwa bulk impoerter analeta mafuta na yanashushwa yote kwenye deport ya tipper.
Huyu anaye shunda tenda ndie anaelipa ushuru kwa mafuta yote ysnayo ingia.
Na tangu utaratibu huu kutumika hakuna local company ilo shinda tenda hii..
Makampuni ya ndani yananua mafuta kutoka muagizaji mafuta ambayo yameshalipiwa ushuru wa kuingiza wao hawahusiki na hizo taratibu za kubadilisha Jet na diesel.
Utaratibu huu ndio ulowezesha EWURA kuweza kuweka bei ya mafuta kwa mlaji kwa sababu wote hawa wananunua bei ile ile kutoka kwa bulk importer...serikali inachukua chake yakkingia tu.
Hivyo ni uongo wa mchana kusema kuna meli imeagizwa na oil com au babako nani...
Hizi ni chuki kwa warabu kwa sababu ndio umetanguliza hayo.
Na world wenyewe ni wwswahili walo amka wachapa kazi.
Mafuta yanayo enda nje ya nchi huagizwa na nchi husika na makampuni ya hapa hushughulika na usafirishaji tu.
Hivyo stori sijui alikua ashushe meli diesel lakini imeandikwa jet 1 ni yauongo.

Kama kuna ulaji katika mita basi mchezo anacheza bulk importer ..usiootoshe watu kwa sababu za chuki binafsi
Hebu tusaidie huyo bulky importer mmoja wapo ni nani?
 
Umeenda mbali sana mkuu. Hawapaswi kufa bali kufilisiwa wao na jamaa zao na rafiki zao wote. Hii italeta discipline ya kuonyana sisi kwa sisi
Hamna mkuu inauma sana mkuu....yaani hawa si watu ni wanyama kabisa....
 
Cha msingi hapa ni kuzifuta hizi kampuni na kuzifilisi, wahusika kunyongwa hadi kufa maana kwa matendo yao wameua watanzania wengi mahospitalini, barabarani, mashambani na sehemu zingine
 
bopwe wacha kutufanya wote tu wajinga,we unaambiwa wizi huu ulikuwa unamuhusisha mpaka Masamaki mwenyewe mkuu wa ushuru wa forodha halafu we unataka kuleta maneno yako??
Kwamba jamaa ana wivu na waarabu sijui wahindi??There is a thin line btn racism and patriotism!!OILCOm si ndio yule mbunge wa kanda ya Ziwa?mwenye asili ya Asia?nyie acheni kutuletea mchezo nyie,watu wamezima pump miaka 5 iwe hiyo ya kukwepa utaratibu?unadishi wako tu unaonyesha umetumw asubuhi a uje utetee,thread toka ndio mnajipanga kuleta utetezi saa hizi
Hujui kitu..bwana unafata mkumbo tu.
Oil com sio ya mu asia wala haina uhusiano na mbunge.
Hii inaonesha vp unafata mkumbo tu.
Pump imeharibika na utaratibu wa zamani kupima ni bora zaidi.
 
mkuu nitakupa namba ya simu au email ya Mh. Rais ili umfafanulie vizuri na kwa lugha rahisi zaidi ili ajue pa kuanzia.

Asante.
kama una email yake tupia humu watu wana mambo mengi wanayotaka yafike kwa Raisi moja kwa moja.
 
wamaanisha Islam huyo wa Moro mwenye mabus?!! kama ndiye mbona mabasi yake yamepoteza mwelekeo au dili za mafuta zimenoga Zaidi?

Mijizi kama wewe ni hulo lunalojiita Islam wakati matendo yake ni ya kipagani anafaa kupigwa risasi hadharani. Ili kujenga taifa lenye nidhamu ni lazima ujinga unaoitwa haki za binadamu uwekwe pembeni kudogo
 
Mijizi kama wewe ni hulo lunalojiita Islam wakati matendo yake ni ya kipagani anafaa kupigwa risasi hadharani. Ili kujenga taifa lenye nidhamu ni lazima ujinga unaoitwa haki za binadamu uwekwe pembeni kudogo
Wajenga misikiti hao
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom