USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
nabado, wamesema ccm ni ileile na sasa wamejipanga, tarajia mwaka huu kukiona. kwa hiyo tegemea wizi zaidi ya huo
 
Nikisoma habari kama hizi naumia sana,imagine mtu mmoja anapewa mil. 80 za kumfunga mdomo!!!!
Najuta kuzaliwa Tanzania,Nchi ya wachache!
Wengine ni vile tumejikuta tumeshazaliwa Tanzania,hakuna namna nyingine!

Pole!!
 
Maskini tanzania yetu. ndio maana waarabu na waindi wanaishi mijini sisi tunaishi kimbiji
 
Nimejikuta natokwa machozi baada ya kusoma taarifa hii....yaani kila nikiona gari la OIL COM au kituo cha mafuta cha OIL COM.... najikuta natetemeka kwa hasira....
Hivi kwanini tusiwe tunawachinja hawa majizi jamaani....haaaaaaaaa......
Mkuu pole sana...hii NCHI ndio maana CCM kwenye Kampeni hawanaga Habari nakuomba vipesa hao watu ndio wanaowapa Sasa ila naona mwaka huu kama wameingia CHOO cha KIKE ngoja tusubiri muda utaamua lkn hali ni ngumu sana
 
Mungu tusaidie,kama Kuna watu WA usalama fanyieni kazi taarifa hii.

Mkuu Umeisha ambiwa Usalama wanahusika na usalama jamani ni kubwa mno msifikilie ni ndogo maana wako wengi mno na kinacho sumbua kabisa Usalama ni kuwa hatujui vitengo vyao kila mtu kule yy ni usalama na gamba lake lakini kujua specifically yy katokea Department ipi hakunaga nchi, hii ni kama CIA NSA FBI kwa mfano tuu nimewapa Je hapa Bongo Usalama ni usalama tuu so huo Muhimili wa Usalama wa taifa nao Utumbuliwe maana wao kabisa wanajua Issue zotee piga uwa wantambua so kwa style hiyo JPM anayo kazi kubwa saana kusambalatisha huo mtandao.

My Take:
Usalama wa Taifa kuna uchafu mkubwa pia na wao ndio Namba one katika hili, kama huko nchi za magharibi hizo agency zinachunguzana wao kwa wao so watu wanakuwa makini katika kazi zao hapa utamchunguza nani wote mnajiita usalama mnareport office mmoja khaaaaaa, wanatuchora hawa watu
 
Inaweza kuwa nzuri .


http://s07.jamiiforums.com/mini/uyE8/bg_000000/txt_000000/border_000000/flags_0/
 
umeongea point kuna vijana wengi wenye moyo safi wanasota mitaani Magufuri futa ajira zote zenye mkondo wa wizi tuanze upya
 
Nimekupata mkuu, Hii nchi narudia kusema kama magufuli nia yake nchi ikae sawa.fukuza TRA wote maafisa na pale TPA ondoa kabisa kizazi cha panya tuanze upya tu,lakini kuondoa mmoja mmoja wakati walioshika system ni wale wale tunacheza tu
yees ondoa kizazi cha nyoka
 
IKULU mpaka sasa ilipaswa isha mwita mtoa taarifa na Huyo Anderson na hao wahusika tajwa hapo juu na Tarehe ya hiyo Issue ilikuwa lini turudi nyuma kwenye Roster zao siku hiyo utawajuwa wahusika wote this isn't a Jock buddies.

Sasa hapa ntakipa Kitengo cha usalama (IKULU) nafasi yake kufanya kazi hii
 
Kwa Nchi HII ilipofikia hata nipewe Urais Bure bila Sheria Ya kunyonga NAKATAA..
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.
 
Aisee. Hii nchi ina majizi sana. Risasi tu zilifaa kutumika. Unauwawa kwenye public huku familia yako wakitazama.
 
Taarifa nyeti sana hii... Sasa Makapuni ya simu yanaibia TAIFA MABILIONI kila mwezi... niko ktk utaratibu wa Kupeleka taarifa IKIBIDI TRA HEAD QUARTER, MAKAPUNI YA SIMU kama vile haya ya Mafuta yanakosesha BILIONS EACH MONTH... kwa kupiga deal na TCRA wasifunge ule mtambo maalum wa kujua mapato ya KILA KAMPUNI KILA MWEZI, ili serikali isijue pato halisi la kampuni husika, kwani mtambo UPO TAYARI PALE TCRA TOKEA JK AULETE... ila unapigwa tarehe, kazi kukagua simu za watu locally na internationally... badala ya kujua mapato ya makampuni haya yote ya Simu tungepata billions za kodi each month... wiki hii ijayo LAZIMA IWE ISIWE, NITAKUWA TRA HQ, kuhakikisha hili nalifikisha haraka... lazima TUMSAIDIE RAIS NA WAZIRI MKUU WETU kupambana na wakwepa kodi... kwa kila njia... lazima lazima... sasa ni sasa... TRA HQ lazima niwaeleze hili vizuri, na MAFUTA WAKIBANA BANDARI, serikali itapata mapato makubwa na kuwahudumia wananchi wetu kwa uhakika... nimeamua...hii ni vita, wakwepa kodi wote lazima washughulikiwe...
 
Ni rahisi sana kusimuliwa hadithi kama kama unaonaonyesha shauku ya kusikiliza, kwanza mimi nikushukuru binafsi, Muombe Mungu kwa ajili ya usalama wako. Maana hata JP anasema muniombee niendelee kutumbua majipu.
 
Aisee hivi Jakaya amepewa ukuu wa UDSM kwa kipi ?? Kuna kila sababu ya kubadilisha sheria inayokataza Rais wa Nchi asifunguliwe mashtaka ,huyo alitakiwa awepo kwenye house of arrest mpaka tunapo ongea hivi sasa,kama Magufuli dhamira yake ni ya dhati aanze na kufuta hiyo sheria then anyonge watu kama kumi hivi ndio mambo mengine yaendelee ,vinginevyo anampigia mbuzi gitaa
Nikisikia jina la Jakaya nasikia kichefuchefu usilitaje
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom