USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Muhongo bado anahisi hii serikali inaendeshwa kwa zengwe kama iliyopita, hatufai
Wajita siyo watu wa kufanya nao kazi haki ya nani! Majitu yana fitina kama nini? Magufuli futa kazi hili jitu! Aisee litakuwa limelowa huko liliko!!
 
Naendelea tena kumshauri Magufuli, badilisha fedha ya Tz na utoe muda wa wiki 2 tu kila mwenye hela yake awe amebadilisha. Pia kuwe na kiwango cha mwisho kuwa nacho cash (sema 20 m), mafisadi yameficha hela majumbani huku benki zikiwa tupu! Inakuwaje mtu anakuwa na 800 m cash? Jambo jingine futa TRA na TPA yote uajiri upya au ukachukue vijana jeshini uwakabidhi hivyo vitengo! Vinginevyo kila mwezi mtakuwa mnarudi bandarini kujionea maajabu!
 
Hi stori ina walakini sana. Ni stori ya kusadikika zaidi.
Sasa hivi Hizi kampuni hazileti meli za mafuta.
Utaratibu unaotumika ni kuwa kila quarter kuna bulk importer mmoja ambaye analeta mafuta. Sio oil com wala world oil au babake yoyote anae agiza mafuta kutoka nje.
Utaratibu uliopo ni kuwa bulk impoerter analeta mafuta na yanashushwa yote kwenye deport ya tipper.
Huyu anaye shunda tenda ndie anaelipa ushuru kwa mafuta yote ysnayo ingia.
Na tangu utaratibu huu kutumika hakuna local company ilo shinda tenda hii..
Makampuni ya ndani yananua mafuta kutoka muagizaji mafuta ambayo yameshalipiwa ushuru wa kuingiza wao hawahusiki na hizo taratibu za kubadilisha Jet na diesel.
Utaratibu huu ndio ulowezesha EWURA kuweza kuweka bei ya mafuta kwa mlaji kwa sababu wote hawa wananunua bei ile ile kutoka kwa bulk importer...serikali inachukua chake yakkingia tu.
Hivyo ni uongo wa mchana kusema kuna meli imeagizwa na oil com au babako nani...
Hizi ni chuki kwa warabu kwa sababu ndio umetanguliza hayo.
Na world wenyewe ni wwswahili walo amka wachapa kazi.
Mafuta yanayo enda nje ya nchi huagizwa na nchi husika na makampuni ya hapa hushughulika na usafirishaji tu.
Hivyo stori sijui alikua ashushe meli diesel lakini imeandikwa jet 1 ni yauongo.

Kama kuna ulaji katika mita basi mchezo anacheza bulk importer ..usiootoshe watu kwa sababu za chuki binafsi
 
Umeandika siku ya deal kulikua na meli ya Oil com(Uongo oil com hawaleti meli siku hizi) halafu unasema huu mzigo umekua declared kama Jet1 ..ati hiya yana Tax excemption ! Kwa Diesel ya transit ina lipa ushuru..wacha ujinga wewe kama huna kitu wacha choyo piga kazi upate..chuki kwa waarabu haikufikishi mahali utakufa na kijiba bure.
Na inshangaza watu humu waingia kichwa kichwa kila kinacho andikwa humu..watu wajabu kabisa
 
Duh Si mchezo nchi hii imetafunwa vya kutosha, sasa iwe basi!
OILCOM watumbuliwe!
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.
Asante kwa taarifa hiyo
 
Ulicho kifanya ni cha kizalendo sana na data zako zinaegemea kwenye ukweli,
Mimi nashauli nasisi tuanze kuibua kila ambacho tuna uhakika nacho tutakuwa tumemsaidia magufuli na serikali kwa ujumla

Nashauri raisi Magufuli au waziri mkuu wamwalike mzee Mkinga ikulu anayafahamu sana masuala ya bandari na jinsi wanavyoiba pale. Wamvumilie kwani ile sauti yake ya kupanda sana ni maumbile tu ila nina hakika atalisaidia sana hili taifa.
 
Do hii ni hatari.... yaani mpaka nimeogopa.... 80m
kila mmoja cash! !..... inahitaji moyo kuzikataa.... na hawa wanajua hakuna atakae kataa.... inahitajika total overhaul ya utaratibu wa mafuta hapa nchini....

Ameandika 'inasemekana', jee kuna yeyote aliyekuwepo akathibitisha hayo? Otherwise ni majungu tu.
 
Hi stori ina walakini sana. Ni stori ya kusadikika zaidi.
Sasa hivi Hizi kampuni hazileti meli za mafuta.
Utaratibu unaotumika ni kuwa kila quarter kuna bulk importer mmoja ambaye analeta mafuta. Sio oil com wala world oil au babake yoyote anae agiza mafuta kutoka nje.
Utaratibu uliopo ni kuwa bulk impoerter analeta mafuta na yanashushwa yote kwenye deport ya tipper.
Huyu anaye shunda tenda ndie anaelipa ushuru kwa mafuta yote ysnayo ingia.
Na tangu utaratibu huu kutumika hakuna local company ilo shinda tenda hii..
Makampuni ya ndani yananua mafuta kutoka muagizaji mafuta ambayo yameshalipiwa ushuru wa kuingiza wao hawahusiki na hizo taratibu za kubadilisha Jet na diesel.
Utaratibu huu ndio ulowezesha EWURA kuweza kuweka bei ya mafuta kwa mlaji kwa sababu wote hawa wananunua bei ile ile kutoka kwa bulk importer...serikali inachukua chake yakkingia tu.
Hivyo ni uongo wa mchana kusema kuna meli imeagizwa na oil com au babako nani...
Hizi ni chuki kwa warabu kwa sababu ndio umetanguliza hayo.
Na world wenyewe ni wwswahili walo amka wachapa kazi.
Mafuta yanayo enda nje ya nchi huagizwa na nchi husika na makampuni ya hapa hushughulika na usafirishaji tu.
Hivyo stori sijui alikua ashushe meli diesel lakini imeandikwa jet 1 ni yauongo.

Kama kuna ulaji katika mita basi mchezo anacheza bulk importer ..usiootoshe watu kwa sababu za chuki binafsi
Hapa kuna harufu ya ukweli 95.8% Ila kuna ambao watapiga kutokana na strees zao za maisha!!
 
Do hii ni hatari.... yaani mpaka nimeogopa.... 80m
kila mmoja cash! !..... inahitaji moyo kuzikataa.... na hawa wanajua hakuna atakae kataa.... inahitajika total overhaul ya utaratibu wa mafuta hapa nchini....
hatari asee mana unaeza kataa hyo 80m af mtoaji akawatafuta wahuni akawapa 10m wakuondoe duniani cku hyo hyo
 
kumbe ndo mana JK alisema wakwepa kodi hawatoacha kirahis,,asee ngekuwa Magu ningemuondolea kinga then nimuwajibishe
 
Mungu akubariki sana mleta uzi. Ujumbe huu murwa rais apite hapa aone watu wake walivyojitoa zaidi yake
 
Kwamaana hiyo Kati ya wale watu 9 walioenda kushuhudia wakiwemo TISS agents waliramba mil80??
 
Mkuu FUHRER nina imani hii taarifa imefika na itafanyiwa kazi, hii vita ya Ukwepaji kodi ni kubwa ila nia njema ya Rais wetu itatiwa nguvu na Mungu hatimaye watajulikana tu.............
 
Hii inaonyesha wazi kuwa kila wizi hujuma zinazofanyika bandarini ulikuwa una baraka za kiongozi/ viongozi waliokuwa serikalini tena ngazi za juu. Viongozi wa awamu hii inawabidi wavae uso wa nyani dume kupambana na hujuma zote hizi, otherwise kuirudisha nchi kwenye mstari wa uadilifu itakuwa sawa na kutafuta dawa ya kutibu ukimwi,
 
Sasa nimeelewa nikwanini "Nyerere" alitaka njia zote za Uchumi ziwe chini ya Serikali.
 
Uzalendo wako ndio unaohitajika katika nchi hii. God bless you!!!
Ukisema ukweli hakuna wanachofanya napingana na wewe kwa asilimia elfu,kwanza wapongeze maana hata mtt akizaliwa kuna hatua zake mpaka kutembea,hapa viongozi wetu walipoanzia ni pazuri maana wanachfanya kinaonekana na watanzania wote,sijui wewe ndugu kwa nini unasema amna wanachofanya?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom