Ushauri: Zitto aanzishe Chama chake kingine...

Ushauri: Zitto aanzishe Chama chake kingine...

Status
Not open for further replies.
Bado kuna wanaoona Zitto (ukiondoa labda yeye mwenyewe) anafaa kugombea urais (achilia mbali kuwa rais kabisa)?
 
Hayo ni mawazo yako tu, ukweli wenyewe unapasua bila kujali mipaka ya bandia.
Hapa Marekani ukitaka kumwangusha mtu kisiasa unamwita Mkommunist wenye kutaka kunyang;anya kwa wenye nacho na kuwapa wasio nacho.
kwetu Tanzania mtu anaitwa informer.
Kifupi ni hivi kinachoendelea ndani ya CDM si siri na wala hakihitaji informer. CCM waliweka mawazo yao ndani ya CDM hata kabla ya kuzaliwa. kwa nini wahitaji informer wakati the whole idea ni ya kwao???

Sisi tunao fuata kinjaanjaa diyo tunadhani kuna SIRI.

POP OPEN your EYES



Yeye ni NDUMILA KUWILI hana WASHABIKI CCM wa kumfanya KUWA RAIS; SHABIKI wake MKUBWA CCM in RAIS wa NCHI na NIA yake ni Kwa KUIVURUGA CHADEMA...

ANGALIA AKIANZISHA CHAMA CHAKE UONE - WAPI atapata PESA na WASHABIKI... atakuwa AMEJIUA KISIASA...
SIASA za BONGO sio kama ZA KENYA... KURUKA RUKA na VYAMA kama CHURA
 
yeye saiz anaiona support yakinafik inayotoka ccm anadhan anawashabik . Aangalie sana ataja haibika uyu bro
 
) Wajerumani walipokuwa wakiingia Tanganyika kabla ya Waingereza, walitengeneza urafiki mkubwa sana kati yao na Watanganyika kiasi kwamba Watanganyika wakawaamini na wakawakaribisha. Watanganyika wakaamini kuwa pengine walikuwa tayari wamepata watu ambao wangeweza kusaidiana nao kuyatatua matatizo yao, lakini ikawa kinyume pale Wajerumani walipodhihirisha unafki wa urafiki waliouanzisha na hao Watanganyika. Ninaweza kumfananisha Zitto na hao Wajerumani. Zitto alitumia moyo wake wote na nguvu zake zote kutuaminisha Watanzania kuwa alikuwa na uchungu na Nchi yetu hasa pale alipoamua kupigana na ufisadi na uadui mwingine kati 2005 na 2010. Kumbe hiyo yoye ilikuwa ni mbinu ya yeye mwenyewe kuwa kama Wajerumani.
b) Nikumungalia kutokea upande wa viongozi wa jadi wa Tanganyika wa miaka ile, namfananisha Zitto na Mangungo wa Msovero Usagara Kilosa aliyeishi na kuongoza watu wake miaka iliyopita na hatimaye kuwauza kwa wakoloni. Zitto alikuwa na dhamira ya kuiuza CHADEMA na Wanachadema kwa Wadharimu na Wazandiki wa Taifa letu, CCM akisahau kuwa kati ya 2005 na 2010 baada ya yeye kusimamishwa kuingia bungeni alizunguka Nchi nzima na kusema mengi sana dhidi ya CCM. Nakumbuka moja ya hotuba zake aliyozotoa katika ziara hiyo pale Tukuyu, Wilayani Rungwe, Zitto alisema,"CCM wanataka kutuuza kama Mangungo wa Msovero Usagara alivyo tuuza kwa Wajerumani, wanahistoria watakuwa wanaungana nani katika hili". Akaongezea kwa kusema, "Tuungane pamoja kuwapinga CCM". Sasa sijui alituhamasisha tuungane naye kivipi kama yeye mwenyewe kwa akili zake mwenyewe (to the best of his knowledge) kaamua kuuza Mustabali wa Taifa zima kwa wadharimu na Wazandiki, CCM?:A S angry::A S angry::A S angry:
 
Namshangaa Zito kwa mvutano na mnyukano baina yake na viongozi wa juu! Hivi anajihesabu kuwa mwanachadema? Dr. Slaa alishatangaza kuwa wanachadema wasihudhurie mikutano yake kwa jina la chadema najiuliza huko bungeni atakuwa anakiwakilisha chama gani?
 
Hilo ndo kosa mnalofanya chama hakiwezi kuwa cha mtu mmoja...hata kama akianzisha chama chake itamlazimu kuomba ridhaa ya wanachama.....mi nadhani kwakuwa mwenyekiti Wa ccm ni baba yake na malishasema anataka rais ajaye awe kijana walipokuwa na Zitto Sudan kusini basi ZITTO AHAMIE CCM...Tena uzuri CCM ina wanachama wengi wanaomtaka awe rais atashinda kirais.....
100% Agree ...
 
kama lengo lake ni urais better aanzishe chama chake kwani kwa hali ilivyo hata kuwa balozi wa nyumba kumi hawezi kupitishwa cdm.
 
Zito ni msaliti na masalia na adui mkubwa hafai hata kidogo kwa chama chochote kwani ni mwepesi kununuliwa.jana kaaibika pale mahakamani alivyokuwa anaimbiwa nyimbo za kumg'oa Idi Amin
 
Zitto anahaha saizi ili kujinasua na kufa kisiasa kwa sababu anajua akiwa CCM hawezi kufanya kama alivyofanya CDM akiakimini hawezi kufukuzwa.

Hata roho ikitaka kutoka lazima mtu atapetape sana na ndiyo hatua ya Zitto sasa.
 
Nyani ngabu. Tuambie ni nani unaeona ww anafaa Tanzania hii.
 
Zitto akianzisha chama atajisaliti mwenyewe. ..
 
Naona mnajifariji vijana wa ufipa .... teh teh teh ... hamumuwezi zitto nyie vifaranga . Toka lini akili ndogo ikaiendesha akili kubwa ????
 
Mkuu the Boss, angalau kuna viongozi wengine wa Chadema walishawahi kuwa wanachama wa vyama vingine na ndio maana wengine hata kadi wanatunza kwa kumbukumbu!, lakini ZZK ni "born 'n' breed" in Chadema!. Kwake Chadema is the only party he knows!.

Kwa vile he was born Chadema, he will die Chadema!. Kwetu sisi wengine, ZZK ni Chadema na Chadema ni pamoja na ZZK, bila ZZK hakuna Chadema na bila Chadema hukuna ZZK!.

Nyie mnaemuona ZZK hawafai katika chama chenu, ili kuhalalisha kuwa Chadema kina wenyewe, na ndio maana wale mnao waona kama sio wenyewe ndio mnawataka watoke wakaanzishe vyama vyao ili mbaki wenyewe?!.

Maadam ZZK hajui chama kingine chochote, kwa baadhi yetu ZZK ni miongoni mwa wenye Chadema na mwakani tunamchagiza agombee Uenyekiti ili kuifutilia mbali ile dhana ya nepotisim kwenye top brass!.

Sasa nyinyi mnaemuona hafai, ndio tungewashauri mfungashe virago vyenu au mrejee kwenye vyama vyenu au mkaanzishe vyama vyenu mumsusie ZZK muone jinsi Chadema kitakavyo geuka ni chama cha kitaifa over night!. Mpaka Zanzibar kitafika!.

Naombeni sana tusimsakame ZZK based on taarifa za Saa8, na jee ikitokea ZZK akamkomalia huyo Saa8 aliyemtuma na kumpa ile sumu ya panya, mtasema nini?.

Dalili zote zinaonyesha "kikulacho", Chadema, "kii nguoni mwako!". Ila pia kuna uwezekano mkubwa mkakuta "Umdhaniye ndiye... siye!".
Pasco

Pasco makosa mengine ni sababu ya kutokuhakiki ulichoandika au ni nini? unawezaje ukasema Bila Zitto hakuna Chadema? Kwamba Akiondoka chama kinafutwa?
 
Mkuu The Boss, Wapiganaji shupavu, huwa hawakimbii vita, wanapigana mpaka risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu linamwagika!, hata kama at the end of the day, jeshi lao halitashinda vita, ila watakumbukwa daima kama mashujaa waliofia nchi yao!.

ZZK ni mpiganaji shupavu na atapambana mpka mwisho!. Mimi naamini ya Wangwe ni ajali tuu kama ilivyo ya Mama Mbatia na mi mi pia nilipata ajali eneo hilo hilo ni notorious kwa ajali, tunaoelewa tunaelewa, ikitokea ni ajali, then ni ajali, ila kama ni mkono wa mtu, "hata panya hatapona"!.
Pasco.
Najikumbushia, kila dalili za kuelekea kwenye risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu, zinaonekana!, naendelea kusisitiza, kama hii ndio ilikuwa mipango ya Mungu, aliyompangia Zitto, na iwe kama Mungu alivyopanga!, yaani its his destiny!, lakini kama kuna mkono wa mtu!, mtashuhudia rebutal ya "karma!" itaitafuna Chadema na hakuna mtakaomini kitakachotokea!.

Pasco.
 
Bila kujali kwamba tuhuma za Ben Saanane na wengine ni kweli au sio kweli naona ni busara kwa Zitto now ajitoe CHADEMA na aunde hama chake ambacho yeye atakuwa mwenyekiti na ataweza kukusanya washabiki wake wote waliopo CCM na CHADEMA na kwingineko.

Sioni ni vipi Zitto anaweza kugombea urais kwa kupitia CHADEMA sio tu 2015 lakini mwaka wowote ule.....CHADEMA will never be the party for him to vie for the presidency..hii now iko waazi mno.

Na Zitto lengo lake kuu ni kugombea urais...basi ni bora ajipange now.

Mimi naona this way it is better kwa kila mtuZitto na CHADEMA pia.
Mkuu the Boss, "YOU HAVE THE POWERS!"

Pasco.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom