Ushauri wa bure: Msije Dodoma mnadanganywa sana

Ushauri wa bure: Msije Dodoma mnadanganywa sana

Samahani Dada, kwani kuna sehem nimekuita wewe mshamba..!!??
Na hata kama ulizaliwa na kukulia maili mbili ama chang'ombe, hiyo haimaanishi kwamba miaka yangu miwili haijatosha kuijadili Dom na Dar.
Na bahati mbaya sana ninyi mlio zaliwa huku na kupakimbia enzi za awamu ya nne, ndio hamuijui tena Dodoma kwasababu wageni tumesha iboresha na tunaendelea kuijenga kwa kasi kuliko enzi za matonya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hivi ghalama ya chini kabisa ili kuchimba kisima cha maji ni sh ngapii.?
 
Wewe ni muelezeaji mzuri ila kwenye hii mada narudia kusema hoja zako ni dhaifu sababu unaongelea mambo kwa utashi wako binafsi bila kuwa na hoja, pia unaongelea mambo mengi yasiyowiana na mada husika.

Kwanza nikusahihishe kwamba serikali haihamishi mji, bali inahamisha utendaji wa ofisi kuu za taasisi na mamlaka za serikali kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma.

Unaongelea ROI kwamba ni muhimu kuliko kuhamia Dodoma, ila nitakujulisha Miradi michache iliyofanywa na serikali ambayo imekamilika na mingine ipo kwenye ujenzi , Miradi hiyo yote ina Economic ROI , Social ROI n.k
Miradi hiyo ni kama Train ya mwendokasi, ndege, flyover , Miradi mikubwa ya kuzalisha umeme, uboreshaji wa miundumbino kama Barabara, usafiri wa majini n.k

Serikali ina Sera yake ya Tanzania ya viwanda ambavyo ndio chachu ya maendeleo katika nchi zote, ndio maana imeamua kuboresha miundumbino ya uwekezaji kama nishati na Barabara kama njia ya kuendelea Tanzania ya viwanda huku ikiendelea kutunga Sera mbali mbali za uwekezaji utakaonufaisha nchi.

Hivyo serikali ili iweze kusimamia utekelezaji wa hivyo vyote kwa ufanisi wa Hali ya juu hasa utekelezaji na usimamiaji, ilikuwa lazima kuhamia Dodoma ili kupata muunganiko mzuri wa maendeleo ya nchi, sababu ilikuwa kila Miradi mikubwa kipindi cha nyuma ilikuwa inafanyika mikoa michache kama Dar es salaam, Arusha, Mwanza n.k
Pia kumbuka nilikuambia serikali haiwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja.

Pia nimesema Capital Development Authority - CDA sio hoja ya msingi sababu ilikosa ufanisi na kujaa urasimu jambo lililopelekea kuvunjwa na serikali ya awamu ya tano

Nimekuambia kwamba acha kuruka ruka na maneno kwa kuandika vitu vingi visivyoendana na hoja husika mfano, mambo ya Korosho, export finished products nilikuambia jibu ni moja tu kwamba " serikali haiwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja "

Umesema nikusaidie faida za kuhamia Dodoma
Faida za kuhamia Dodoma ni kama zifuatazo,

1. Nchi itakuwa na muunganiko mzuri wa kimaendeleo kwa mikoa yote kuliko kukalili mikoa michache kama Dar es salaam, Mwanza na Arusha, muunganiko wa nchi ni jambo litakalo shawishi wawekezaji wakubwa kuwekeza sehemu yeyote ya nchi , uwekezaji mfano hotels za kisasa, viwanda , nyumba za kuishi ( apartments ) n.k

2. Itasaidia wanachi mikoa yote kupata huduma za Kiserikali kuu kwa wakati ikizingatiwa dodoma ni kati Kati ya nchi hivyo ni rahisi wanachi wa mikoa yote kufika dodoma kwa mda mfupi

3. Itapelekea kuendelea kwa mikoa mingine ya jirani ya dodoma, mikoa kama singida, Morogoro, manyara n.k

4. Itasaidia usimamiaji na ufuatiliaji wa serikali katika Miradi mbalimbali katika mikoa yote ya nchi, Miradi kama umeme, maji, viwanda, afya n.k pia dodoma ni sehemu sahihi kwa usalama wa nchi ikizingatiwa ni kati Kati ya nchi. N.K

Hoja ya msingi kwangu ni kwamba serikali kuhamia Dodoma ni jambo zuri pia faida ni nyingi kuanzia sasa na miaka mingi ijayo, hivyo faida ni kubwa kuliko gharama iliyotumika, hivyo acha kuwa kama bendera fuata upepo kwa kuandika upotoshaji wa jambo la serikali kuhamisha utendaji wa serikali kuu kutoka dar es salaam kwenda Dodoma
Au unaweza kuelezea ni gharama gani kubwa sana iliyotumika hadi Sasa tangu serikali imehamia dodoma?

achana na hoja zako nyepesi kuelezea eti gharama ni mafuta, nyumba za wafanyakazi na wakati kitendo cha kuhama ni kama mfanyakazi wa kawaida anaamishwa mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine ambapo analipwa stahiki zake kama usafiri na makazi, na ili kupunguza gharama serikali ili wahamisha kwa train na magari ya jeshi, pia hata wakiwa dar es salaam Walikuwa wanalipwa posho za nyumba na mafuta
jambo la ofisi nimekuelezea vizuri namna Yale Majengo ya Wizara yalivyojengwa pale mji wa Kiserikali kwa gharama ndogo sana.

Kuhusu nchi kama Nigeria, India, Brazil, Misri, Mozambique n.k kuhamisha makao makuu ya miji Yao mikuu, hiyo iliwasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji wa serikali zao sababu hizo nchi zote zilitawaliwa hivyo miji mikuu iliwekwa na wakoloni kurahisisha utendaji wa serikali za kikoloni hivyo kuhamisha makao makuu ya nchi zao ilikuwa lazima wahamishe kwenda miji mikuu mingine bila kujali gharama kubwa, pia kwa Tanzania ni hivyo hivyo.

Pia acha kukalili vitabu vilivyoandikwa na watu kama wewe, Hao ni waandishi tu na ni watu kama wewe na pia wanakosea kama wewe, hivyo hizo link za vitabu kama hazina msaada kwenye Sera ya Sasa ya serikali ya Tanzania, basi hivyo vitabu ni useless kwa Sasa ikifika mda vikihitajika na Sera ya nchi tutavitumia

Sent using Jamii Forums mobile app
Umemjibu vizuri sana. Asipokuelewa atakuwa na jambo lake binafsi.
 
Hoja dhaifu kivipi? Mambo yasiyowiana na mada husika yapi?



Serikali haijahamisha mji mkuu wa Tanzania kutoka kuwa Dar na kuwa Dodoma?

Unakataa hili?



Unaweza kueleza ROI ya ndege, kwa mfano tu?



Huwezi kuwa na Tanzania ya viwanda serious kama unaweka kipaumbele kuhamisha mji mkuu wakati huna kiwanda cha kubangulia korosho, zao la kwanza kwa kuleta forex nchini.



Kwani serikali ilishindwa kupeleka miradi ya maendeleo sehemu nyingine bila kuhamisha mji mkuu?



Unaelewa kwamba siongelei kuhamishwa mji mkuu na awamu ya tano, naongelea kuhamishwa kwa mji mkuu? Unajua tofauti?



Kama serikali inaweza kufanya mambo yote kwa wakati mmoja, mbona mpaka leo korosho za Tanzania zinakuwa exported kama raw products? Kwa nini hakuna ubanguaji unaofanywa nchini kabla ya exports?



Kuna lolote kati ya haya ambalo lisingewezekana kufanyika kama mji mkuu usingehamishiwa Dodoma?



Kuna faida gani kuhamishia mji mkuu Dodoma? Mbona hujataja faida yoyote ambayo ilihitaji mji mkuu kuhamishiwa Dodoma?



Umesoma hiyo link niliyokupa? Hayo majengo ya serikali yaliyojengwa Dodoma yamejengwa bila gharama? Safari za kwenda na kurudi Dodoma?



Kuhamisha mji mkuu na shughuli za serikali ni sawa na uhamisho wa kawaida? Do you even believe what you are writing?



Mozambique imehamisha mji mkuu lini? Do you even know what you are writing here?



Tatizo hujui tofauti ya "kukalili" na "kukariri" halafu unataka kubishana na mimi.

Wewe hata Kiswahili tu hujui, unataka kubishana na mimi?
Asili yako ni ubishi na kwa ujinga wako unafikiri unajua kila kitu hapa duniani, pole sana.
Kuna vitu vingi unatakiwa kujifunza katika hii Dunia kuliko unavyovifahamu wewe,

Serikali imehamia Dodoma ni jambo zuri na kubwa la kupongezwa sana na uongozi uliofanya hivyo.

Kuanzia sasa
Dodoma - mji wa Kiserikali
Dar es salaam - mji wa kibiashara
Arusha - utalii na diplomasia
Mwanza - madini na uvuvi
Mbeya - biashara na kilimo n.k



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asili yako ni ubishi na kwa ujinga wako unafikiri unajua kila kitu hapa duniani, pole sana.
Kuna vitu vingi unatakiwa kujifunza katika hii Dunia kuliko unavyovifahamu wewe,

Serikali imehamia Dodoma ni jambo zuri na kubwa la kupongezwa sana na uongozi uliofanya hivyo.

Kuanzia sasa
Dodoma - mji wa Kiserikali
Dar es salaam - mji wa kibiashara
Arusha - utalii na diplomasia
Mwanza - madini na uvuvi
Mbeya - biashara na kilimo n.k



Sent using Jamii Forums mobile app
Hujui unachoandika. Ndiyo maana umeandika Mozambique ni kati ya nchi zilizohamisha capital cities.

Nimekuuliza lini?

Umeruka swali. Hujajibu.
 
Akili yako unaijua wewe mwenyewe. kwani ni bonge la mvivu.

Mwenye akili akishagundua kuna fulsa au kuna watu wavivu ni nafasi nzuri ya kuanzisha uwekezaji au biashara.

Lakini wewe unabaki unabwabwaja tu.

Fulsa hiyo ndugu.

Dodoma sio Dsm maneno maneno na vijiwe vya kahawa na kupiga soga.
 
Hujui unachoandika. Ndiyo maana umeandika Mozambique ni kati ya nchi zilizohamisha capital cities.

Nimekuuliza lini?

Umeruka swali. Hujajibu.
Hoja zako bado dhaifu sana ndugu, Kuna mambo mengi unatakiwa ujifunze.

Katika hilo jambo nimeelezea nchi zifuatazo zilihamisha utendaji wa serikali zao kuu kutoka mji mmoja kwenda mwingine pia nitaongezea nchi chache mfano

Brazil : Rio de Janeiro to Brasilia,
Nigeria : Lagos to Abuja,
Misri : Cairo to new Cairo,
India: Delhi to new Delhi,
Mozambique : Maputo to new Maputo,
Australia : Melbourne and Sydney to Canberra ,
USA : New York, Philadelphia and Baltimore to Washington DC
Hata kama Mozambique hawajahamisha serikali yote kwenda new Maputo lakini bado Kuna new Maputo na old Maputo.

Inakuaje unaanza kusimamia hoja ndogo Kabisa ya Mozambique na kuacha mambo ya msingi niliyoelezea kabla?
Ndio maana nakuambia Kuna mambo mengi unatakiwa kujifunza, ila kwa ujinga wako unazani unajua kila kitu hapa duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hivi ghalama ya chini kabisa ili kuchimba kisima cha maji ni sh ngapii.?
Sina uzowefu na uchimbaji wa visima mkuu, minatumia maji toka kwenye miundombinu ya Duwasa.
Lakini ukipitia humu kuna nyuzi za makampuni yanayo jishugulisha na uchimbaji wa visima.
Ama ukielekea Dar road kama umbali wa kilometers 25 kutoka mjini Dom kuna kampuni naona inajishughulisha na uchimbaji wa visima na wana yard yao pale baada ya Mtumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja zako bado dhaifu sana ndugu, Kuna mambo mengi unatakiwa ujifunze.

Katika hilo jambo nimeelezea nchi zifuatazo zilihamisha utendaji wa serikali zao kuu kutoka mji mmoja kwenda mwingine pia nitaongezea nchi chache mfano

Brazil : Rio de Janeiro to Brasilia,
Nigeria : Lagos to Abuja,
Misri : Cairo to new Cairo,
India: Delhi to new Delhi,
Mozambique : Maputo to new Maputo,
Australia : Melbourne and Sydney to Canberra ,
USA : New York, Philadelphia and Baltimore to Washington DC
Hata kama Mozambique hawajahamisha serikali yote kwenda new Maputo lakini bado Kuna new Maputo na old Maputo.

Inakuaje unaanza kusimamia hoja ndogo Kabisa ya Mozambique na kuacha mambo ya msingi niliyoelezea kabla?
Ndio maana nakuambia Kuna mambo mengi unatakiwa kujifunza, ila kwa ujinga wako unazani unajua kila kitu hapa duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
New Maputo ni mji gani huo? Hata kwenye ramani haupo.

Hahaaaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe usitake kujipenyeza uje uniombe hela.

Umechelewa, nimemaliza bajeti ya kutoa misaada ya mwaka huu.
Ngosha unajihami sana!
Nimecheka mpaka nimeshangaza nzengo hapa,nakuja pm wallah!
Sikuombi pesa mingi Mimi kiduchu tu ulizobakiza bakiza kwenye mfuko wa nyuma wa sarawili.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, swala zima la uhamisho na kumuacha mwenza ni janga.
Na hapa ndipo huwa pagumu sana kwetu sisi wana ndoa, hata hufikia wengine kuamua mmoja kuacha kazi ili abaki na familia.
Uhamisho penginge huu ndio wakati mgumu kukiko kipindi chote kwa wana ndoa kwamba uchaguwe kazi ama uchaguwe ndoa..??
Hivyo nirudie tu kusema kwamba Dodoma haina mahusiano na kuyumba kwa ndoa yako mkuu


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo unataka kuniambia ndoa yangu haijayumbishwa na serikali kuhamia dodoma utamu wa ngoma ingia kati uucheze cc ushimen
 
Sasa kama hakuna maslahi wala mzunguko kwann frem ndogo ni ghali? Si kwamba inatakiwa sehemu ambapo hakuna biashara frem ndo iwe rahisi?
 
kama ipi itaje
kuna mikoa kama DSM/Mwanza/Morogoro...kilichosaidia kuchangamsha wenyeji ni WAGENI kutoka kila pahala Tanzania..naamini hata Dodoma itakuja changamkaaa

Angalia mikoa/miji waliyopingana na wageni ka imebadilika? ipo vile vile...kuanzia January hadi December...1990's adi 2010's haibadiliki
 
Mimi Niko Dom na huwa nakuja Mara kwa Mara ....


Asilimia 70 ya miradi ya Ujenzi hapa Ni ya serikali na sio watu binafsi ... Hizi programs zikiisha Dom itakuwa dormant... Kuna sababu nyingi kwanini dom itasinyaa na zipo wazi labda ujifanye kipofu



Dom haina shughuli nyingi za kiuchumi Kama Mbeya , kahama , mwanza au Arusha ... Huu Ni ukweli mchungu ...


Kinachowavuta watu sehemu ni shughuli za kiuchumi (uvuvi, UFUGAJI, ukulima , madini, usafirishaji n.k))... Hivi vyote Dodoma vipo kwa kiasi kidogo au Hakuna kabisa ....


Kwasasa watu ni Kama wamerusha shilingi ndio maana unaona watu wengi Dodoma ila nakwambia miradi yote ikikamili na mji ukianza kuwa kwenye "Acceleration" hakuna mji utakao kuwa wa hovyo Kama Dom ... Utakuwa Ni mji mzuri ila wa kuspend na sio kutafuta maisha Kama wengi wanavyodhani.







Sent using Jamii Forums mobile app
Good point.. kinachofanya dodoma inaonekana ku shine ni hiyo miradi ya serikali.. watu wanasahau mji unachangamshwa na shughuli za watu binafsi na sio serikali.
 
Back
Top Bottom