Ushauri wa bure: Msije Dodoma mnadanganywa sana

Ushauri wa bure: Msije Dodoma mnadanganywa sana

Hili ndilo kosa ambalo watu wengi wanalifanya. Ukweli naona watu hapa wanajaribu kuilinganisha Dom na Dar, lakini wanasahau kwamba ili Dom ije ifananishwe na Dar inatakiwa juhudi zifanyike kwa walau miaka mingi kidogo mbeleni.
By the way, hata Dar mpaka inafikia hapo ilipo kwanza ilijengwa kwa miaka mingi na vivyo hivyo itakavyo kuwa Dodoma in ten years to come

Sent using Jamii Forums mobile app
na ukweli ni huu, DODOMA inabadilika kwa kasi ,tatizo ni kuwa ukiingalia kwa jicho la Dar,Mwanza au Mbeya haya mabadiliko hutayaona ...tunaijua Dodoma Ya kabla ya UDOM,na maamuzi ya JPM ya Mwaka 2017 Dodoma inakua kwa kasi!
 
Wajapan walianzisha nursery pale maili mbili, SNV ilianzisha kitengo cha miti huko huko maili mbili na kupanda miti Dodoma nzima kwenye mradi wa DOVAP. hivyo vyote vilitoweka sababu ya siasa zetu za kuchagua kipi kwanza. Wafadhili walipoondoka wakaondoka na kila kitu sis tupo tu. Dodoma inahitaji kupandwa miti nyingi na itasaidia hata mvua kuongezeka. Mimi kama mwenyeji wa Dodoma nimejitahidi kupanda miti ya kidumu kibao na nina kisima ambacho natumia kumwagllia maji. Karibuni Idodomya jamani.
Tunashauri Kuwe Basi hata na political move na uhamasishaji wa upandaji miti kila mwaka .... hasa kipindi hiki ambapo angalau mvua zinanyesha. Niliona Kilimanjaro walikuwa na activity ya upandaji miti million 3 katika kukabiliana na kuyeyuka kwa barafu ya mlima Kilimanjaro. Kwa Dodoma Kama Makao Makuu ..... wananchi tupo tayari kushiriki iwapo kutakuwa na movement Kama hii. Ni kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo. Karibuni sana Idodomya😀
 
Jirani, huyu jamaa nimegundua haijui Dodoma zaidi ya kusimuliwa na kufuata mkumbo.
Maana kama maji yapo hadi Ndachi, iweje mji mkongwe kama Nkuhungu ukose maji..!!??

Sent using Jamii Forums mobile app
Jirani.... Huyo amehadithiwa Dodoma ya zamani sio ya sasa. Maji yapo..... sikumbuki Ni lini nimehangaika kununua maji kuwa maji hayatoki bombani. Mambo ya Makao Makuu haya.... Yamenoga.😀
 
Jirani.... Huyo amehadithiwa Dodoma ya zamani sio ya sasa. Maji yapo..... sikumbuki Ni lini nimehangaika kununua maji kuwa maji hayatoki bombani. Mambo ya Makao Makuu haya.... Yamenoga.[emoji3]
Haya jirani, basi natuanze kupanda miti ili kuifanya Dodoma ya kijani.
Mimi tayari hapa Area-C nina miti kama minne nyumbani na imekuwa mikubwa. Na kule nala, tayari nimepanda miti zaidi ya 10 na inaendelea kukuwa.
Hawa acha ajifanye hawaoni, lakini baada ya miaka michache ijayo watakuja kuijutia kutowekeza Dodoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, kwa Dodoma mjini hakuna eneo ambalo halipati maji kwasababu chanzo cha maji tunayo yapata Dodoma nzima hatujaweza kuyatumia hata kwa asilimia hamsini.
Sehem ambayo haina maji Dodoma ni pale tu ambapo Duwasa haija fikisha miundombinu kwaajili ya kusambaza maji

Sent using Jamii Forums mobile app
Kijana nimeishi Dodoma zaidi yako ... Wewe kuwa na miaka miwili Dom usituone wengine ni washamba wa Dom.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijana nimeishi Dodoma zaidi yako ... Wewe kuwa na miaka miwili Dom usituone wengine ni washamba wa Dom.

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani Dada, kwani kuna sehem nimekuita wewe mshamba..!!??
Na hata kama ulizaliwa na kukulia maili mbili ama chang'ombe, hiyo haimaanishi kwamba miaka yangu miwili haijatosha kuijadili Dom na Dar.
Na bahati mbaya sana ninyi mlio zaliwa huku na kupakimbia enzi za awamu ya nne, ndio hamuijui tena Dodoma kwasababu wageni tumesha iboresha na tunaendelea kuijenga kwa kasi kuliko enzi za matonya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo nikikujibu popote, una uwezo wa kuliona jibu? Utaelewa ninachoandika?

Sijakujibu na kukuambia serikali itangulize vitu vyenye Return On Investment kabla ya kufanya straight up expenditures kama kuhamisha mji?

Unaelewa hilo maana yake nini? Unaelewa Return On Investment ni nini?

Kama huelewi, kwa nini huulizi ueleweshe? Kama unaelewa, kwa nini unaandika sijakujibu?

CDA inakosaje kuwa sehemu ya msingi wa hoja wakati ni mamlaka iliyoanzishwa kuhamisha mji kwenda Dodoma, ikashindwa? Inakosaje kuwa sehemu ya msingi wa hoja wakati inaonesha incompetency ya serikali?

Unasemaje si msingi wa hoja?

Sasa unataka niweke laundry list ya miradi badala ya kuongelea main ideas hapa? Nimeongelea ujinga wa serikali kuingilia biashara ya korosho, saidia wakulima waweze ku add value kwenye korosho waongeze exports na revenue. Tumia hela chache kuwatengenezea miundombinu na kuwezesha wafanyabiashara wajenge viwanda vya kubangua korosho, tu export finished products badala ya raw materials. This is a basic example of how the government has wrong priorities.

Una export raw korosho, huna kiwanda cha kubangua korosho cha kueleweka, halafu unahamisha mji mkuu.

Ni kama vile watoto wanakufa kwa njaa hawana chakula, baba unaenda bar kulewa!

Unafananisha chumi za Nigeria, Misri na Brazil na uchumi wa Tanzania? Umeangalia hata GDPs tu za hizo nchi?

Nchi zote ulizozitaja hazipo katika level ya GDP ya Tanzania. Umasikini wetu hauturuhusu kufanya mradi wa luxury kama kuhamisha mji mkuu. Nigeria wametumia petrodollars kuhamisha mji mku. Walivyotaka kuhamisha walikuja kuchukua uzoefu kwetu. Matokeo yake, waliokuja kujifunza kwetu wamemaliza kuhamisha mji mkuu, sisi hatujamaliza. Kwa sababu hatuna hela, hatuna commitments.

Kuhamisha mji mkuu ni expenditure. Nchi masikini zina demands nyingi sana kwenye forex zake. Zinatakiwa kuwa makini kutumia forex kwenye miradi yenye

Hapa unaonesha uvivu wa kujenga hoja tu, unasema kitu, halafu unashindwa kukitetea.

Faida ya kuhamia Dodoma ni ipi ambayo isingeweza kupatikana kama mji mkuu usingehamishiwa Dodoma?

Again, unaonesha uvivu wa kujenga hoja. Nilitegemea uorodheshe faida ni hii na hii na hii.

Hujaorodhesha. Hata wewe mwenyewe unazijua hizo faida au unasema zipo bila kuzijua tu?

Hoja ukiiona utaijua? CDA mismanangement itakosaje kuwa hoja katika mjadala wa kuhamia Dodoma? Serikali isiyo na mkakati kwenye biashara ya korosho lakini inayoweka kipaumbele kuhamia Dodoma itakosaje kuwa hoja?

Kuanguka kwa exports za agriculture kwa sababu serikali haina mkakati wa ku add value kwenye agricultural products wakati serikali ina prioritize kuhamisha mji mkuu kutakosaje kuwa hoja?Nchi yenye watu wasio na social benefits za kueleweka, halafu manakimbilia kuhamisha mji mkuu itakosaje kuwa hoja kuonesha misplaced priorities?

Msingi wa hoja ni nini? Unaweza ku define msingi wa hoja?

Hilo Bunge limejengwa kwa hewa? Ofisi za serikali? Nyumba za wafanyakazi wa serikali? Mafuta ya kupeleka watu Dodoma na kurudi Dar

Soma wataalam wameandika hapa "Poverty stricken Tanzania, unlike Nigeria, cannot throw hundreds of millions of pounds at the scheme and it will take some time to develop".

Bado unasema hakuna gharama?

Wewe ni muelezeaji mzuri ila kwenye hii mada narudia kusema hoja zako ni dhaifu sababu unaongelea mambo kwa utashi wako binafsi bila kuwa na hoja, pia unaongelea mambo mengi yasiyowiana na mada husika.

Kwanza nikusahihishe kwamba serikali haihamishi mji, bali inahamisha utendaji wa ofisi kuu za taasisi na mamlaka za serikali kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma.

Unaongelea ROI kwamba ni muhimu kuliko kuhamia Dodoma, ila nitakujulisha Miradi michache iliyofanywa na serikali ambayo imekamilika na mingine ipo kwenye ujenzi , Miradi hiyo yote ina Economic ROI , Social ROI n.k
Miradi hiyo ni kama Train ya mwendokasi, ndege, flyover , Miradi mikubwa ya kuzalisha umeme, uboreshaji wa miundumbino kama Barabara, usafiri wa majini n.k

Serikali ina Sera yake ya Tanzania ya viwanda ambavyo ndio chachu ya maendeleo katika nchi zote, ndio maana imeamua kuboresha miundumbino ya uwekezaji kama nishati na Barabara kama njia ya kuendelea Tanzania ya viwanda huku ikiendelea kutunga Sera mbali mbali za uwekezaji utakaonufaisha nchi.

Hivyo serikali ili iweze kusimamia utekelezaji wa hivyo vyote kwa ufanisi wa Hali ya juu hasa utekelezaji na usimamiaji, ilikuwa lazima kuhamia Dodoma ili kupata muunganiko mzuri wa maendeleo ya nchi, sababu ilikuwa kila Miradi mikubwa kipindi cha nyuma ilikuwa inafanyika mikoa michache kama Dar es salaam, Arusha, Mwanza n.k
Pia kumbuka nilikuambia serikali haiwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja.

Pia nimesema Capital Development Authority - CDA sio hoja ya msingi sababu ilikosa ufanisi na kujaa urasimu jambo lililopelekea kuvunjwa na serikali ya awamu ya tano

Nimekuambia kwamba acha kuruka ruka na maneno kwa kuandika vitu vingi visivyoendana na hoja husika mfano, mambo ya Korosho, export finished products nilikuambia jibu ni moja tu kwamba " serikali haiwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja "

Umesema nikusaidie faida za kuhamia Dodoma
Faida za kuhamia Dodoma ni kama zifuatazo,

1. Nchi itakuwa na muunganiko mzuri wa kimaendeleo kwa mikoa yote kuliko kukalili mikoa michache kama Dar es salaam, Mwanza na Arusha, muunganiko wa nchi ni jambo litakalo shawishi wawekezaji wakubwa kuwekeza sehemu yeyote ya nchi , uwekezaji mfano hotels za kisasa, viwanda , nyumba za kuishi ( apartments ) n.k

2. Itasaidia wanachi mikoa yote kupata huduma za Kiserikali kuu kwa wakati ikizingatiwa dodoma ni kati Kati ya nchi hivyo ni rahisi wanachi wa mikoa yote kufika dodoma kwa mda mfupi

3. Itapelekea kuendelea kwa mikoa mingine ya jirani ya dodoma, mikoa kama singida, Morogoro, manyara n.k

4. Itasaidia usimamiaji na ufuatiliaji wa serikali katika Miradi mbalimbali katika mikoa yote ya nchi, Miradi kama umeme, maji, viwanda, afya n.k pia dodoma ni sehemu sahihi kwa usalama wa nchi ikizingatiwa ni kati Kati ya nchi. N.K

Hoja ya msingi kwangu ni kwamba serikali kuhamia Dodoma ni jambo zuri pia faida ni nyingi kuanzia sasa na miaka mingi ijayo, hivyo faida ni kubwa kuliko gharama iliyotumika, hivyo acha kuwa kama bendera fuata upepo kwa kuandika upotoshaji wa jambo la serikali kuhamisha utendaji wa serikali kuu kutoka dar es salaam kwenda Dodoma
Au unaweza kuelezea ni gharama gani kubwa sana iliyotumika hadi Sasa tangu serikali imehamia dodoma?

achana na hoja zako nyepesi kuelezea eti gharama ni mafuta, nyumba za wafanyakazi na wakati kitendo cha kuhama ni kama mfanyakazi wa kawaida anaamishwa mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine ambapo analipwa stahiki zake kama usafiri na makazi, na ili kupunguza gharama serikali ili wahamisha kwa train na magari ya jeshi, pia hata wakiwa dar es salaam Walikuwa wanalipwa posho za nyumba na mafuta
jambo la ofisi nimekuelezea vizuri namna Yale Majengo ya Wizara yalivyojengwa pale mji wa Kiserikali kwa gharama ndogo sana.

Kuhusu nchi kama Nigeria, India, Brazil, Misri, Mozambique n.k kuhamisha makao makuu ya miji Yao mikuu, hiyo iliwasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji wa serikali zao sababu hizo nchi zote zilitawaliwa hivyo miji mikuu iliwekwa na wakoloni kurahisisha utendaji wa serikali za kikoloni hivyo kuhamisha makao makuu ya nchi zao ilikuwa lazima wahamishe kwenda miji mikuu mingine bila kujali gharama kubwa, pia kwa Tanzania ni hivyo hivyo.

Pia acha kukalili vitabu vilivyoandikwa na watu kama wewe, Hao ni waandishi tu na ni watu kama wewe na pia wanakosea kama wewe, hivyo hizo link za vitabu kama hazina msaada kwenye Sera ya Sasa ya serikali ya Tanzania, basi hivyo vitabu ni useless kwa Sasa ikifika mda vikihitajika na Sera ya nchi tutavitumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni muelezeaji mzuri ila kwenye hii mada narudia kusema hoja zako ni dhaifu sababu unaongelea mambo kwa utashi wako binafsi bila kuwa na hoja, pia unaongelea mambo mengi yasiyowiana na mada husika.

Hoja dhaifu kivipi? Mambo yasiyowiana na mada husika yapi?

Kwanza nikusahihishe kwamba serikali haihamishi mji, bali inahamisha utendaji wa ofisi kuu za taasisi na mamlaka za serikali kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma.

Serikali haijahamisha mji mkuu wa Tanzania kutoka kuwa Dar na kuwa Dodoma?

Unakataa hili?

Unaongelea ROI kwamba ni muhimu kuliko kuhamia Dodoma, ila nitakujulisha Miradi michache iliyofanywa na serikali ambayo imekamilika na mingine ipo kwenye ujenzi , Miradi hiyo yote ina Economic ROI , Social ROI n.k
Miradi hiyo ni kama Train ya mwendokasi, ndege, flyover , Miradi mikubwa ya kuzalisha umeme, uboreshaji wa miundumbino kama Barabara, usafiri wa majini n.k

Unaweza kueleza ROI ya ndege, kwa mfano tu?

Serikali ina Sera yake ya Tanzania ya viwanda ambavyo ndio chachu ya maendeleo katika nchi zote, ndio maana imeamua kuboresha miundumbino ya uwekezaji kama nishati na Barabara kama njia ya kuendelea Tanzania ya viwanda huku ikiendelea kutunga Sera mbali mbali za uwekezaji utakaonufaisha nchi.

Huwezi kuwa na Tanzania ya viwanda serious kama unaweka kipaumbele kuhamisha mji mkuu wakati huna kiwanda cha kubangulia korosho, zao la kwanza kwa kuleta forex nchini.

Hivyo serikali ili iweze kusimamia utekelezaji wa hivyo vyote kwa ufanisi wa Hali ya juu hasa utekelezaji na usimamiaji, ilikuwa lazima kuhamia Dodoma ili kupata muunganiko mzuri wa maendeleo ya nchi, sababu ilikuwa kila Miradi mikubwa kipindi cha nyuma ilikuwa inafanyika mikoa michache kama Dar es salaam, Arusha, Mwanza n.k
Pia kumbuka nilikuambia serikali haiwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja.

Kwani serikali ilishindwa kupeleka miradi ya maendeleo sehemu nyingine bila kuhamisha mji mkuu?

Pia nimesema Capital Development Authority - CDA sio hoja ya msingi sababu ilikosa ufanisi na kujaa urasimu jambo lililopelekea kuvunjwa na serikali ya awamu ya tano

Unaelewa kwamba siongelei kuhamishwa mji mkuu na awamu ya tano, naongelea kuhamishwa kwa mji mkuu? Unajua tofauti?

Nimekuambia kwamba acha kuruka ruka na maneno kwa kuandika vitu vingi visivyoendana na hoja husika mfano, mambo ya Korosho, export finished products nilikuambia jibu ni moja tu kwamba " serikali haiwezi kufanya mambo yote kwa wakati mmoja "

Kama serikali inaweza kufanya mambo yote kwa wakati mmoja, mbona mpaka leo korosho za Tanzania zinakuwa exported kama raw products? Kwa nini hakuna ubanguaji unaofanywa nchini kabla ya exports?

Umesema nikusaidie faida za kuhamia Dodoma
Faida za kuhamia Dodoma ni kama zifuatazo,

1. Nchi itakuwa na muunganiko mzuri wa kimaendeleo kwa mikoa yote kuliko kukalili mikoa michache kama Dar es salaam, Mwanza na Arusha, muunganiko wa nchi ni jambo litakalo shawishi wawekezaji wakubwa kuwekeza sehemu yeyote ya nchi , uwekezaji mfano hotels za kisasa, viwanda , nyumba za kuishi ( apartments ) n.k

2. Itasaidia wanachi mikoa yote kupata huduma za Kiserikali kuu kwa wakati ikizingatiwa dodoma ni kati Kati ya nchi hivyo ni rahisi wanachi wa mikoa yote kufika dodoma kwa mda mfupi

3. Itapelekea kuendelea kwa mikoa mingine ya jirani ya dodoma, mikoa kama singida, Morogoro, manyara n.k

4. Itasaidia usimamiaji na ufuatiliaji wa serikali katika Miradi mbalimbali katika mikoa yote ya nchi, Miradi kama umeme, maji, viwanda, afya n.k pia dodoma ni sehemu sahihi kwa usalama wa nchi ikizingatiwa ni kati Kati ya nchi. N.K

Kuna lolote kati ya haya ambalo lisingewezekana kufanyika kama mji mkuu usingehamishiwa Dodoma?

Hoja ya msingi kwangu ni kwamba serikali kuhamia Dodoma ni jambo zuri pia faida ni nyingi kuanzia sasa na miaka mingi ijayo, hivyo faida ni kubwa kuliko gharama iliyotumika, hivyo acha kuwa kama bendera fuata upepo kwa kuandika upotoshaji wa jambo la serikali kuhamisha utendaji wa serikali kuu kutoka dar es salaam kwenda Dodoma

Kuna faida gani kuhamishia mji mkuu Dodoma? Mbona hujataja faida yoyote ambayo ilihitaji mji mkuu kuhamishiwa Dodoma?

Au unaweza kuelezea ni gharama gani kubwa sana iliyotumika hadi Sasa tangu serikali imehamia dodoma?

Umesoma hiyo link niliyokupa? Hayo majengo ya serikali yaliyojengwa Dodoma yamejengwa bila gharama? Safari za kwenda na kurudi Dodoma?

achana na hoja zako nyepesi kuelezea eti gharama ni mafuta, nyumba za wafanyakazi na wakati kitendo cha kuhama ni kama mfanyakazi wa kawaida anaamishwa mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine ambapo analipwa stahiki zake kama usafiri na makazi, na ili kupunguza gharama serikali ili wahamisha kwa train na magari ya jeshi, pia hata wakiwa dar es salaam Walikuwa wanalipwa posho za nyumba na mafuta
jambo la ofisi nimekuelezea vizuri namna Yale Majengo ya Wizara yalivyojengwa pale mji wa Kiserikali kwa gharama ndogo sana.

Kuhamisha mji mkuu na shughuli za serikali ni sawa na uhamisho wa kawaida? Do you even believe what you are writing?

Kuhusu nchi kama Nigeria, India, Brazil, Misri, Mozambique n.k kuhamisha makao makuu ya miji Yao mikuu, hiyo iliwasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji wa serikali zao sababu hizo nchi zote zilitawaliwa hivyo miji mikuu iliwekwa na wakoloni kurahisisha utendaji wa serikali za kikoloni hivyo kuhamisha makao makuu ya nchi zao ilikuwa lazima wahamishe kwenda miji mikuu mingine bila kujali gharama kubwa, pia kwa Tanzania ni hivyo hivyo.

Mozambique imehamisha mji mkuu lini? Do you even know what you are writing here?

Pia acha kukalili vitabu vilivyoandikwa na watu kama wewe, Hao ni waandishi tu na ni watu kama wewe na pia wanakosea kama wewe, hivyo hizo link za vitabu kama hazina msaada kwenye Sera ya Sasa ya serikali ya Tanzania, basi hivyo vitabu ni useless kwa Sasa ikifika mda vikihitajika na Sera ya nchi tutavitumia

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo hujui tofauti ya "kukalili" na "kukariri" halafu unataka kubishana na mimi.

Wewe hata Kiswahili tu hujui, unataka kubishana na mimi?
 
Back
Top Bottom