Ushauri wa bure: Msije Dodoma mnadanganywa sana

Ushauri wa bure: Msije Dodoma mnadanganywa sana

Mayala B

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2019
Posts
2,353
Reaction score
5,723
Aman itamalaki kwenu

Leo nimejitolea kutoa ushauri wa bure kabisa bila malipo. Toka Rais atangaze Dodoma kuwa makao makuu ya nchi watu wengi wamekuwa wakidhani kuwa Dodoma mambo ni shwari sana. Ukweli ni kwamba Dodoma mambo ni magumu sana hakuna mzunguko wa pesa wala nini.

Ni pakame sana na pana watu wavivu sana wasio penda kazi. Kwa hiyo basi ndugu zangu msije Dodoma. Kuna watu wengi sana wanakuwa wanatoka mikoa yao na kuja Dodoma wakidhani kuna maisha mazuri na maisha ni magumu sana

Hakuna pesa wala nini. Kwanza flame bei juu na hakuna pesa kabisa

Shauri yenu
 
Kuna jamaa walijidanganya wakapeleka tipa za mchanga huko, walipigika na maisha hadi wakaamua kurudi, Dodoma kuna michongo kweli kwa sasa lakini sio kama inavyosimuliwa mitandaoni. Kiufupi ni overrated
 
Kwanza mvua ya vumbi. Yaani upepo unavuma ukiambatana na vumbi ndo maana jamii ya kule macho yao yamepofuka. So take care vipofu wataongezeka huko.

Maji ni kama yana chumvi, nashangaa mtu mmoja kuamlia nchi kuhamia Dodoma. Nyerere alitaka makao makuu ya nchi yahamie kwasababu kipindi kile miundombinu kama barabara na mawasiliano ya simu, internet havikuwepo sasa hivi mawasiliano yapo, barabara nii rami, mitandao ipo so, hakukuwa na ulazima tena wa Dodoma kuifanya iwe makao makuu badala yake limetengenezwa tatizo tena, watu wanajirundika huko huku huduma muhimu kama maji safi, nyumba nzuri huduma nyinginezo zikiwa za shida. Kwanini mtu ujitengenezee shida na muda wa kuishi ni kidogo??
 
Andika tena ili ueleweke inaonekana hujui hata maana ya kukutana pesa na huelewi kabisa maana na sababu za mzunguko wa pesa.
Utakuwa mongoni mwa washauri hatari na wakurupukaji sana.
Ulichokiandika kinaonekana kama vumbi lenye funza.
 
Hahaha kwani wewe ulienda kufanya shughuli gani..au ulienda kutembea..Sasa jomba watu wanahangaika kuchapa kazi we unafanya utani..wewe umeenda Dodoma unataka ubaki peke yako upige hela jomba,, tumekuelewa..hizo no propaganda mfu
 
kuna mikoa kama DSM/Mwanza/Morogoro...kilichosaidia kuchangamsha wenyeji ni WAGENI kutoka kila pahala Tanzania..naamini hata Dodoma itakuja changamkaaa

Angalia mikoa/miji waliyopingana na wageni ka imebadilika? ipo vile vile...kuanzia January hadi December...1990's adi 2010's haibadiliki
 
Back
Top Bottom