matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,587
- 15,373
Eti popoUsiku nawaachia popo wacha nitembee asubuhi,mchana,jioni!
Ma kuna wengine wako na magogo au mawe njiani..usiku raha ,shida kuna wengine giza likiingia hawaon vizuri
Huo unaousema ni mwendo wa kawaida sana siku hizi nadhani kipindi cha mzee wa msonga ungekuwa umechunguza ungelog off magari mwanza to Dar ilikuwa saa mbili zimechelewa ngoma tatuKuhusu speed aisee Kwenye haya Mabus niliyopanda hamna nilikaa mbele karibu na Dereva nimeona jamaa anapiga Hadi speed 127 km/h.....kama ujuavyo bus likiwa speed hiyo ni balaa yaani Ngoma inatembea balaa Hadi Mwanza nyegezi tumeingia saa 4:48 usiku
Aisee haya uliyoyasema uwa nayazingatia sana. Uwasha indicator ya kulia kuonyesha mwisho wa gari langu. Pia uwasha high beam tokea mbali ili kuwasiliana na dereva anayekuja.Kusafiri usiku siyo mbaya ila ni vizuri njia uwe unaipita mara kwa mara hivyo ni mzoefu wa njia hiyo vile vile taa zako ziwe na mwanga wa kutosha ili kuona mbali zaidi.
Kwa upande wa magari makubwa changamoto si nyingi kikubwa uwe unajuwa njia za mawasiliano na dereva mwenzio wa kutumia taa. Idereva w tahadhari unapopishana na magari makubwa na mara nyingi huwa wanatembea kwa kufatana hivuo tumia taa zako ukiwa mbali kidogo kuwasiliana na dereva unaepishana nae na ni lazima atakujibu tu hapo unaanza kujuwa kuwa ninaepishana nae yuko macho maana wengine huendesha wakiwa nusu macho nusu wako usingizini.
Indicate mwisho wa gari yako nae atafanya hivyo hapo unakuwa salama kupishana na ni vizuri ukipishana nae/nao ukiwa na speed 60km/h au chini ya hapo.
Tukafika maeneo ya tabora nadhani igunga sijui mida ya saa 5 usiku, kitu kimewaka moto.
Hamadi kuna lorry kama mita 50 limezima kati ya barabara na halijaweka alama yeyote. Uzoefu wa dereva ulituokoa lasivyo tusingekuwa duniani leo.
Hata maeneo ya Same wapo wa aina hiyo.Hivyo huwa vinaitwa vicheche...
Sasa kuna hao wa malori na kuna wale wapumbavu wanaowahi na matrekta alfajiri kuanzia saa tisa kwenda kulima, na huwa hayana taa wala refleta yale...
Ushawasha mashine inacheza 170-180kph, anatokea kiazi mmoja na Powertila lake porini huko analiingiza barabarani kama mbwa anayevuka barabara...
Hawa wapo sana maeneo ya Iringa hadi Igurusi kwa barabara ya Tan-Zam, au maeneo ya Singida hadi Nzega kwa barabara ya kati...
usiku raha ,shida kuna wengine giza likiingia hawaon vizuri
Kweli kabisa, Usiku ni balaa. Huyu jamaa hii mada sijui anatafuta kuungwa mkono?Safari za usiku nzuri hujapatwa na janga kama breakdown nk
Nilikuwa nikisafiri usiku, siku moja porini kabisa hakuna watu bearing za nyuma zika jam. Sijawahi safiri tena usiku.
Pia niliwahi nusurika maeneo ya dakawa kupigwa na roli, nalipisha linajaa tu kwangu kesha vuka mstari wa kati unaotenganisha barabara.
Lakini pia usiku usisafiri kama gari yako haina beam ya kutosha taa za mbele. Barabara zetu ni mbovu sana hata za lami. Kukuta shimo katikati ya barabara ni kawaida sana
Mwaka 2013, baada ya kuvuka sekenke kutafuta vijiji vinavyofuata, almanusura na ingekuwa usiku pale na gari haina taa zenye mwanga, leo ningekuwa nishaihama Dunia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa, nimewahi kutoa ushauri humu kwamba, ukiona kuna ulazima wa kusafiri usiku basi hakikisha unawasha taa kubwa zote na mwendo usizidi 50km kwa saa. Nimewahi kufanya hizi safari mara mbili si kwa kupenda. Moja nikiwa peke yangu na nyingine nikiwa na familia yangu. Yaani ajali ni nje nje. Hii spidi 50km kwa saa ilinisaidia kusima ghafla pia ilinisaidia kwenda nje ya barabara pindi malori yaapotanua barabara yote.Nakumbuka kuna siku tulikuwa tunawahi harusi kesho yake. Tukatoka Mwanza saa 12 jioni ili tuingie Dar saa 2 au 3 asubuhi.
Kwenye gari kila mtu alilala, tukabaki mi na dereva tu tunapiga story.
Tukafika maeneo ya tabora nadhani igunga sijui mida ya saa 5 usiku, kitu kimewaka moto.
Hamadi kuna lorry kama mita 50 limezima kati ya barabara na halijaweka alama yeyote. Uzoefu wa dereva ulituokoa lasivyo tusingekuwa duniani leo.
Tulivyofika manyoni mida ya saa 7 hivi tukaamua kulala tu. Hatukuona sababu ya kuwahi tena mjini.
Safari za usiku zinahitaji chombo na dereva imara.
Safari ya usiku hapana binafsi. Kama macho si mazuri, mara umepata dharura au mnyama anakatiza barabarani.
Unafungua madirisha tu! Ile kelele ya upepo huwezi lalaUfunge madirisha tena? Utafia ruvu hapo