Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

Kwa kweli jamani tunakohoa sana tutafuata ushauri wenu, nashukuru sana kwa ushauri wenu
 
Poleni sana, kama unatumia asali, mdalasini na kitunguu saumu walau mara mbili kwa juma, huwezi kupata tatizo hilo.
 
Funika pua yako..unakumbuka Wacko Jacko alipotua Bongo.? Usinywe vinywaji vya baridi sana
 
Sijajua kama tatizo ni uchavuzi wa hali ya hewa Dar au ni nini lakini watu wa Idara ya afya inabidi waangalie hiki kitu tusijekuwa wahanga wa sumu bila kujitambua. .

Hii inatokana na ile milipuko ya mabomu Mbagala na baadaye Gongo la Mboto, ndio maana wana athirika zaidi ni watu wa maeneo haya na karibu. Wizara inaogopa kutoa taarifa msije kuanza kudai fidia wakati hatujamali hata kuwalipa walivunjiwa nyumba.
 
Tumia maziwa fresh glass moja weka kijiko viwili 20mls za asali ya nyuki wadogo , mara mbili kwa siku ,me imemsaidia mtoto wangu. Pia chua na viksi kabla kulala, kifuani na mgongoni.
 
nilifikiri niko peke yangu kumbe tuko wengi, mie nakohoa kuanzi 10 alifajiri kibaridi kikikubali haswaaa, ni siku ya pili leo
 
aisee mwanangu anakohoa kweli usiku.. ana 5yrs yaani ikishafika miga ya kuanzia saa moja usiku ni kukohoa tuuuuu. mpaka anywe dawa ndo kinapona kwa siku hiyo tu kesho yake tena yaani almost two weeks sasa!!!!
 
Ndugu zangu Wana JF,

Mdogo wangu alianza kuwa na ugonjwa huo tangu mwaka 2002, hadi leo ana miaka 20 hajapona, keshatumia dawa za kila aina. Vipi tatizo lake linaweza kuwa ni lipi?

Msaada wenu jamani.
 
MATATIZO YA MAFUA

Kwa wale wenye matatizo ya mafua sugu au ya muda mrefu, wanaweza kupata nafuu au kupona kabisa kwa kutengeneza na kutumia mchangayiko wa asali na mdalasini . Changanya asali kijiko kimoja cha chakula na robo kijiko cha unga wa mdalasini, tumia mara tatu kwa siku.


 
Back
Top Bottom