Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

Discussion in 'JF Doctor' started by BelindaJacob, Jul 31, 2010.

 1. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Dear Doctors,

  Kila nikiamka asubuhi nina mafua na chafya nyingi sana. Yani hii inaniumiza na situmii dawa yoyote kwa mazoea tu.

  Pia muda mwingine kama mchana/ jioni nayapata kutokana na mazingira tofauti kama nikipaka/ nikinusa perfume labda kama nimekaa na mtu jirani, nikifanya usafi kutoa vumbi/ kufagia, nikipigwa na baridi sana au joto kali kweli. Sasa lazima kila siku niwe na mafua.

  Naomba msaada wa kitabibu, maana kila siku lazima niwe na mafua! Inanitesa!

  Asanteni.


  sneeze.jpg  Majibu kutoka kwa wanaJF

   
 2. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Kifupi una-allergy na vumbi + perfume.

  Wakati mwingine mafua husababishwa na sehemu unayoishi, I mean mkoa/jimbo nk. Unaweza ukashangaa mafua yanakoma kabisa pindi utakapohamia sehemu/mkoa mwingine.

  Ushauri
  Tumia COLDAR 1 X 3.

  Ikibidi jaribu kuhamia mkoa mwingine, I assure u kuwa utapona kabisa, vumbi, joto na hata baridi havitakusumbua kabisa.
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nami nilikuwa na tatizo kama lako Konyagi pekee ilinitatulia hilo tatizo sugu.
   
 4. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mawazo yako bwana F80 nina wasiwasi nayo, hiyo tabibu ni mbaya sana, nafikiri mshauri wa kwanza yuko sahihi, jaribu kwenda mkoa mwingine utaona mabadiliko, nami nilikuwa na tatizo hilo hilo, lakini nilipoondoka hayo mazingira nikabadilika kabisa, kama ni mafua yanakuja tu yale ya kawaida kutokana na weather, pole sana, ila jaribu kuhama kidogo,
   
 5. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako kama langu, 100%. Nimetumia lozenges aina nyingi, kila nikienda hospitali nabadilishiwa aina ya dawa. Cha ajabu nikienda mikoani, kwenye vumbi na upepo kama vile Singida, Mbeya, Dodoma napona kabisa.
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Allergies hizo, hata mimi ninazo tafuta Claritine, Clarinese au anti-histamin yoyote huwa zinasaidia.
   
 7. M

  Mubii Senior Member

  #7
  Jul 31, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hata mimi nimepata mafua makali kidogo na kupewa dawa claritine. Nameza dawa hizo leo siku ya tatu. Unameza kimoja tu kwa siku. Inakausha mafua lakini nimejikuta baadae bado napiga chafya kidogo. Natumaini mafua yangu yatakatika within 5 days.
   
 8. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hizo dawa ni vitulizo tu wandugu kwani mzio hauna dawa bali kukaa mbali na vyanzo. Kwako dada nadhani usafi kwako ni tatizo. Kama unaamka asubuhi na mafua cheki na neti na mashuka yako. Usiwe mvivu na usafi
   
 9. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,839
  Likes Received: 20,859
  Trophy Points: 280
  Labda una HAY FEVER,allergy ya pollen... imenisumbua sana the last 2/3 weeks... jaribu kutumia piritize, claritine na dawa nyingine za allergy.
   
 10. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Belinda ningekushauri ukenda hospitali kufanya allergy test halafu utajua ni kitu gani hasa kinakudhuru.

  Mimi mtoto wangu alikuwa kila siku na mafua tukenda kwa Daktari kufanya allergy test na akagunduliwa kuwa anadhurika na manyoya (njiwa, paka.....) na chakula jamii ya kaa (crabs). Nilishangaa sana kuhusu kaa lakini mwenyewe alinithibitishia kwamba anakula akiwa na rafiki zake.
   
 11. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  pole sana , kama wengi walivyo sema inaweza kuwa ni allergy angalia na sabuni unayotumia pia na mambo yote yaliotajwa na wadau hapo juu.


  Nunua air purifier itakusaidia pia.
   
 12. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Asante kaka kwa uchambuzi na ushauri huu,nitajaribu hiyo dawa ya mafua..Nitajitahidi kubadili mazingira nione eneo gani nafuu nihamie mana itakuwa ahueni..je kwa mtazamo wako nihamie mkoa wenye baridi au joto?au inategemea?

  mmh!..tatizo konyagi hata puani haisogei mana harufu kali nalewa.. labda nichanganye na juice..au?!hivi kweli ilikusaidia kutibu au mtego??


  fidel anataka nilewe nahisi..Asante kwa pole&ushauri,sasa uliondoka hayo mazingira moja kwa moja au muda mfupi?nataka nijaribu kuhama nione itakuwaje..

  Pole sana mkuu..Yani mie mwenyewe dawa mpaka nimechoka sijui piriton,celestemine etc..ndo mana siku hizi navumilia yanakuja na kuisha yenyewe..tatizo yamekuwa kama routine,sasa hii inanikosesha raha muda mwingine hadi usiku naamka na flu zinatiririka..
  Nitajaribu kuenda Dom ila na hilo vumbia sijui kama nitasalimika..yani kutabiri ni ngumu!


  Mkuu asante kwa kunielezea,nitazitafuta na hizo dawa nione ipi nitaimudu..nikitibu hii flu itakuwa ahueni sana!!


  ooh pole pia mkuu,nitaicheki hiyo claritine,naona hata Kanga kaitaja kati ya dawa pale kwa bandiko lake..ulipewa hospt?

  siyo nikiwa ndani ya nyumba tu ni mafua ndugu yangu however ushauri wako utazingatiwa!!..situmii neti halafu!!..mashuka nabadili na sina carpet...au hizi perfume na hali ya hewa nazo ni uchafu?!

  Inawezekana la nikacheki na doctor kupata uhakika..pole na wewe,nitazicheki kwa ukaribu hizo dawa na matumizi yake!!

  Ushauri mzuri, nitaenda kituo cha afya na kucheki kwa ukaribu suala hili nipate uvumbuzi..kama ni allergy au la! huo mfano wa mwanao ni dhahiri kuwa mtu unaweza kuwa na tatizo fulani hujui mpaka ukacheki kwa wataalam wa afya..angalau mmepata kumtibu baada ya kucheki kama ana allergy..
   
 13. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Thanx AW,pia umesema sabuni huwa pia inanipa chafya sana huwa nimeshakuwa mchambuzi wa hizo..well,nitatafuta hiyo kitu na kucheki hiyo allergy mku..Asante!!!
   
 14. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Punguza pafyum pengine uko na aleji na pafyums au pua iko sensitive na strong smell . ukiona bado hali mbaya muone mzizimkavu (JF member) akupatie zile dawa zake za porini.
   
 15. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Sawa Dr.Klorokwin itabidi nipunguze perfume au nipulize mbali na pua..sometimes,nikikaa karibu na mtu ana perfume kali mara chafya hizoo na fluu..huyo mzizimkavu nitamtafuta japo sijawahi kutumia dawa za porini!! Asante mkuu!!
   
 16. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  ubarikiwe sana kwa kuniita kwa cheo changu! hiyo avatar inanifanya nikuweke kwenye kundi la VIP patients, ukija dispensary yangu tafadhali usipange queue ingia moja kwa moja chumba cha dr klorokwini.
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Aug 2, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,343
  Trophy Points: 280
  Kwa maelezo yako ya awali hali inayokukabili ni Allergy. Hii inatokana na mwili wako kuwa ''hyper sensitive'' na baadhi ya vitu. Inaweza kuwa ni pollen, manyoya, chemicals[ including perfumes,soap] na hata chakula kama peanuts n.k.

  Kuhamia mkoa au sehemu nyingine si jibu sahihi kwasababu huko uendako vitu vile vile vinavyokusumbua vyaweza patikana. Mathalani kama ni allergy ya vumbi fulani ni ngumu kutambua vumbi hilio na vumbi lipo kila mahali.

  Njia nzuri ni kutafuta kitu gani kina sababisha. Mathalani, unesema ukiwa karibu na perfume, basi jaribu kuepuka vitu hivyo hata kama vipo chumbani kwako. Anza kuondoa ''rule out'' kimoja baada ya kingine na hatimaye utajua kipi kinasababisha. kwanfano, kama unatumia mto wa sufi jaribu kuacha siku moja, kama unatumia sabuni zenye manaukato jaribukutotumia kwa muda fulani.

  Hata vumbi haliwezi kuwa tatizo peke yake mpaka kuwe na allergen, yaani vumbi lenye kile mwili usichokipenda. Kwahiyo kama unagodoro la sufi ni wazi kuwa vumbi likichanganyika na sufi utapata allergy, hapa haina maana vumbi ni allergy kwako, bali ni vumbi lenye sufi.

  Muhimu ni kuatafuta kile kinachosumbua na jaribu kukiepuka.

  Ama kwa konyagi nimejaribu kuatafuta ''literature'' hakuna mahali kitu hicho kimetajwa, lakini yaweza kuwa inatumika kama miti shamba,kwahiyo siwezi kuwa na usahihi wake kwa vile sina knowledge ya mitishamba,ingawa ningependa kuwa nayo!!
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  sasa mtoto mzuri kama wewe (as far as avatar is concerned) unasumbuliwa na mafua? pigana nayo aisee maana uzuri huo utakuwa ni wa bure tu
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Pole Belinda mie pia naona kama sasa nasumbuliwa na tatizo kama lako sikuwa nalo ila naona limeanza nina takribani 4 month mafua yanakuja kwa style kama yako.Ila hao wanaokwambia uhame mkoa kama ume-Settle sehemu na mzee utamwambia naomba niamie sehemu nyingine hapa mafua hayaponi???
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Kula kitunguu somu changanya na wali punje moja kutwa mara tatu kila siku ukisha kula kitunguu somu kula ganda la chungwa husaidia kuondowa harufu ya kitunguu somu tumia kwa muda wa siku 21 kishautaniambia hayo matatizo yako yatakuwa yamekwisha ondoka usisahau kusema Asante.
   
Loading...