Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

kula kitunguu somu changanya na wali punje moja kutwa mara tatu kila siku ukisha kula kitunguu somu kula ganda la chungwa husaidia kuondowa harufu ya kitunguu somu tumia kwa muda wa siku 21 kishautaniambia hayo matatizo yako yatakuwa yamekwisha ondoka usisahau kusema Asante.

Wali punje moja:confused2: ebanee!!!
 
Nguruvi3

Itabidi nifanye uchambuzi wa vitu kimoja baada ya kingine na kuweka kando vinavyonisumbua..Mkubwa nashukuru kwa ushauri mzuri!
kwa sababu hata harufu ya pilipili kichaa inanipa mafua makali sana tena kama ninatengeneza chachandu ya kupika kama unaijua. Kwahiyo ni wazi kuwa nina allergy na vitu kadhaa sina budi kuviepuka..

Again,nashukuru mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Pole Belinda mie pia naona kama sasa nasumbuliwa na tatizo kama lako sikuwa nalo ila naona limeanza nina takribani 4 month mafua yanakuja kwa style kama yako.Ila hao wanaokwambia uhame mkoa kama ume-Settle sehemu na mzee utamwambia naomba niamie sehemu nyingine hapa mafua hayaponi???

Nashukuru mpendwa Firstlady1..mie mwenyewe kuhusu kuhama naona ni ngumu tena kama una familia na majukumu yapo based na mnapoishi sasahivi..vizuri tu nikujua pia vitu amavyo vinakusababishia mafua na kupima allergy ili kuviepuka!..mafua yangu mie ikiwa baridi sana au joto sana au vumbia kali yanatiririka sasa nitahamia wapi?!
Pole na wewe, jaribu kwenda hospitali kufanya check-up na pia kuangalia vitu gani vinakupa madhara ya flu hiyo, unaweza kuvi-list chini na kuvifanyia kazi..
 
ubarikiwe sana kwa kuniita kwa cheo changu! hiyo avatar inanifanya nikuweke kwenye kundi la VIP patients, ukija dispensary yangu tafadhali usipange queue ingia moja kwa moja chumba cha dr klorokwini.

Na hilo jina lako Doctor ndo mana cheo hakipotei..nipo mfungo avatar nimeweka kando ila naomba niwe VIP still kwa dispensary yako, nitakuja keshokutwa..Ushauri wako umezingatiwa!!!
 
kula kitunguu somu changanya na wali punje moja kutwa mara tatu kila siku ukisha kula kitunguu somu kula ganda la chungwa husaidia kuondowa harufu ya kitunguu somu tumia kwa muda wa siku 21 kishautaniambia hayo matatizo yako yatakuwa yamekwisha ondoka usisahau kusema Asante.

Mzizimkavu hiyo punje moja ni moja kweli ya mchele au?du!..hebu subiri nijaribu nikupe feedback..ila sijawahi kula ganda la chungwa, lina utamu kweli?hii tiba si mchezo..
Asante sana lakini kwa hii tiba!!:confused2:
 
Mzizimkavu hiyo punje moja ni moja kweli ya mchele au?du!..hebu subiri nijaribu nikupe feedback..ila sijawahi kula ganda la chungwa, lina utamu kweli?hii tiba si mchezo..
Asante sana lakini kwa hii tiba!!:confused2:
Kitunguu Somu punje moja sio wali kisha ule hilo ganda la Chungwa linasaidia kwa kutowa harufu ya hiyo kitunguu somu.
 
Fanya mazoezi,cheki minyoo, au pima afya yako (body check up) hata mimi nilikuwa na hilo tatizo nilipopima nikakutwa nina fungus kwenye damu nakumbuka ilinisumbua sana hiyo hali, nikapigwa sindano fulani siikumbuki, mbona nilipona hadi leo toka 2007. Kwa hiyo jaribu kucheck hiyo kitu.

Uko mitaa/mkoa gani?
 
attachment.php
Kitunguu swaumu tangu kale kimekuwa kikijulikana kama 'dawa ya kushangaza' na kutumiwa na watu wengi katika kutibu mafua na influenza. Miongoni mwa faida za kitunguu swaumu ni kuzuia kupatwa na magonjwa mbalimbali na maambukizo ya virusi.

Hivyo kitunguu swaumu hujulikana kama antibiotiki ya asilia. Uchunguzi umeonyesha kwamba kula kitunguu swaumu kunapunguza kushadidi ugonjwa wa influenza na hata kuzuia kupatwa na ugonjwa huo. Vilevile kula kila mara kitunguu swaumu, huzuia kupatwa na magonjwa ya moyo, kwani kitunguu swaumu huzuia damu isigande kwenye mishipa ya damu.

Halikadhalika kitunguu swaumu ambacho pia ni kiungo muhimu cha chakula kina potassium, na hivyo watu wenye ugonjwa wa shinikizo la damu wanashauriwa kula vyakula vilivyopikwa kwa kitunguu swaumu.

Si vibaya kujua kuwa katika uchunguzi uliochapishwa mwaka 2001, imeelezwa kwamba, kitunguu swaumu kina athari kubwa na nzuri pale kinapochanganywa na baadhi ya dawa nyinginezo katika kutibu Ukimwi au HIV.

Haya shime jamani… kuanzia leo vyakula visikose kuungwa na kitunguu thomu, iwapo unaogopa kupatwa na influenza kama mimi!
 
...mnh, pole sana.

Matatizo mengi yanayodhaniwa ni allergy utakuta ni psychological zaidi.
Binafsi naamini nikigusa tu pilipili manga huwa ni chafya na mafua mfululizo hata kama nitafanya kila juhudi 'vumbi' lake lisifike puani.
Miaka ya nyuma, kulala na feni ilikuwa ni kasheshe... lakini sasa aaah, nilijiambia itawezekana na imewezekana japo nikiamka chafya zitakuwepo japo si ki vile.

Try meditation,...kidogo kidogo uta conquer hilo tatizo.
It's all in your brain, hata kama hutapoa kabisa utapata nafuu.
 
Pole sana Belinda. Hata hivyo naona umepewa shule ya nguvu-prevention + cure!
 
kitunguu somu punje moja mkuu sio wali

OOh..nimekusoma vizuri sasa mkuu pia kitunguu swaumu nakulaga hata kwa kuchanganya na chakula ili nipate hamu ya kula mana mara nyinginen nakuwa sijisikii kabisa kula..nimevizoea kwahiyo navila tu..ila hilo ganda la chungwa nimeshindwa kabisa, chungu wayiiiii!!


Fanya mazoezi,cheki minyoo, au pima afya yako (body check up) hata mimi nilikuwa na hilo tatizo nilipopima nikakutwa nina fungus kwenye damu nakumbuka ilinisumbua sana hiyo hali, nikapigwa sindano fulani siikumbuki, mbona nilipona hadi leo toka 2007. Kwa hiyo jaribu kucheck hiyo kitu.

Uko mitaa/mkoa gani?

Mkuu asante kwa jambo hili, zaidi ya kucheki aleji basi nitafanya na general check-up ya afya yangu mana kiukweli sifanyagi hii kila mara bali mara moja kwa mwaka!..niko mitaa ya kanda ya kati,Dom huku ni full upepo..


...mnh, pole sana.

Matatizo mengi yanayodhaniwa ni allergy utakuta ni psychological zaidi.
Binafsi naamini nikigusa tu pilipili manga huwa ni chafya na mafua mfululizo hata kama nitafanya kila juhudi 'vumbi' lake lisifike puani.
Miaka ya nyuma, kulala na feni ilikuwa ni kasheshe... lakini sasa aaah, nilijiambia itawezekana na imewezekana japo nikiamka chafya zitakuwepo japo si ki vile.

Try meditation,...kidogo kidogo uta conquer hilo tatizo.
It's all in your brain, hata kama hutapoa kabisa utapata nafuu.

Mbu, asante sana xxx
Nina appointment na doctor hivyo nitapata jibu mana nijue kama ni allergy au basi tu vitu vingine.
Pia kulala na feni nilikuwa nikiamka asubuhi ni full chafya ila usiku usingizi mzuri tu tena kama kuna joto.
sasa unanishauri nifanye Yoga?ha ha..okay,ushauri utazingatiwa mana mbele ya afya yangu nitajitahidi kwa lolote mana ni muhimu sana..


Pole sana Belinda. Hata hivyo naona umepewa shule ya nguvu-prevention + cure!

Ubarikiwe Buchanan..Yani darasa nimekuwa zuri sana,jf doctor kiboko!..nasubiri na kusikia toka kwa docta...Thanx!!
 
Pole Belinda kwa flu ya kila siku.

Nafahamu sana jinsi inavyokera.

Kuna natural juice inaitwa Berry Nectar na anti- allergy tablets zaitwa Bee Pollen zitakusaidia kabisa.

Ukizihitaji nitafute through my email stronglife101@gmail.com
 
Ushauri wangu ni kwenda kucheki kwanza hapa Regency hospital wana vipimo vizuri sana.
 
Mimi nina ndugu yangu, ana tatizo kama hilo, hana mafua ile ya sana lakini akizinduka tu usingizini, hasa mishale ya saa 9 usiku na kuendelea hadi asubuhi, lazima apige chafya za nguvu na nyingi, hadi makamasi yamtoke kibao ndo anasikia ka-unafuu.

Ameshaenda kucheki hospitali (Agakhan na Mikocheni) kama ambavyo wengi wameshauri na ikaonyesha tatizo lake ni alergy na inasababishwa na 'vijidudu vinavyopatikana ktk vumbi la ndani ya nyumba', mfano nguo zilikokaa mahali muda mrefu, vumbi la godoro, alichoambiwa na Dr ni kwamba tatizo lake halina tiba, dawa ni za kutuliza tu. Sijui mpaka hapo atasaidikaje?
 
Njia Rahisi za Kiasili za Kutibu Mafua

Mafua ni ugonjwa unaosumbua watu kila mwaka, hasa yanapoanza kutokea mabadiliko ya hali ya hewa, kutoka msimu wa joto kuingia baridi au kutoka msimu wa kiangazi kuingiza masika. Ili kujikinga na ugonjwa wa mafua, ni lazima mwili uwe na kinga ya kutosha.

Orodha ya vyakula vifuatavyo vimeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili na kupambana na maambukizi mengine kwa kuwa na kiasi kikubwa cha protini na virutubisho vingine.

SUPU YA KUKU
tian_qi_chicken_soup%5B1%5D.jpg


Supu ya kuku wa kienyeji inaelezwa kuwa na virutubisho vinavyosaidia kupunguza utokaji wa makamasi. Utapata virutubisho vingi zaidi ukitengeneza supu ya kuku kwa kuchanganya na mboga za majani. Weka chumvi kiasi kidogo katika supu hiyo.

VITUNGUU SAUMU
vegetable_a_176.jpg


Vitunguu saumu vina kirutubisho aina ya ‘allicin’ ambacho kina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza. Kitunguu saumu kinatoa kinga halikadhalika kinapunguza muda wa mtu kuumwa na mafua. Tumia kitunguu hicho kwa kupika kwenye chakula au kwa kutafuna punje zake.

CHAI
Tea1.jpg

Chai, hasa ya kijani, (green tea) ina virutubisho vya kuimarisha kinga ya mwili. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani (Journal of the American College of Nutrition) umeonesha kuwa watu wanaotumia chai kwa mpangilio maalum hawasumbuliwi mara kwa mara na mafua pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza, huwa salama na mafua au siku za kuumwa mafua hupungua kwa asilimia 36 ukilinganisha na wale wasiokuwa na kinga imara.

Hata hivyo, tahadhari inatolewa kwa watoto wa shule kutokupewa kiasi kingi cha chai kwa siku. Unywaji wa kikombe kimoja kwa siku kwa mtoto wa shule siyo mbaya. Kwa mtu mzima, asizidishe vikombe vitatu kwa siku. Ikumbukwe kuwa chai inapotumika kwa wingi kupita kiasi, huweza kusababisha pia tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu. Kunywa kiasi kwa afya yako.

MACHUNGWA, PILIPILI KALI

oranges.jpg
Chili_Pepper_Final.jpg
Utafiti unaonesha kwamba ulaji wa vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi kila siku husaidia kuondoa au kuzuia ugonjwa wa mafua. Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin C ni pamoja na machungwa, mboga za majani aina ya Brokoli na pilipili kali.
Ili kupata kiasi kingi cha Vitamin C, inashauriwa machungwa yaliwe pamoja na nyama zake za ndani au kunywa juisi yake.

ASALI

honey.jpg

Kama inavyojulikana, asali ni tiba ya matatizo mengi ya kiafya, miongoni mwa hayo ni pamoja na mafua. Asali inasaida kuondoa kikohozi na muwasho kwenye koo. Halikadhalika, asali inaweza kutumiwa na watoto wadogo kama dawa.

Watoto wanaoruhusiwa kutumia asali kama tiba ni wa umri kati ya miaka 2 hadi 5. Hawa dozi yao ni nusu kijiko kidogo cha asali, wenye umri wa miaka 6-11 wapewe kijiko kimoja kidogo na wenye umri kuanzia miaka 12 hadi 18, wapewe vijiko vidogo viwili vya asali wakati wa kulala.

MTINDI

yogurt-410x546.jpg

Kutokana na kiwango kikubwa cha protini ilichonacho, Mtindi ni chakula kingine kinachofaa kuliwa na mtu mwenye mafua ili kupunduza siku za kusumbuliwa na ugonjwa kukohoa.

CHOKOLETI NYEUSI

darkchocolate1.jpg

Wataalamu wanakubaliana kuwa ulaji wa ‘chocolate’ nyeusi (dark chocolate) huimarisha kinga ya mwili, hivyo inapoliwa na mgonjwa wa mafua huweza kumpa ahueni mgonjwa kwa namna moja ama nyingine. Halikadhalika huwa kinga kwa maambukizi mengine.

PWEZA

001.jpg


Samaki aina ya pweza wana virutubisho vingi vya kuongeza kinga ya mwili yenye uwezo wa kupambana na bakteria pamoja na virusi vya mafua. Kiasi kidogo cha pweza, awe wa kukaangwa au kuchemshwa kama supu, anafaa kuliwa mara kwa mara kuimarisha kinga ya mwili.
VIAZI VITAMU
ttar_sweet_potatoes_h.jpg

Kirutubisho aina ya ‘Beta-carotene’ huimarisha kinga ya mwili. Kirutubisho hicho huwa ni muhimu kwa ustawi na uimarishaji wa kinga mwilini na kinapatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu na vyakula vingine kama vile karoti, maboga na mayai, (kiini).

Kwa ujumla, suala la kuimarisha kinga ya mwili ni muhimu kwa afya zetu. Ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu na vingine, unatakiwa kuwa ni wa mara kwa mara kama siyo wa kudumu, kwa sababu mwili unapokosa kinga imara, ni rahisi kushambuliwa na maradhi ya kuambukiza
 
du asante sana ndugu. hii inaonyesha jinsi gani Mungu alivyotuwekea Vyakula sio tu kula na kushiba bali na kutibu afya zetu pia.
 
Back
Top Bottom