Wana JF habari zenyu bana hope mko poa.
Naomba mnisaidie ndg zangu,
Nina MAMA yangu 69 yrz ANAKOHOA like 2 yrz sasa, mwanzo madaktari walisema ni kikohozi cha kawaida akawa anapewa dawa za kawaida tu. Ila mwanzoni mwaka huu madaktari walisema ni Kifua Kikuu akapewa dozi ya kifua kikuu ila problem ikawa akitumia vile vidonge (kwa mda wa miezi mitatu) anakohoa sana kuzidi siku za nyuma, tukaamua kustopisha dozi.
Tatizo huwa anajisikia kuwashwa kooni then atakohoa, ila anapoanza kukohoa anaweza kohoa mfururizo kama dakika 5 hivi nonstop, baada ya kikohozi kukoma tu huwa anajisikia haja ndogo kila baada ya dakika kwa mda wa saa nzima hivi, mkojo wenyewe huwa mdogo tu mda mwingine, na huo mkojo hawezi kuuzuia (kuicontrol ) na akijichelewesha kwenda toilet basi atajikojolea.
Please mtanisaidiaje wanajamii nimsaidie my dearest mom, thanx, i will appreciate.
Chukuwa kitunguMaji menya kata vipande 4 ,, weka katika Asali fresh funika uzuri u weke pembeni kesho yake itatowa maji ,, kama Syrup basi mpe kijiko kimoja mara tatu au mara 4kwa siku inshaallah itamsaidiya .
Katika kila kiungo kuna hekima na siri yake.
Hewa ambayo tunaivuta sisi wanaadam ni hewa yenye vitu tofauti ndani yake kuna maji, oxygen, nitrogen, mvuke n.k kuna ambavyo ni muhimu ndani ya mwili wa mwanaadam na kuna vitu ambayo havina umuhimu wala havihitajiki katika mwili wa mwanaadam.
Lakini tunapovuta hewa, hewa ile huenda moja kwa moja kupitia katika tundu za pua hushuka katika bomba la koo hadi kwenda kwenye mapafu ya mwanaadam. Hewa hiyo haipiti hivi hivi kila sehemu inakuwa na kazi yake maluum.
Ndio maana ndani ya pua utakuta kitu kama maji maji yale ya lugha inaitwa MUCUS mucus kazi yake ni kukamata taka taka na vumbi ambalo linalopita ndani ya mwili wa mwaadam.
Hivyo maradhi ya kifua huwa yanasababishwa na taka taka au vumbi linalopita katika tundu za pua na kuelekea katika mapafu, hii hutokana ikiwa pua itashindwa kusafishwa kila mara hivyo taka hubakia ndani ya pua na pua hushindwa kupokea taka nyengine.
Zabibu: Glassi moja ya zabibu changanya na kijiko kimoja cha asali tumia kwa muda wa wiki, inasemakana zabibu ni burudisho la mapafu.
Kwa wale wenye kifua kikavu basi Inshallah Lozi iwe dawa yao basi alazae lozi saba katika maji usiku wa kucha asubuhi atoe maganda yake ya uzisage uchanganye na siagi kidodo pamoja na sukari kidogo uwe unakula kijiko kimoja kikubwa kila siku asubuhi na jioni.
Maji ya kitunguu maji changanya na kijiko kimoja asali uweke katika chupa kwa muda wa masaa manne hadi matano, uwe unakunywa mara mbili kwa siku.
Kwa kifua kikavu: Chemsha maziwa glassi moja changanya na manjano acha ichimkie na baadae unywe.
Ikiwa kifua cha kuumia kwa kuanguka basi chukua manjano uchanganye na maji ya moto na umpake pale alipoumia.
Ikiwa ni kifua kinachotokana na hali ya hewa ya ubaridi basi uwe unakunywa juisi ya machungwa iliyozimuliwa kwa maji ya moto kila baada masaa mawili.
Pia jaribu kuacha sigara kama ni mvutaji au kukaa karibu na moshi wa aina yoyote ule, pia vitu vikali, nyama, soda pamoja na chai.