Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

Jamani kuna ugonjwa wa kikohozi kikavu sasa hivi umeibuka Dar, fatilia kwenye mikusanyiko ya watu sasa hivi utagundua watu wengi wanapiga "starter" kali kama mara 2 au mara 3 kila baada ya dakika 5. Kwa wale ambao imeshawatokea (Nikiwa mmoja wao) ugonjwa huu unatesa sana muda wa kulala. Utakuta siku nzima unafanya kazi vizuri tu lakini ukishalala unajikuta unakohoa vibaya sana, bila kutoa hata makohozi na unaendelea hivyo mpaka asubuhi.

Sijajua kama tatizo ni uchavuzi wa hali ya hewa Dar au ni nini lakini watu wa Idara ya afya inabidi waangalie hiki kitu tusijekuwa wahanga wa sumu bila kujitambua. Na kwa yeyote anaefahamu tiba yake naomba atujuze manake dawa za kawaida kama koflyn, coldrill hazifanyi kazi kabisa.
 
ni kweli kabisa watu wanakohoa sana, ukienda Dispensaries, health centres, hospitals unawakuta asilimia kubwa watoto wanakohoa. Afya tusaidieni
 
ni kweli kabisa watu wanakohoa sana, ukienda Dispensaries, health centres, hospitals unawakuta asilimia kubwa watoto wanakohoa. Afya tusaidieni

Dah watoto ndo utawahurumia wakiwa wanakohoa, nadhani tuna tatizo kubwa ambalo hatujalishtukia.
 
Jamani kuna ugonjwa wa kikohozi kikavu sasa hivi umeibuka Dar, fatilia kwenye mikusanyiko ya watu sasa hivi utagundua watu wengi wanapiga "starter" kali kama mara 2 au mara 3 kila baada ya dakika 5. Kwa wale ambao imeshawatokea (Nikiwa mmoja wao) ugonjwa huu unatesa sana muda wa kulala. Utakuta siku nzima unafanya kazi vizuri tu lakini ukishalala unajikuta unakohoa vibaya sana, bila kutoa hata makohozi na unaendelea hivyo mpaka asubuhi.

Sijajua kama tatizo ni uchavuzi wa hali ya hewa Dar au ni nini lakini watu wa Idara ya afya inabidi waangalie hiki kitu tusijekuwa wahanga wa sumu bila kujitambua. Na kwa yeyote anaefahamu tiba yake naomba atujuze manake dawa za kawaida kama koflyn, coldrill hazifanyi kazi kabisa.

Mkuu nipo Arusha lakini hata mimi jumamosi kuamkia Jumapili niliingia kitandani safi kabisa na nilipoanza kuutafuta usingizi nikaanza kukohoa bila kutoa kitu na nakumbuka nilienda hadi saa 8 usiku nikikohoa. Nilipoamka asubuhi nikawa mzima ila hiki kikohozi ni kikavu hata hapa ninapoandika natembea na ZECUF mfukoni ingawaje hazisaidii kama ulivyosema.

Sijajua ni upepo gani unakatiza katika nchi.
 
Kaka same here, nimetumia syrup zaidi ya 2 hadi zinaishia kuniletea usingizi. Wasiwasi wangu isijekuwa kuna uchavuzi wa hali ya hewa umefanyika bila sisi kujua.
 
Kaka same here, nimetumia syrup zaidi ya 2 hadi zinaishia kuniletea usingizi. Wasiwasi wangu isijekuwa kuna uchavuzi wa hali ya hewa umefanyika bila sisi kujua.

ni kweli kabisa,hata mimi yamenikuta watoto wangu wakikohoa sana kipindi cha usiku lakini cha kushangaza mchana hutawasikia,
inawezekana kabisa kuna uchafuzi wa hali ya hewa either kwa moshi wa sumu au vumbi la barabarani kwa watu tunaoishi kwenye barabara zinakojengwa
 
Mkuu nipo Arusha lakini hata mimi jumamosi kuamkia Jumapili niliingia kitandani safi kabisa na nilipoanza kuutafuta usingizi nikaanza kukohoa bila kutoa kitu na nakumbuka nilienda hadi saa 8 usiku nikikohoa. Nilipoamka asubuhi nikawa mzima ila hiki kikohozi ni kikavu hata hapa ninapoandika natembea na ZECUF mfukoni ingawaje hazisaidii kama ulivyosema.

Sijajua ni upepo gani unakatiza katika nchi.

Nilikwenda kumtembelea mtoto shuleni (boarding) nikamkuta hoi na kikohozi, nilipochunguza nikagundua nusu ya wanafunzi shuleni wanakohoa vibaya sana.

Jaribuni kutumia mchanganyiko wa asali mbichi, mdalasini na maji ya moto.
 
Nadhani tatizo litakuwa ni uchafuzi wa hewa, vumbi na moshi wa magari..
 
Jamani kuna ugonjwa wa kikohozi kikavu sasa hivi umeibuka Dar, fatilia kwenye mikusanyiko ya watu sasa hivi utagundua watu wengi wanapiga "starter" kali kama mara 2 au mara 3 kila baada ya dakika 5. Kwa wale ambao imeshawatokea (Nikiwa mmoja wao) ugonjwa huu unatesa sana muda wa kulala. Utakuta siku nzima unafanya kazi vizuri tu lakini ukishalala unajikuta unakohoa vibaya sana, bila kutoa hata makohozi na unaendelea hivyo mpaka asubuhi. Sijajua kama tatizo ni uchavuzi wa hali ya hewa Dar au ni nini lakini watu wa Idara ya afya inabidi waangalie hiki kitu tusijekuwa wahanga wa sumu bila kujitambua. Na kwa yeyote anaefahamu tiba yake naomba atujuze manake dawa za kawaida kama koflyn, coldrill hazifanyi kazi kabisa.
Duh hapo kwenye blue kali sana, Ila dawa ni kunywa maji (sii ya baridi) utaendelea na usingizi nyororo kama kwaida hata kama ni mtoto mpatie kitasimama! ila maumivu yakizidi muone daktari!
 
Nilikwenda kumtembelea mtoto shuleni (boarding) nikamkuta hoi na kikohozi, nilipochunguza nikagundua nusu ya wanafunzi shuleni wanakohoa vibaya sana.

Jaribuni kutumia mchanganyiko wa asali mbichi, mdalasini na maji ya moto.

Kaka asante kwa ushauri wako nimeshanunua chupa ya asali mbichi nasubiri kwenda kufanya hiyo mixa nyumbani.
 
Duh hapo kwenye blue kali sana, Ila dawa ni kunywa maji (sii ya baridi) utaendelea na usingizi nyororo kama kwaida hata kama ni mtoto mpatie kitasimama! ila maumivu yakizidi muone daktari!

Nimejaribu sana mkuu kila nikiamka nagonga glasi kadhaa lakini haijasaidia ndo maana nikaamua kuipost hapa, nataka nijaribu tiba mbadala aliyoitoa mwanajamvi mmoja hapa nahisi inaweza kunipa ahueni.
 
Nadhani hii imesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Watu wengi wanadai Dar kuna "Baridi" ya hapa na pale imebidi wengine hata wakaibue makoti yao ya "ja........" 🙂...Kunywa maji ya yenye moto kiasi na kujisugua na vicks sehemu za shingoni na mgongoni wakati unaenda kulala husaidia sana.
 
Mkuu ni kweli. Hii hali hata huku kwetu mikoani ipo sana.Ukitembea barabarani utakutana ma makohozi mazito yenye rangi ya njano yametapakaa pembeni (yanaleta kinyaa lakini hamna jinsi)! Huenda ndiyo athari za kuvuja kwa mitambo ya nuklia ya Fukushima!
 
Nilikwenda kumtembelea mtoto shuleni (boarding) nikamkuta hoi na kikohozi, nilipochunguza nikagundua nusu ya wanafunzi shuleni wanakohoa vibaya sana.

Jaribuni kutumia mchanganyiko wa asali mbichi, mdalasini na maji ya moto.

Suala hapo ni upatikanaji wa hiyo asali mbichi,kuna jamaa maeneo ya ubungo wanauza eti ni asali mbichi lakini ni full kuchakachuliwa.
 
Vumbi mara nyingi hua linasababisha kikohozi cha aina hiyo....muhimu kubhwa maji ili kulainisha koo na kuondoa chembe chembe za uchafu kama zipo.
 
yaaaani
watu tunaugua huku wahusika wamelala kabisa

utasema kuna sumu imeenea
 
Kutakuwa na virus anatembea, of cause mabadiliko ya hali ya hewa yanamchango.Na hivi waswahili hatuna utamaduni wa kuziba midomo tunapokohoa, so virus wanakuwa wengi kwenye hewa!
 
Yaani hili ni tatizo kubwa sana hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa ila kuna mpishano wa aina ya makohozi, makohozi yanayotoka yakiambatana na kuumwa kifua kwa ndani unapokohoa unaweza ukatafuta amplyciline ukameza huku ukitumia pia na cofta!kwa makohozi ya ndani ambayo unasikia yapo lkn hayatoki chukuwa kwanza maji ya chumvi sukutua vzr kbs thn katafute amoxline itasaidia ila kwa wagonjwa wote wa kifua ukitoka kazini nenda straight hm pumzika kama ni mwanafunzi pia hvy hvy haifai kuzungukazunguka hasa mida ya jioni ukifanya hvy usiku itakuwa tabu
Thanx poleni kwa kuumwa!
 
Tumia bidhaa za Aloe Vera na Honey bee

Aloe Vera barbadensis ambazo zimethibitishwa na International Aloe Vera Science.

Try: FOREVER ECHINACEA SUPREME

Huongeza Kinga ya Mwili, Huzuia Vikohozi na mafua na majipu, kiungulia,vidonda vya tumbo, magonjwa ya ngozi.

GARLIC THYME

mafua, chunusi na fangasi

FOREVER BEE PROPOLIS: Hii ndo dawa haswaaa

pumu, mafua,kifua,koo,na huongeza kinga ya mwili

Haya haya, pia kuna bidhaa nyingine nzuri original za Aloe Vera

Kuna Aloe Vera gel.

-Huondoa sumu mwilini
-husaidia chakula kuyeyuka vizuri (digestion)
-wagonjwa wa kisukari
-presure
vidonda vya tumbo
na huongeza kinga ya mwili (improves immunity.

Contact or read more here

ALOE VERA AND HONEY BEE DISTRIBUTOR ( CHAMPION) APPROVED BY FOREVER LIVING - USA
 
Ni kweli watoto wetu wanapata shida sana! Maji yanasaidia kiasi.
Kuna hisia kuwa huu MOSHI wa majenereta yaliyotapakaa sasa kwa kukosekana umeme ni moja ya chanzo cha uchafuzi wa hali ya hewa.

Je kuna utafiti na ukweli juu ya hilo wana JF?
 
Back
Top Bottom