Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

Ushauri: Tiba ya kikohozi na mafua

hata mimi ni muathirika wa tatizo hilo tokea 2002 pia. ila hivi karibuni tu nimevumbua dawa kwa kweli ni msaada tosha kwa wale wote wenye matatizo hayo na yanayofanana na hayo. Nenda katika maduka makubwa ya dawa then ulizia NASAL PRAY huwa inatumika kublow tundu za pua na kwa kweli ni msaada. mimi natumianasal spray inaitwa AVAMYS ila kama hamna hii chukua yoyote na itamsaidia Inshaallah.
 
Mwambie ajaribu kutumia Kitunguu thomu

Kitunguu swaumu tangu kale kimekuwa kikijulikana kama 'dawa ya kushangaza' na kutumiwa na watu wengi katika kutibu mafua na influenza. Miongoni mwa faida za kitunguu swaumu ni kuzuia kupatwa na magonjwa mbalimbali na maambukizo ya virusi. Hivyo kitunguu swaumu hujulikana

kama antibiotiki ya asilia. Uchunguzi umeonyesha kwamba kula kitunguu swaumu kunapunguza kushadidi ugonjwa wa influenza na hata kuzuia kupatwa na ugonjwa huo. Vilevile kula kila mara kitunguu swaumu, huzuia kupatwa na magonjwa ya moyo, kwani kitunguu swaumu huzuia damu isigande kwenye mishipa ya damu.

Halikadhalika kitunguu swaumu ambacho pia ni kiungo muhimu cha chakula kina potassium, na hivyo watu wenye ugonjwa wa shinikizo la damu wanashauriwa kula vyakula vilivyopikwa kwa kitunguu swaumu.

Si vibaya kujua kuwa katika uchunguzi uliochapishwa mwaka 2001, imeelezwa kwamba, kitunguu swaumu kina athari kubwa na nzuri pale kinapochanganywa na baadhi ya dawa nyinginezo katika kutibu Ukimwi au HIV.
Haya shime jamani… kuanzia leo vyakula visikose kuungwa na kitunguu thomu, iwapo unaogopa kupatwa na influenza kama mimi!

IKIWA BADO HAJAPONA JARIBU KUWASILIANA NA MIMI KWA NJIA YA P.M. NIPO NJE YA NCHI NAWEZA KUKULETEA DAWA IKAMSAIDIA HUYO MGONJWA WAKO.
 
<br />
<br />
utani huu mkuu
hata mi nilishangaa sana lakini sasa naanza kuamini baada ya maelezo ya Mzizimkavu

Wadau naomba kujulishwa ni dawa gan inaweza ikamaliza kikohozi cha kubanja (japokuwa ni kiangaz na kuna vumbi) nilienda hospital wakanipa amoxlin na mess nikamaliza lakin bado nabanja nikashauriwa kutumia tangawiz kuwa inalainisha makoozi na unamaliza kubanja lakini bado je nifanyaje?
 
Kwa wiki sasa ninasumbuliwa na kikohozi kikavu kisicho na makohozi. Nimetumia Antibacteria na syrups sijaona dalili za kupona, naomba ushauri wenu?
 
Hivi na wewe una shida ka yangu? Mi pia nina ka wiki ivi. Yaani nakohoa ile mbaya lakini kikohozi hakitoki. Nimetumia dawa lakini ndo hivyo tena wala hakijigusi. Tuendelee kusubiri wataalamu wako hapa hapa.
 
Kwa wiki sasa ninasumbuliwa na kikohozi kikavu kisicho na makohozi. Nimetumia Antibacteria na syrups sijaona dalili za kupona, naomba ushauri wenu?

Nami pia nasumbuliwa kama wewe hii sasa ni wiki ya pili yaani sioni makohozi yakitoka ila nikikohoa nasikia ila hayatoki. Pia ninachoka ile mbaya. Mwenye ushauri atoa msaada
 
Daktari ni wajibu kuwaona na nimeshapita huko hata hizo dawa nilojaribu ni zakuambiwa na madaktari, lkn wajua watu huzidiana kulingana na cases. Ushauri ninaohitaji ni kufikia tiba halisi. Nimechunguza pia nakuwaona hospital wengine wenye matatizo kama haya, wakihangaika.
 
Lamba asali mbichi ya nyuki wadogo, mimi huwa inanisaidia sana kwenye kikohozi kikavu sababu huwa nakohoa hadi koo lauma sana.
 
Lamba asali mbichi ya nyuki wadogo, mimi huwa inanisaidia sana kwenye kikohozi kikavu sababu huwa nakohoa hadi koo lauma sana.

Ni kweli hata mimi nilitumia ikanisaidia sasa mwaka na nusu sijawahi pata tena. Lakini tafuta majani ya chai chemsha kwaenye maji. Chai iwe nzito (yaani na majani mengi) halafu weka asali unywe mara tatu kwa siku, kijiko kimoja tu kikubwa. kesho yake umepona.

Hata hivyo changu kilikuwa na makohozi na kubanja. Nilikuwa na mafua pia
 
Chukua pingili za vitunguu saumu 7 chemchia kwenye grass i ya maziwa acha yapoe kunywa na vile vitunguu saumu tafuna
 
Kama kikohozi kina dalili hizi:
  • Kikavu
  • Hakiumizi kifua
  • Hakiambatani na homa
  • Unasikia kuwashwa kooni
  • Unakohoa zaidi asubuhi au/na usiku
Basi hicho kikohozi ni cha allergy, siyo cha infection. Moja wapo ya dawa ambazo zinasaidia ni Phernagan syrup (scientific name: promethazine). Kunywa kijiko kimoja cha chai usiku unapolala, ikwezekana hata asubuhi. Hii dawa inaweza kuleta drowsiness.

Nipe feedback
 
Mheshimiwa kwa maelekezo yako nimepata kupona, yaonekana ni allergy km ulivyosema. Dawa hiyo imenisaidia sana.
 
Jamani,

Mimi nina allergy na perfume, spray na mafuta ya taa. Yani hivyo vitu vikiwa karibu yangu tu, usiku napata tabu ya kupumua.

Nisaidieni dawa na ushauri.
 
nenda sister consolata mbagala mission muone dk isaya mwisho wa matatizo yako
 
Uzio au allergy kama wengi wetu tunavyofahamu husababishwa na vitu mbalimbali ikiwemo ulivyo vitaja hapa. Kikubwa ni jujiweka mbali na hivyo vitu vinavyoweza kutriger reaction.

Kama alivyosema msemaji kumwona mtaalamu ni muhimu ili vile dawa atakazokupa natumaini anti allergy itabidi akupe zile ambazo hazileti usingizi ila nakushauri utumie kwa muda mrefu kidogo miezi mitatu mfululizo ile uweze kusuppress allegic mediators ulizonazo ndio maana nakushauri uende kwa dr ili aweze kuangalia hali yako. anaweza kukupatia nasal spay ili iweze kukusaidia. Ni hayo tu kwa sasa

Wana JF habari zenyu bana hope mko poa.
Naomba mnisaidie ndg zangu,

Nina MAMA yangu 69 yrz ANAKOHOA like 2 yrz sasa, mwanzo madaktari walisema ni kikohozi cha kawaida akawa anapewa dawa za kawaida tu. Ila mwanzoni mwaka huu madaktari walisema ni Kifua Kikuu akapewa dozi ya kifua kikuu ila problem ikawa akitumia vile vidonge (kwa mda wa miezi mitatu) anakohoa sana kuzidi siku za nyuma, tukaamua kustopisha dozi.

Tatizo huwa anajisikia kuwashwa kooni then atakohoa, ila anapoanza kukohoa anaweza kohoa mfururizo kama dakika 5 hivi nonstop, baada ya kikohozi kukoma tu huwa anajisikia haja ndogo kila baada ya dakika kwa mda wa saa nzima hivi, mkojo wenyewe huwa mdogo tu mda mwingine, na huo mkojo hawezi kuuzuia (kuicontrol ) na akijichelewesha kwenda toilet basi atajikojolea.

Please mtanisaidiaje wanajamii nimsaidie my dearest mom, thanx, i will appreciate.
 
Pole sana rafiki, mungu atamsaidia atapona. Jaribu kumpa asali mbichi, ikichanganywa na juice ya limao. Mara 3 kwa siku.
 
Back
Top Bottom