Ushauri: Ripoti ya CAG isirudiwe tena kusomwa hadharani, inatia hasira na kuleta manung'uniko, wanaotuhumiwa hawajawahi kukamatwa

Mimi Huwa naishangaa jamhuri!!hivi Kuna nini huko jikoni has!?Kuna makubaliano gani hasta kati ya nyie na Rais aliepo madarakani!!?

Huwa mnamwachia nchi aiamue kama familia yake!!?hakuna mstari unaochorwa asivuke!!?

Sasa KAZI ya Cag ni nini!?mbona ripoti hazifanyiwi kazi!!?

Yaani Tatizo Huwa ni nini!!?
Njoo vile TZ ifanane na US kimfumo Ila US sio TZ
 
Ibaki kuwa siri ya Rais na watu wake baasi, maana kiukweli pamoja na madudu yote yanayoanikwa lakini hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua.

Zaidi ya kuleta manung'uniko na hasira kwa wananchi, hakuna lolote linalofanyika , kuna haja gani sasa ya kutupotezea muda kuangalia na kusikiliza ripoti hiyo?

Acha waendelee kujitafunia mihela yetu ya bure watakavyo waendelee kutuongopea kwamba bado Nchi yetu ni Changa.

Tunawatakia Kila la heri katika ulaji huo wa Nchi.

Kwa sababu hakuna anayekamatwa kwa kula fedha za umma kutokana na Report mbalimbali za huko nyuma mm nadhani CAG yuko sahihi kabisa kwa alichokifanya leo yaani kusifu tu kwamba wizi haupo,kwa sababu hata akisema huo wizi upo,ni nani atakaye fuatilia hakuna chochote kitachofanyika ni wastage of time tu.CAG amechagua upande ambao mama anaupenda nao ni wizi hakuna.
 
Aibu kubwa sana
 
Matamanio ya walio wengi ni kuona wanaofanya au waliofanya ufujaji, ubadhirifu na ufisadi wa fedha za umma wanawajibishwa.

Iweke hii akilini kuwa "Jinai haina umauti". Ipo siku watafikiwa.
Wanafalsafa wanatuambia: in the long run we’re all dead! Hiyo siku ya kuwajibishwa hao mafisadi itakuwa na maana endapo tulioshuhudia na kuathirika na maovu yao tutaiona. Nje ya hapo tutakuwa tumetapeliwa na kufanywa mazuzu wa karne.

Inaonekana viongozi wa CCM wanatumia mkakati wa kusukuma muda. Wanafanya kila hila kukatisha tamaa (frustrate) wakosoaji na wapinzani wakielewa kuwa baada ya muda watazeeka na kuchoka na kukaa pembeni. Vijana wao nao wataendeleza hiyo vicious circle wakizidi kutoa ahadi za uongo kwa wananchi kusukuma muda kuendeleza utawala wa kifisadi milele.

Nakumbuka mwanzo wa vyama vingi milango ilipofunguliwa, wapinzani wa Nyerere kina Kambona, Tumbo na Fundikira walijitokeza kuanzisha vyama vya siasa. Siku moja Nyerere alikutana na mmojawao akatabasamu na kumwambia “bwana wewe ndio unataka kuingia kwenye haya mambo leo hii? Wenzio tulishaachana nayo zamani!” Ilikuwa kama kejeli hivi.

Nikakumbuka kusoma jinsi Nyerere alivyosafisha uwanja wa siasa enzi zake na kubaki mwenyewe huku “maadui” zake hatimaye wakiishiwa nguvu na kutawanyikia kusikojulikana. Kisha wakajaribu kuinuka tena bila mafanikio. Bila kujua kwamba it was too late. Nikasema: Indeed, the world is not fair.

Sasa naona mafisadi wa CCM nao wanatumia janja ya muda wakiamini watadanganya vizazi na vizazi vya Watanzania kwa mafanikio. Msiwe na wasi wasi. Kuweni na subra. CCM haina mchezo na mafisadi. Ipo siku watashughulikiwa kikamilifu!
 
Ibaki kuwa siri ya Rais na watu wake baasi, maana kiukweli pamoja na madudu yote yanayoanikwa lakini hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua.

Zaidi ya kuleta manung'uniko na hasira kwa wananchi, hakuna lolote linalofanyika , kuna haja gani sasa ya kutupotezea muda kuangalia na kusikiliza ripoti hiyo?

Acha waendelee kujitafunia mihela yetu ya bure watakavyo waendelee kutuongopea kwamba bado Nchi yetu ni Changa.

Tunawatakia Kila la heri katika ulaji huo wa Nchi.

hivi huwa husikii,wapo waliokamatwa na kufikishwa mahakamani,pia ufahamu nchi inaendeshwa kwa kuzingatia sheria,hizo ni audit queries zinatakiwa majibu na serikali huzijibu,na ndipo tunapata zipi ni jinai,zipi ni uzembe na zipi ninafutwa
 
Ibaki kuwa siri ya Rais na watu wake baasi, maana kiukweli pamoja na madudu yote yanayoanikwa lakini hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua.

Zaidi ya kuleta manung'uniko na hasira kwa wananchi, hakuna lolote linalofanyika , kuna haja gani sasa ya kutupotezea muda kuangalia na kusikiliza ripoti hiyo?

Acha waendelee kujitafunia mihela yetu ya bure watakavyo waendelee kutuongopea kwamba bado Nchi yetu ni Changa.

Tunawatakia Kila la heri katika ulaji huo wa Nchi.

Mimi naona wawe wanatumiana wao kwa wao tu hata kwenye simu zao.

Sisi hayatuhusu
 
Back
Top Bottom