Ushauri: Ripoti ya CAG isirudiwe tena kusomwa hadharani, inatia hasira na kuleta manung'uniko, wanaotuhumiwa hawajawahi kukamatwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,730
218,296
Ibaki kuwa siri ya Rais na watu wake baasi, maana kiukweli pamoja na madudu yote yanayoanikwa lakini hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua.

Zaidi ya kuleta manung'uniko na hasira kwa wananchi, hakuna lolote linalofanyika , kuna haja gani sasa ya kutupotezea muda kuangalia na kusikiliza ripoti hiyo?

Acha waendelee kujitafunia mihela yetu ya bure watakavyo waendelee kutuongopea kwamba bado Nchi yetu ni Changa.

Tunawatakia Kila la heri katika ulaji huo wa Nchi.

FB_IMG_1711640411248.jpg
 
Mimi Huwa naishangaa jamhuri!!hivi Kuna nini huko jikoni has!?Kuna makubaliano gani hasta kati ya nyie na Rais aliepo madarakani!!?

Huwa mnamwachia nchi aiamue kama familia yake!!?hakuna mstari unaochorwa asivuke!!?

Sasa KAZI ya Cag ni nini!?mbona ripoti hazifanyiwi kazi!!?

Yaani Tatizo Huwa ni nini!!?
 
Ukiacha mihemko na hisia hasi kwa kuheshimu taaluma za kikaguzi hutakaa uwaze na kuandika mfano na ulichokiandika.

Hizi ripot zinasaidia sana kukosoa, kurekebisha na kusahihisha njia ambazo hazikuwa sawa hapo awali.

Ukweli huwa na kawaida ya maumivu awali ila ukizoeleka huponya na kufanya kuwa imara. Ipo siku utaona matunda ya hizi ripot na sio vile wewe unavyotaka kwa wakati wako. Kila jambo lina njia yake na wakati wake.

Uishi umri mrefu, uje ujifunze mambo.
 
Wacha ISOMWE labda Watanganyika wataamka,..pia ni WAJIBU wenu CHADEMA,kuchukua haya MAUCHAFU na kuyapeleka kwa wananchi,bara na visiwani,Ukerewe hadi Nanyamba..Ujiji hadi Kwediboma

Kikubwa mtumie LUGHA rahisi ili watanganyika wote waelewe,ni kwa namna gani WIZI huu,unaathiri maisha yao ya sasa na ya vizazi vijavyo!
 
Back
Top Bottom